Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 227
- 333
Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa kwenye mjadala wa namna ya kudhibiti ndoa za utotoni ambazo bado zinashamiri katika baadhi ya maeneo hususani vijijini.
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya 1971 ya Tanzania inatoa uhuru kwa msichana mwenye umri wa miaka 14 na mvulana mwenye miaka 18 kuolewa na kuoa mtawalia.
Wakati huohuo kwa mujibu wa katiba nchini Tanzania umri sahihi wa utu uzima ni miaka 18 na kuendelea.
Kwa mantiki hii sheria inayoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa inaonekana kuwa ni sheria isiyofaa inayokwamisha maendeleo ya wasichana kwa kuoelewa katika umri mdogo wa miaka 14.
Ingawaje serikali imefanya maboresho kadhaa ya Sheria ya ndoa ya 1971 lakini bado Sheria hiyo haikufanyiwa maboresho kwenye umri wa msichana kuolewa jambo ambalo linakoleza mjadala wa wadau wa sheria, watetezi wa kijinsia na wanaharakati wa haki za binadamu.
Hata hivyo 2019 aliyekuwa waziri wa katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi aliwahi kutamka wazi kuwa sheria ya ndoa ya 1971 ni ya kimapinduzi licha ya kuwa na udhaifu huo mdogo haimaanishi kuwa sheria hiyo sio bora.
Sio hivyo tu baadhi ya wanaharakati wamewahi kupeleka shauri mahakamani kupinga umri wa msichana kuolewa Kuomba mahakama ibatilishe umri huo na mahakama ikaiagiza serikali kufanya hivyo lakini hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika mpala leo.
Vifungu namba 13 na 17 vya Sheria ya ndoa ya 1971 vinakinzana na sheria ya ulinzi wa mtoto ya 2002 na sheria mbalimbali za kitaifa na kimataifa ikiwemo sheria ya msichana kupata elimu.
Ni wakati sasa serikali kutafuta Suluhu ya changamoto ya Sheria hii ikiwemo kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria hii Bungeni ili kubadili kifungu cha umri sahihi wa msichana kuolewa kutoka umri wa miaka 14 hadi 18 ili kuendana na katiba.
Kufanya hivyo kutasaidia kupunguza tatizo la ndoa za utotoni, kumuinua msichana kielimu kwakua itawapa muda Wasichana kusoma badala ya kuozeshwa katika umri mdogo.