Usifuate wala kuyaamini malengo ambayo ulijiwekea utotoni

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,169
15,851
Wakati wa utoto wetu kila mmoja akiulizwa una malengo ya kuwa nani basi atajibu mwalimu,daktari au mtu fulani.

Malengo yale ni upuuzi mtupu na wala hatutakiwi kuyazingatia kwa sababu malengo yale ni utumwa ambao tujilijapndikizia katika akili zetu.

Tuliyachagua malengo yale kwa sababu ndio kazi ambazo tumekuwa tukiziona kila siku watu wakifanya hivyo hatuwezi kuwaza kitu kingine bora zaidi ya hicho.

Ukimchukua mtoto wa kijijini huko ambako tv na umeme ni kwa tabu alafu umuuulize anataka kuwa nani hawezi kukujibu kwamba anataka kuwa body builder kwa sababu hicho kitu hakioni na wala hakijui, lakini huwenda hiyo kazi ya body builder akaifanya kwa ufanisi baadae ila akaidharau kwa sababu sio malengo yake ambayo alijiwekea utotoni.

Hivyo tunapokuwa wakubwa tunatakiwa tuondoe zile malengo za utotoni ambazo tulijiwekea kwa sababu zilikuwa zimejifunga mno kutokana na taarifa ama mambo ambayo tuliyaona kwa wakati huo.

Kwa sasa sisi kama vijana tuangalie wapi tunaweza kutoboa,unaweza kutoboa kwenye ishu ambayo umekuja kuijua ukubwani kabisa ukiwa na miaka 30 wakati huo kazi ya ndoto yako ikikupa ugali na nauli tu.
 
Back
Top Bottom