BAKWATA itakufa CCM ikiondoka madarakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAKWATA itakufa CCM ikiondoka madarakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr.Toyo, Sep 16, 2011.

 1. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo.

  Ifuatayo ni makala hii iloachapishwa tarehe 27 April 2011 katika Gazeti la Mwana Halisi

  BAKWATA itakufa CCM ikiondoka madarakani  BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), limepotea njia. Baraza hilo lililoanzishwa mwaka 1968 kwa nia ya kutetea maslahi ya waislam, limeacha kazi yake ya asili iliyokusudiwa, badala yake sasa linafanya kazi ya kutetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wake.

  Kiongozi mkuu wa BAKWATA, Mufti Simba Shabani Bin Simba, amekuwa akisikika akituhumu viongozi wa vyama vya upinzani kuwa wanataka kuleta vurugu, huku akiacha jukumu lake la msingi la kutetea waislam.

  Wala hakuna shaka kuwa BAKWATA, chombo chenye mamlaka ya kusimamia waislam, kilichowahi kuwa na mahusiano mazuri na wafadhili wa ndani na nje, imekuwa taasisi ya mwisho kimaendeleo kutokana na viongozi wake kuingiza siasa ndani ya chombo hiki.
  Matumaini yaliyobaki ya waislam kwa BAKWATA, ni ya kiimani zaidi kama kupata taarifa za kuandama mwezi mtukufu wa Ramadhan na kusherehekea sikukuu za kiislam. Basi!

  Wakati baadhi ya taasisi za kidini zinashindana na serikali katika uanzishwaji wa vyuo vikuu, hospitali za rufaa kama Bugando na KCMC, BAKWATA imeishia kumiliki zahanati, vituo vya afya na shule za sekondari zinazoongoza kwa matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha nne na sita.

  BAKWATA haina hata chuo kikuu kimoja inachokimiliki, wala ardhi iliyotengwa kwa ajili hiyo. Pengine inasubiri kupewa jengo na serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

  Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro hakimilikiwi na BAKWATA, wala majengo yake yaliyotolewa na serikali wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa.

  Wakati Mtume Muhammad (SAW) alipanga mikakati madhubuti kusaidia waislam kwa kuanzisha benki ya waislam (Baitl-Mal) na kuwachagua viongozi makini na wenye uchungu wa maendeleo kuwa wasiadizi wake, uaminifu wake katika kutunza mali za waislam na wasiokuwa waislam uliwavutia hata waliokuwa wakimpinga.

  Inaelezwa kwamba msimamo huo wa mtume, ndiyo chanzo cha ndoa yake na Bi. Khadija ambaye historia inaonyesha kabla ya kumuoa alikuwa mfanyakazi wake katika masuala ya biashara. Mtume alitunza kwa uaminifu mkubwa na hatimaye Bi. Khadija alivutiwa na kufunga naye ndoa na mtume.

  Baada ya kufariki masahaba walichukua jukumu la kuwatumikia waislam, waliogopa kula mali ya waislam. Waliwasikiliza na kuyatatua matatizo yao, walitoa chao kuwapa wenye shida siyo kuchukua cha wenye shida kutia matumboni.

  Yote haya walifanya kwa kuamini uongozi ni dhamana, na kubwa zaidi wakiamini ipo siku watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu na kujibu jinsi walivyotumikia waliowaongoza.

  Ni tofauti na viongozi wa sasa wa BAKWATA ambao husoma tu historia za masahaba na makhalifa waliowahi kutumia jamii ya kiislam kama vile umar bin Abdul Azeez (R.A).

  Swali linakuja, kama hivi ndivyo, mbona tuhuma dhidi ya kutafuna hata mali za yatima na wale wasiojiweza zinazidi kuongezeka katika chombo hiki?

  Baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani, Desemba 2005 alikuwa mgeni rasmi katika baraza la Iddi mjini Arusha. Katika hotuba yake, aliilaumu BAKWATA kwa kushindwa kuwatumikia waislam kwa dhati.

  Alisema waislam wameichoka BAKWATA na kwamba chombo hicho kimekuwa kama kikundi cha watu wachache chenye manufaa binafsi.
  Waliokuwapo na waliosikiliza kupitia vyombo vya habari waliona jinsi waislam walivyozizima kwa furaha kutokana na kauli ya rais. Waliokuwapo ukumbuni walipiga takbir kwa kishindo kuashiria wameguswa na kauli ya rais.

  Hili lilitokea mbele ya wafuasi wa BAKWATA na viongozi wake. Ulikuwa ujumbe kwa Mufti Simba na waislam kwa ujumla, hasa wale wanaotaka mabadiliko katika utendaji wa chombo chao.

  Vyombo vya habari viliripoti kauli ya rais, na kwamba wengi waliamini kuwa kauli ya mkuu wa nchi ingesaidia kuwatoa BAKWATA katika usingizi wa pono. Wapi!

  Nyingi ya shule zinazomilikiwa na BAKWATA zinatoa matokeo mabovu katika mitihani ya kidato cha nne na sita; huku zahanati zake nyingi zikilaumiwa kwa kutoa huduma duni.

  Wengi walitarajia kuwa chombo hiki kingetumia raslimali zake kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabenki, hospitali, vyuo vya elimu ya juu na kuanzisha mifuko ya pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi zake. Wangetumia misaada inayotolewa kwa faida ya waislam na jamii kwa ujumla.

  Hoja kwamba waislam hawapendi kusoma haiwezi kuingia akilini mwa wengi. Mamia kwa makumi ya waislam wanasoma katika vyuo vikuu mbalimbali dunuani kama vile Khartoum, Tehran, Misri, Algeria, Senegal. Wengi wao wamejikita katika masomo ya uhandisi, udaktari, kilimo, teknolojia, uhusiano wa kimataifa na hata sheria za kimataifa.

  Je, nani asiyetambua jinsi Zanzibar ilivyotikisa nyanja ya habari duniani? Kwa mfano, Zeyana Seif, mwanamke wa kwanza Afrika ametangaza idhaa ya Kiswahili ya Uingereza (BBC).

  BAKWATA wanafahamu kuwa waislam walikuwa wa kwanza kuandaa mpango wa kujenga chuo kikuu cha kimataifa huku viongozi wa jumuiya za kiislam wakitafuta misaada ndani na nje.

  Baadhi ya waislam licha ya umasikini waliokuwa nao walijitolea kuchangia kabla jumuiya hiyo kukumbwa na mgogoro na hatimaye kuvurugika na majukumu ya jumuiya hiyo kukabidhiwa BAKWATA. Maafa ya waislam kimaendeleo yalianza hapo.

  Katiba ya BAKWATA imelalamikiwa mahakamani na baadhi ya waislam kuwa ina mapungufu. Lakini hadi leo BAKWATA haijatatua tatizo hilo kwa faida ya jamii ya kiislam.

  Aidha, BAKWATA badala ya kujiingiza katika siasa, ingejikita katika kusimamia mali za waislam zilizouzwa na zinazouzwa na baadhi ya viongozi wake kinyume cha taratibu.

  Tarehe 17 Aprili 1991, rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi aliwataka waislam kukaa pamoja na kutafuta suluhu juu ya mgogoro wa chombo chao, lakini BAKWATA imegoma kutii agizo la kiongozi huyo kwa kudhani kuwa inalindwa na CCM. Wapo wanaosema, siku CCM ikiondoka madarakani, BAKWATA nayo itakufa kifo cha mende.

  Wanaosema CCM ikishindwa uchaguzi BAKWATA itakufa wanasema pia kuwa kifo cha BAKWATA utakuwa mwanzo mpya wa kimaendeleo kwa jamii ya kiislam na waislam kwa ujumla.

  Waislam wanalalamika kunyimwa fursa za maendeleo na watawala wanaolalamikia hali hiyo, siyo Mufti wala viongozi wakuu wa BAKWATA.

  Kuna taarifa mara baada ya wakiristo kufunga mkataba na serikali (MoU) baadhi ya taasisi za kiislam zilikaa na kutunga rasimu ya mkataba kama huo na kuupeleka serikalini kwa manufaa ya waislam, lakini walipata vizingiti huku serikali ikitaka BAKWATA iandae.
  BAKWATA imekaa kimya. Haitaki kutenda yale ambayo waislam wanataka. Wanadhani kwao hilo si tatizo, bali tatizo ni CHADEMA.

  Je, katiba ya BAKWATA si inasema kila kiongozi wa BAKWATA lazima awe muislam mwaminifu mwenye kufuata quran na sunna, wapi wanapoteleza viongozi hawa kuwatumikia waislam?  1-Je ina ukweli wowote?
  2-Na kama ina mantiki JE nini nini kifanyike?
  3- je Kuna umuhimu wa ku-resolve BAKWATA?

  NAOMBENI MAONI YENU NDUGU ZANGU KATIKA IMANI..
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ilishakufa hata kabla ccm kufa..imebakiza kuitwa kwenye sherehe za ikulu..Taasisi zingine za kiislamu mwendo mdundo..tutafika tu Inshallah
   
 3. M

  MAKAKI Senior Member

  #3
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  napita udini, udini huu!
   
 4. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa ukipita ndio mpaka useme si upite kimya kimya tu!
   
 5. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama haikuhusu waachie inaowahusu (wenye uchungu na dini yao)
   
 6. doup

  doup JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Hivi Mufti anapatikanaje? au ni style ya moshi mweupe, akishawekwa pale hatolewi mpaka mwenyezi amuite? kama ni tofauti waislam fanyezi mapinduzi ya uongozi ili viongozi wenye upeo na dira washike hatamu. Sio waganga njaa.

  Watu wanabishana hata kuandama kwa mwezi, ili nao tu waonekane kuwa wananguvu na mamlaka.
   
 7. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  ...alfu ukirudi usipite tena hapa,njia imefungwa...watu tuko ndani tunaongea we wapita karibu na dirisha wapiga kelele...
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  hiyo ni kweli tupu!hii thread ilishajadiliwa kipindi cha nyuma
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  unamtangazia naaaani....................au untaka tu kuongeza idadi ya post?
   
 10. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo nakuunga mkono,
  Halafu kinachoniuma zaidi ni kukataa kwao kuunganisha waislamu.

  Tarehe 17 Aprili 1991, rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi aliwataka waislam kukaa pamoja na kutafuta suluhu juu ya mgogoro wa chombo chao, lakini BAKWATA imegoma kutii agizo la kiongozi huyo.

  Inasikitisha sana kuwa mbali na kuwa na vitega uchumi mbalimbali taasisi hii haina hata TV (luninga) moja na kama wana redio basi haizidi moja.

  I think its time to dissolve it or unless viongozi wa BAKWATA wajivue GAMBA, ikishindikana basi waangalie mikakati yao upya.
   
 11. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa muda mrefu nilikuwa nikisikia kuwa Bakwata haipo kwa maslahi ya waislam,nikawa siamini kwa kuzani huenda kulikuwa na chuki miongoni mwa madhehebu ya kiislam. Tamko la bakwata Tabora limenifanya niamini kuwa wapo kisiaza zaidi kuliko kidini. Kwamba wanawataka waislamu wote igunga wasimpigie kura mgombea wa chadema inaonyesha kuwa wanapiga kampeni.

  Hivi ni nani asiyejua kwamba suala la mkuu wa wilaya igunga lipo mahakamani? Bakwata inadhani waislam wote akili zao zinafanana na wao, hapana tumewastukia.Eti kabla ya kutolewa kwa tamko hilo walifanya kikao cha pamoja ccm kwenye hotel kwa mujibu wa Radio five Arusha 2:30 usiku, hii ni aibu. Waislam tunapenda kuona chombo kinachotoa matamko baada kufanya utafiti sio kisiasa.

  Mfano mzuri ni namna kikwete alivyoijibu bakwata wakati wa baraza la Idd,ile ni aibu,hivi zile shule za bakwata zilizopo zinafanana na seminari za kikristo kwa ufaulu na uendeshaji wake.Haya ndio mambo ya kujadiliwa na bakwata na si kupigia kampeni CCM.
   
 12. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Bora wewe ulie ona kuwa wanatumiwa na wamekuwa mambumbu hawawezi hata kudigest issue yoyote wao ni kuropoka tu.
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Dini yenyewe ilianzishwa kisiasa kama chama cha walalamikaji unategemea wataishi aje? c ni kupewa ubwabwa tu kisha wanakurupuka kuropoka?
   
 14. m

  mtznunda Senior Member

  #14
  Sep 23, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa ww unafka mbali unatutukana hata tucio kuwepo nataman nikukate kichwa chaki
   
 15. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2011
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo Raisi wa bakwata kachaguliwa na ccm unategemea nini hapo
   
 16. M

  MPG JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waoneeni huruma tu hao mambumbu wa darasa la pili hawana mbele wala nyuma wamekalia kucheza bao na kunywa kahawa na kuoa wake wengi wakati hawana uwezo.
   
 17. S

  Straight JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hey ma' fellow Muslims... Cnt we wake up... We ar bein used without any reason... Ngoja niwape siri, wafanya maamuz pale ccm ni christian, wana22mia kwa mgongo wa Rais.. Cnt we thnk why thr waz no any benefit we obtain relatn 2 our support 2 ccm... SABABU 2NA2MIKA KWA WAKRISTO KWA MGONGO WA RAIS MUSLIM, u al knw 2na rais sanamu he cant mek any decisn, na maamuz meng ya ccm yanakuwa influence na xstian waliopo ndan ya ccm, sasa 2baki na ujuha we2... 2tatumiwa na ku2pwa kama Condoms..
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ....na bado!

  gadem zenu
   
 19. S

  Straight JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ha2oni hata wagombea waliopo na wenye nguvu, they r al xstian.... Let us wake up Muslims, ooh God..! Its so painful...
   
 20. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  hapo mbona unatukana wote. Tatizo la viongozi si la waislamu wote.
   
Loading...