BAKWATA itakufa CCM ikiondoka madarakani

BAKWATA itakufa CCM ikiondoka madarakani

Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo.

Ifuatayo ni makala hii iloachapishwa tarehe 27 April 2011 katika Gazeti la Mwana Halisi

BAKWATA itakufa CCM ikiondoka madarakani



BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), limepotea njia. Baraza hilo lililoanzishwa mwaka 1968 kwa nia ya kutetea maslahi ya waislam, limeacha kazi yake ya asili iliyokusudiwa, badala yake sasa linafanya kazi ya kutetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wake.

Kiongozi mkuu wa BAKWATA, Mufti Simba Shabani Bin Simba, amekuwa akisikika akituhumu viongozi wa vyama vya upinzani kuwa wanataka kuleta vurugu, huku akiacha jukumu lake la msingi la kutetea waislam.

Wala hakuna shaka kuwa BAKWATA, chombo chenye mamlaka ya kusimamia waislam, kilichowahi kuwa na mahusiano mazuri na wafadhili wa ndani na nje, imekuwa taasisi ya mwisho kimaendeleo kutokana na viongozi wake kuingiza siasa ndani ya chombo hiki.
Matumaini yaliyobaki ya waislam kwa BAKWATA, ni ya kiimani zaidi kama kupata taarifa za kuandama mwezi mtukufu wa Ramadhan na kusherehekea sikukuu za kiislam. Basi!

Wakati baadhi ya taasisi za kidini zinashindana na serikali katika uanzishwaji wa vyuo vikuu, hospitali za rufaa kama Bugando na KCMC, BAKWATA imeishia kumiliki zahanati, vituo vya afya na shule za sekondari zinazoongoza kwa matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha nne na sita.

BAKWATA haina hata chuo kikuu kimoja inachokimiliki, wala ardhi iliyotengwa kwa ajili hiyo. Pengine inasubiri kupewa jengo na serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro hakimilikiwi na BAKWATA, wala majengo yake yaliyotolewa na serikali wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa.

Wakati Mtume Muhammad (SAW) alipanga mikakati madhubuti kusaidia waislam kwa kuanzisha benki ya waislam (Baitl-Mal) na kuwachagua viongozi makini na wenye uchungu wa maendeleo kuwa wasiadizi wake, uaminifu wake katika kutunza mali za waislam na wasiokuwa waislam uliwavutia hata waliokuwa wakimpinga.

Inaelezwa kwamba msimamo huo wa mtume, ndiyo chanzo cha ndoa yake na Bi. Khadija ambaye historia inaonyesha kabla ya kumuoa alikuwa mfanyakazi wake katika masuala ya biashara. Mtume alitunza kwa uaminifu mkubwa na hatimaye Bi. Khadija alivutiwa na kufunga naye ndoa na mtume.

Baada ya kufariki masahaba walichukua jukumu la kuwatumikia waislam, waliogopa kula mali ya waislam. Waliwasikiliza na kuyatatua matatizo yao, walitoa chao kuwapa wenye shida siyo kuchukua cha wenye shida kutia matumboni.

Yote haya walifanya kwa kuamini uongozi ni dhamana, na kubwa zaidi wakiamini ipo siku watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu na kujibu jinsi walivyotumikia waliowaongoza.

Ni tofauti na viongozi wa sasa wa BAKWATA ambao husoma tu historia za masahaba na makhalifa waliowahi kutumia jamii ya kiislam kama vile umar bin Abdul Azeez (R.A).

Swali linakuja, kama hivi ndivyo, mbona tuhuma dhidi ya kutafuna hata mali za yatima na wale wasiojiweza zinazidi kuongezeka katika chombo hiki?

Baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani, Desemba 2005 alikuwa mgeni rasmi katika baraza la Iddi mjini Arusha. Katika hotuba yake, aliilaumu BAKWATA kwa kushindwa kuwatumikia waislam kwa dhati.

Alisema waislam wameichoka BAKWATA na kwamba chombo hicho kimekuwa kama kikundi cha watu wachache chenye manufaa binafsi.
Waliokuwapo na waliosikiliza kupitia vyombo vya habari waliona jinsi waislam walivyozizima kwa furaha kutokana na kauli ya rais. Waliokuwapo ukumbuni walipiga takbir kwa kishindo kuashiria wameguswa na kauli ya rais.

