Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,116
Wakati Dunia ikiwa inaendelea kupigana vita ili kumuokoa mtoto wa kike kutoka kwenye kitanzi cha ndoa za utotoni BAKATWA wamemekuja na kauli yao ya kupinga kuondolea kwa sheria ya ndoa inayoruhusu mtoto wa miaka 14 kuolewa kwa ridhaa ya wazazi wake.
Ajabu ni kwamba wao wameongza kuwa mtoto wa kuanzia umri wa miaka 11. 12, 13, 14, anaweza kuolea iwapo mzazi ameridhia na mahakama pia kwa kuangalia mazingira ya mtoto kama hasomi na tayari kavunja ungo.
Kila siku Serikali ya Tanzania na na wadau wa elimu wanapigia kelele watoto wa kike wapate elimu, waweze kuondokana na ujinga ili kujikwamua kimaisha na lakini nyie BAKWATA mnataka akaolewe ili azidi kuwa tegemezi na baadae aonekane mzigo kwenye ndoa asiyeweza kuwa na msaada wowote kwa familia yake kiuchumi wala kwake mwenyewe.
Nawauliza BAKWATA kabla ya kuwaza upande 1 tu kuwa akivunja ungo basi anafaa kuwa mke, hamkuwaza kuwa kuvunja ungo ni hatua za ukuaji anazopitia mwanamke katika kuelekea kukomaa? Hamjui kuwa kabla ya ungo huanza kuota matiti nk? Au hata wao waolewe maana tayari wanaonekana wamekua? Tayari kavunja ungo ndio je, akili yake imekomaa kuweza kutambua kuwa ni mtu mzima mwenye jukumu la kulea mme na familia kwa ujumla, au kuweza kulelewa na mme kama mke au nyie mnajua ndoa ni kuingiliana kimwili tu na kupata mimba basi?
Hivi mnajua changamoto za mimba za utototni wakati wa kujifungua? Au hao wanaume mnaowataka kuoa watoto wadogo mtawazuia kuwapa ujauzito hadi wafikishe mri unashauriwa na wataalamu wa afya wa angalau miaka 20 ndio mtu aweze kubeba ujauzito wa kwanza?
Vipi kuhusu kumpa mtoto majukumu ya kuwa mama wa mtoto hali ya kuwa yeye mwenyewe anatamani kucheza na watoto wenzake? Maswali ni mengi sana natamani kuwauliza na najaribu kufikiria kwa nini mmeweza kuongea swala la aibu na hili tena kwa ujasiri na bila kuona aibu?
Natamani mnioneshe watoto wenu wenye umri wa miaka 11, 12, 13, 14 mliowaozesha kwa wanaume na namna wanavyoweza kumudu ndoa zao au mnapigia kelel jambo ambalo kwenye familia zenu hamuwezi kuruhusu litokee. Naona mnataka kuleta janga kwa Taifa kwa vifo vya watoto kwa kujifungua na kupigwa kwenye ndoa zao kwa kuchanganya utoto na majukumu ya mazito kuliko umri wao wa ndoa.
Hivi BAKWATA mnajua kuwa wazazi wenye tamaa mkiwapa ruhusa hiyo watawashawishi watoto wao waache shule ili wawaoze kwa wanaume wazazi wapate hela? Au watoto kushawishiwa na wanaume waache shule shule ili wawaoe huku wakiwaahidi zawadi kedekede na watoto hao kuamini ili wapate hivyo vitu.
Inanipa mashaka kila nikiwaza wakati mnakuja na tamko lenu, mlikuwa na hali gani ya kushindwa kujua kuwa ndoa si kuzaa tu au ndoa si suluhisho la binti aliyeacha shule au anayesumbua kmalezi.
Nachokiona, Watoto wataolewa watazaa na kuchokwa na waume zao na kuachwa kisha waje uraiani warudi kuwa mzigo kwa familia zao walikotoka na kuzalisha wamama wanaolea watoto peke yao bila baba eti kisa nyie mnaoshindwa kuona hasara ya uwepo wa ndoa za utotoni.
Nimfiche wapi binti yangu dhidi ya nyie wanaume wenye tamaa na watoto wadogo? Oneni aibu futeni kauli. Ndoa za watoto ni hatari kwa mtoto wa kike na jamii kwa ujumla.
Pia soma: BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa