Shida yenu wafia dini iko hapo. Hakuna haja ya kuwa na munkari kwa jambo jepesi namna hii kaka. Mwalimu Nyerere nia yake ilikuwa njema, lkn inahitaji ubongo makini kuelewa hilo.
Tukubaliane kwamba, all over the World, Uislam hauna HIERARCHY ya uongozi yenye kueleweka nje ya dola ya Kiislam. Namaanisha, hata Waislam wenyewe hawalijui lipi ni jukumu la nani kwenye masuala ya kiuongozi.
Hii dini haikuanzia hapa, imeletwa. Walioileta wana misimamo tofauti ya kiimani, sasa ulitaka nani awe mwakilishi wa Waislam ikiwa Sunnni hawawatambui Ishailia kuwa Waislam? Hebu chukulia mfn wa Kanisa Katoliki. Yajulikana wazi kuwa Askofu Mkuu wa Tanzania anaripoti kwa Pope, kwa hiyo jambo linalohitaji msimamo au kauli ya Kanisa basi linajulikana lipelekwe wapi.
Je, unaweza kunitajia makao makuu ya dini ya Kiislam? Na je, kuna makubaliano yanayoweza kusimama kwa upamoja kati ya Sunni, Shia, Ismailliya na Bohora kiasi kundi fulani liwe radhi kuwakilishwa na lingine ilhali lipo moja linalolishutumu lingine kuwa si Islamic?
Linapotokea jambo la kitaifa, nani katika Uislam anayo hadhi ya ngazi ya Askofu awasemee Waislamu nje ya BAKWATA?
You tell me...ni chombo gani serikali imekianzisha kwa minajili ya kuwacontrol wakristo ndan ya taifa hili.
Hakukuwa na haja ya hili, ROME does. Sasa je kwa Waislamu, Iran? Oman? Saudia? Iraq?
Utatukana mchana kutwa ndugu yangu lkn ukweli ni kwamba, kitu chochote kisicho na uongozi wa juu kabisa kina ugumu kukiendesha.