Hili lilitokea mbele ya wafuasi wa BAKWATA na viongozi wake. Ulikuwa ujumbe kwa Mufti Simba na waislam kwa ujumla, hasa wale wanaotaka mabadiliko katika utendaji wa chombo chao.

Vyombo vya habari viliripoti kauli ya rais, na kwamba wengi waliamini kuwa kauli ya mkuu wa nchi ingesaidia kuwatoa BAKWATA katika usingizi wa pono. Wapi!

Nyingi ya shule zinazomilikiwa na BAKWATA zinatoa matokeo mabovu katika mitihani ya kidato cha nne na sita; huku zahanati zake nyingi zikilaumiwa kwa kutoa huduma duni.

Wengi walitarajia kuwa chombo hiki kingetumia raslimali zake kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabenki, hospitali, vyuo vya elimu ya juu na kuanzisha mifuko ya pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi zake. Wangetumia misaada inayotolewa kwa faida ya waislam na jamii kwa ujumla.

Hoja kwamba waislam hawapendi kusoma haiwezi kuingia akilini mwa wengi. Mamia kwa makumi ya waislam wanasoma katika vyuo vikuu mbalimbali dunuani kama vile Khartoum, Tehran, Misri, Algeria, Senegal. Wengi wao wamejikita katika masomo ya uhandisi, udaktari, kilimo, teknolojia, uhusiano wa kimataifa na hata sheria za kimataifa.

Je, nani asiyetambua jinsi Zanzibar ilivyotikisa nyanja ya habari duniani? Kwa mfano, Zeyana Seif, mwanamke wa kwanza Afrika ametangaza idhaa ya Kiswahili ya Uingereza (BBC).

BAKWATA wanafahamu kuwa waislam walikuwa wa kwanza kuandaa mpango wa kujenga chuo kikuu cha kimataifa huku viongozi wa jumuiya za kiislam wakitafuta misaada ndani na nje.

Baadhi ya waislam licha ya umasikini waliokuwa nao walijitolea kuchangia kabla jumuiya hiyo kukumbwa na mgogoro na hatimaye kuvurugika na majukumu ya jumuiya hiyo kukabidhiwa BAKWATA. Maafa ya waislam kimaendeleo yalianza hapo.

Katiba ya BAKWATA imelalamikiwa mahakamani na baadhi ya waislam kuwa ina mapungufu. Lakini hadi leo BAKWATA haijatatua tatizo hilo kwa faida ya jamii ya kiislam.

Aidha, BAKWATA badala ya kujiingiza katika siasa, ingejikita katika kusimamia mali za waislam zilizouzwa na zinazouzwa na baadhi ya viongozi wake kinyume cha taratibu.

Tarehe 17 Aprili 1991, rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi aliwataka waislam kukaa pamoja na kutafuta suluhu juu ya mgogoro wa chombo chao, lakini BAKWATA imegoma kutii agizo la kiongozi huyo kwa kudhani kuwa inalindwa na CCM. Wapo wanaosema, siku CCM ikiondoka madarakani, BAKWATA nayo itakufa kifo cha mende.

Wanaosema CCM ikishindwa uchaguzi BAKWATA itakufa wanasema pia kuwa kifo cha BAKWATA utakuwa mwanzo mpya wa kimaendeleo kwa jamii ya kiislam na waislam kwa ujumla.

Waislam wanalalamika kunyimwa fursa za maendeleo na watawala wanaolalamikia hali hiyo, siyo Mufti wala viongozi wakuu wa BAKWATA.

Kuna taarifa mara baada ya wakiristo kufunga mkataba na serikali (MoU) baadhi ya taasisi za kiislam zilikaa na kutunga rasimu ya mkataba kama huo na kuupeleka serikalini kwa manufaa ya waislam, lakini walipata vizingiti huku serikali ikitaka BAKWATA iandae.
BAKWATA imekaa kimya. Haitaki kutenda yale ambayo waislam wanataka. Wanadhani kwao hilo si tatizo, bali tatizo ni CHADEMA.

Je, katiba ya BAKWATA si inasema kila kiongozi wa BAKWATA lazima awe muislam mwaminifu mwenye kufuata quran na sunna, wapi wanapoteleza viongozi hawa kuwatumikia waislam?



1-Je ina ukweli wowote?
2-Na kama ina mantiki JE nini nini kifanyike?
3- je Kuna umuhimu wa ku-resolve BAKWATA?

NAOMBENI MAONI YENU NDUGU ZANGU KATIKA IMANI..

