Tujikumbushe historia ya bakwata october - december 1968 sehemu ya tatu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,268
Hadi kufikia juma la kwanza la mwezi wa Desemba, mikoa mitatu kati ya kumi na saba ilikuwa tayari imeshajitenga kutoka EAMWS.

Kile kikundi cha Adam Nasibu kikaunda kamati kwa ushirikiano na Kamati ya Maulidi ya Dar es Salaam, Adam Nasib akiwa Katibu.

Kamati hii ikaitisha mkutano Ukumbi wa Arnatouglo tarehe 3 Desemba, 1968 kujadilia ‘’mgogoro.’’

Aliyetumiwa kutoa tangazo lile alikuwa katibu wa Kamati ya Maulidi na Swala ya Iddi, Y. Osman.

Kundi la Adam Nasib lilikuwa na mchanganyiko wa watu waliokuwa wanaungwa mkono na serikali Adam Nasib akiwa kiongozi, halikadhalika kulikuwa na Waislam waliokuwa na nafasi katika TANU.

Kuna mambo mengi yamepita katika kipindi hiki si rahisi kuyaeleza yote.

Itoshe kusema tu serikali ilikuwa tayari kuasisi BAKWATA ila ikishindwa kufanya hivyo kwa kumhofia Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Ili kuitisha mkutano wa kuasisi BAKWATA lazima Sheikh Hassan bin Ameir awepo kwenye mkutano huo na akiwepo haitawezekana kulifanya hilo kwani wazi atalipinga tena hadharani.

Ikabidi Sheikh Hassan bin Ameir akamatwe na kufukuzwa nchini arejeshwe kwao Zanzibar.

Hili likafanyika.

Waislam wa Tanganyika wakawa hawana kiongozi.

Katika hali hii ndipo ukaitishwa mkutano wa kuasisi BAKWATA.

Serikali ikifanya kazi nyuma ya pazia ilijitahidi sana kuhakikisha kuwa mkutano unafanikiwa.

Serikali ndiyo iliyotoa fedha za kufanyia mkutano ule, ukatoa vyombo vyake vya habari kwa ajili ya kuutangaza vizuri na ukatoa ulinzi kwa wajumbe wote.

Wajumbe waliohudhuria mkutano ule walikuwa kama mia mbili.Mkutano huu ulihudhuriwa na Waislam waliokuwa na vyeo katika serikali na TANU, Waislam waliokuwa wakuu wa wilaya na mikoa na Waislam wenyeviti wa TANU.

Waislam wote wenye majina walialikwa, pamoja na Waislam waliokuwa katika Halmashauri kuu ya TANU na baadhi ya wajumbe wa mkutano walitoka Zanzibar.

Ulikuwa mkutano wa wanasiasa Waislam ambao ukitoa majina yao walikuwa hawana chochote katika harakati za Uislam isipokuwa majina yao.

Hawa laiti Mufti Sheikh Hassan bin Ameir angekuwapo katika mkusanyiko ule hapakuwa na yeyote ambae angeweza kunyanyua uso wake kumtazama.

Agenda ya mkutano huu ilikuwa kujadili katiba ya BAKWATA katiba ambayo ilinakiliwa kutoka katiba ya TANU neno baada ya neno.
 
Back
Top Bottom