Hata mimi binafs nitafurahi sana sana
 
Bakwata hawana zuri hata moja?

Baraza hilo zuri walilonalo ni la kutangaza mwezi na kuadhimisha maulidi ya mtume SAW. Zaidi ya hapo hakuna kengine walichokifanya cha maana kwa waislam. Hospitali na zahanati wanazozimiliki ni mali za EAMWS na kwa bahati mbaya nyingi waliziuza pamoja na viwanja vya mayatima na waislamu.
 
hivi nyinyi mnaelewa maana ya neno MFUMO?

Kwani BAKWATA Nyerere aliiweka kwenye katiba ya nchi mpaka iwe vigumu kuibadilisha. Mwinyi amekaa miaka 10 Ikulu amebadilisha karibu mambo yote ya msingi aliyoanzisha Mwalimu, nani alimzuia kubadilisha bakwata?

Alhaji Kikwete anatawala wakati Mwalimu alikufa zamani, makamu wake na mkuu idara ya usalama ni imani moja, nani anayemtisha asiibadili Bakwata?


Wakati mwingine huwa naona waislam wenyewe ndo wanafiki wa kiwango kisichoelezeka.

Ni upumbavu kuendelea kumlalamikia Nyerere na serikali yake kuunda BAKWATA ilhali tuna awamu mbili sasa zikiwa chini ya waislamu.

Mmeshindwaje kuivunja sasa wakati haina masilahi kwenu au Kikwete na Mwinyi hawalijui hili?

Hivi sasa mnadai mahakama ya kadhi ianzishwe na serikali ilhali mnaitukana serikali ya Nyerere kuanzisha BAKWATA eti kwa nini ilijihusisha na mambo yasiyoihusu huu ni ujuha.

Ukipata mtu ama mfumo wa kuulalamikia kila changamoto zinapokukabili na wala hujishughulishi kuzitatua then utabaki hivyo maisha yako yote.

Tuseme Nyerere ni mdini ndo maana alianzisha BAKWATA ili kuwakandamiza waislamu FINE!!

Sasa mmeshindwaje kuivunja? Achilia mbali kung'atuka Nyerere kesha kufa kabisa lakini kelele bado hizo hizo tu eti Nyerere kaanzisha.

WHO IS NYERERE??? Mbona mambo kibao tu aliyoyaanzisha hatunayo tena why not BAKWATA?

Mbaya zaidi,hata Ph.D holders na Professors(Muslims) wa nchi hii bado wanamlalamikia Nyerere!!!​
 
Kulaani Mtu Aliyekufa,tena Aliyejitahidi Kuwahimiza Kupenda Shule Kuliko Madrasa Ni Zaidi Ya Upagani
 
Hivi unajua maana ya mfumo? Naona unaandika pumba tu.


mkuu,
una ushahidi wa mwinyi kupewa maagizo makali au story za kwenye viringe vya kahawa tu?

Hayo maagizo alipewa na nani(usiniambie nyerere)

kwa nini sasa hamumtukani mwinyi kwa kushindwa kupigania uislam na waislamu(kwa kumsikiliza kaffir) ili hali alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo badala yake lawama na matusi ni nyerere.(huu si ndo unafiki)

mbona mkapa alimpuuza nyerere juu ya uuzwaji wa nbc?alimfanyaje?

Haya tuseme mwinyi naye ni kaffir,ameingia kikwete lakini hakuna chochote kilichofanyika juu ya bakwata mpaka sasa lakini bado mnaona poa tu maana ameianzisha nyerere.kweli?

Kwa hiyo nyie kama waislamu mmefanyaje juu ya uchaguzi sijui elimu ya sheikh mkuu,mishahara etc au hapo napo nyerere anahusika?

Tatizo watu mmeaminishwa kwamba matatizo yenu yote wakumlaumu nyerere na wala hamhangaiki kuyatatua.

Kwa hiyo mnamsubiria nyerere afufuke aje aivunje bakwata?

Kazi kwelikweli
 
hivi nyinyi mnaelewa maana ya neno MFUMO?


Watu tunatofautiana uelewa wa mambo hivyo kama unaona hatuko sawa katika maelezo yetu ni ruksa kusahihisha.

Siyo kuulizana maswali ya sekondari.
 
Siichukiii BAKWATA,ila naichukia sana viongozi wa bakwata
 
muislam anaejitambua hawezi kuitambua bakwata kama chombo kinachomuwakilisha.bakwata imeundwa na nyerere ili kuwaumiza waislam.na ndo maana viongozi wa bakwata huwa hawajitambui haiwezekani taasisi kubwa kama ile iongozwe na mtu ambae hajui asubuhi wala jioni.mimi ni muislam lakini kitu ambacho ninakichukia katika nchi hii ni bakwata.naandika maneno haya kwa uchungu sana r.i.p shekh ilunga inapotajwa bakwata huwa nakukumbuka sana.

Kwa hiyo mnamsubiri Nyerere aje atatue tatizo lenu na bakwata kwa vile ndiye aliyeianzisha? Nyie waislamu mumefanya nini ili kutatua tatizo hilo au mmekubali yaishe? Na kwa nini mlalamike bila kuchukua hatua?
 
Hivi unajua maana ya mfumo? Naona unaandika pumba tu.

Mbona sioni mahali uliopoweka huo mchele wako sasa?

Kama huna hoja acha ku-quote wanaume ovyo,nenda JF Photo huko ndo kunakufaa hii mada imekuzidi kimo
Kwa nini uhangaike na pumba?

Na kama unaona ni pumba chukua ukalishie nguruwe maana umenikomalia kweli ilhali hakuna chochote cha maana ulicho-comment kwenye mada.

Au unataka ligi tu?

Nimekuambia unikosoe nilipopotosha umekazana kupakazia tu.

Hivi una akili kweli wewe?

Acha nikupuuze.
 
nilifikiri ungejifunza kitu hapo. kama anaweza kumsifia hadharani ili awafurahishe nyinyi lakini akiwa vichorochoroni anaongea kinyume unaweza kuona kabisa dhamira ya mhusika iko wapi.
between nawatakia kila la heri kuomba baraka kupitia kwa binadamu kama wewe aliekuwa anaenda chooni kama wewe na madhaifu mengine kibao badala ya kuomba baraka kwa yule aliyemuumba huyo unayemuomba na wewe. sishangai mnaenda kutubu hata dhambi kwa watu hao hao ambao hata wao wanafikia hatua ya kulawiti mpaka watoto achilia mbali kuwa na mahusiano na watu wazima wenzao.
nikiyafikiria haya yote na mengine mengi kama ushoga nk; najiona mwenye bahati ya pekee kuzaliwa Muislam. ASANTE MUNGU KWA NEEMA HII YA AINA YAKE ULIYONIJAALIA.

Kitu pekee ninachoweza kukusaidia ni kwamba Mungu wa Nyerere ni tofauti na Mungu unayemwabudu wewe.Mungu wa Nyerere(YEHOVA) anafundisha watu kusamehe,Heshima,Adabu na kuwaombea wenye matendo mabaya.Naamini Mungu wa Nyerere ana nguvu kuliko Mungu unayemwamini wewe, ndio maana wengi wanaompinga Nyerere vichochoroni hawana ubavu wa kumsema hadharani.Mifano ipo mingi sana ukiwemo wa juzi ambapo Shekh Jongo alilia sana Bungeni kwa ajili ya waliokuwa wakimtusi Nyerere ijapokuwa akiwa Msikitini huongea kinyume. Mfano mwingine ni kuanzisha BAKWATA ambayo waislamu kwa Umoja wao wameshindwa kuiondoa pamoja na kwamba ameshatangulia mbele ya haki kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita.Hii ni dalili kwamba hiki alichokianzisha ni kitu chema.Si ajabu hivi karibuni akatangazwa Mtakatifu ili watu waanze kupata BARAKA NA NEEMA kupitia jina lake.
 
kwani ile ya Tundu Lisu kumsema nyerere kuwa alizoea vya kunyonga vya kuchinja hataviweza au alizoea kuishi kwa uongo ukweli hakuuweza unalionaje?
Lisu ni mkirsto mwenzenu lakini ameyaona mapungufu ya mkirsto mwenzake. naye mnampinga kama mlivyobize kutukejeli kwenye mitandao?

Ndugu yangu mabo ya dini ni Makubwa sana na Mgumu.Mungu wa Nyerere ni YEHOVA.Kwa tafsiri nyingine anaitwa yeye NIKO AMBAYE NIKO.Yeye hafi.Aliyekufa ni Nabii Isa,huyu ni Miongoni mwa manabii 25 wanaoheshimiwa na Waislamu.Ila hata huyu nabii Isa alifufuka na kupaa Mbinguni kwa hiyo bado yungali hai mpaka leo. Wengi wanamkubali Nyerere na ndio maana imetengwa siku maalum ya kupumzika kwa ajili yake.Wakristo wana msemo kwamba"Sauti ya wengi ni Sauti ya Mungu"Wengi wanamsifu Nyerere hivyo hata Mungu yu Pamoja nae. BAKWATA ilianzishwa kwa lengo Jema tatizo imejigeuza tawi la CCM hivyo panahitajika waislamu wanaojitambua ili wairekebishe lakini sio hawa wanaonunuliwa kumtukana Baba wa Taifa.
 
nguruwe pita tu leo sina mkuki.

Mbona sioni mahali uliopoweka huo mchele wako sasa?

Kama huna hoja acha ku-quote wanaume ovyo,nenda JF Photo huko ndo kunakufaa hii mada imekuzidi kimo
Kwa nini uhangaike na pumba?

Na kama unaona ni pumba chukua ukalishie nguruwe maana umenikomalia kweli ilhali hakuna chochote cha maana ulicho-comment kwenye mada.

Au unataka ligi tu?

Nimekuambia unikosoe nilipopotosha umekazana kupakazia tu.

Hivi una akili kweli wewe?

Acha nikupuuze.
 
nilifikiri ungejifunza kitu hapo. kama anaweza kumsifia hadharani ili awafurahishe nyinyi lakini akiwa vichorochoroni anaongea kinyume unaweza kuona kabisa dhamira ya mhusika iko wapi.
between nawatakia kila la heri kuomba baraka kupitia kwa binadamu kama wewe aliekuwa anaenda chooni kama wewe na madhaifu mengine kibao badala ya kuomba baraka kwa yule aliyemuumba huyo unayemuomba na wewe. sishangai mnaenda kutubu hata dhambi kwa watu hao hao ambao hata wao wanafikia hatua ya kulawiti mpaka watoto achilia mbali kuwa na mahusiano na watu wazima wenzao.
nikiyafikiria haya yote na mengine mengi kama ushoga nk; najiona mwenye bahati ya pekee kuzaliwa Muislam. ASANTE MUNGU KWA NEEMA HII YA AINA YAKE ULIYONIJAALIA.

Masuala ya Dini ni Mazito sana.Wenye dini wenyewe ndio wanayaelewa.Kuna Dini inamheshimu M-bakaji mmoja ambaye alinajisi katoto ka Miaka Tisa huko Uarabuni,Vilevile kuna madhehebu yanaabudu NG'ombe.Kwa ujumla suala la Imani ni Zito na huwezi kulielewa kama upo upande wa Pili.Kinachotakiwa ni kufuata matakwa ya Dini yako na kuwaacha wenzako waendelee na ya kwao.
 
kwani ile ya Tundu Lisu kumsema nyerere kuwa alizoea vya kunyonga vya kuchinja hataviweza au alizoea kuishi kwa uongo ukweli hakuuweza unalionaje?
Lisu ni mkirsto mwenzenu lakini ameyaona mapungufu ya mkirsto mwenzake. naye mnampinga kama mlivyobize kutukejeli kwenye mitandao?

Anachokisema Lissu sio lazima kiwe kweli.Bunge la katiba lilijaa Waislamu lakini wengi walipinga Mahakama ya Kadhi.Sidhani kama huo ndio msimamo wa Waislamu eti kwa sababu waislamu waliokuwa Bungeni waliipinga Mahakama hiyo.
 
Tunarudi kule kule.

You have to employ your thinking skills.

I can see unadiscuss outcomes na kuacha chanzo kikuu cha uwepo wa hiyo bakwata.

Tumeeleza mara nyingi humu ndan kadhia ya hiki chombo mamluki cha bakwata jins nyerere laanatullah alivyokianzisha kwa kuvunja EAMWS kwa hila na kwa islamohobia zake.

Jins alivyoianzisha bakwata na kuifanyia political affialition na chama pamoja na siasa za nchi hii.

Ikiwa ni pamoja na kuifund bakwata na kusimamia malipo ya viongoz wake na kuratibu viongoz gan waongize bakwata.

Walipokuja viongoz wengine na political ambitions zao usidhan km bakwata wakiona ina wafaa wanaweza kuiweka kando.

Struggle for political power is by all means.

Hao ni wanasiasa ambao wamechaguliwa kuja kutekeleza ilan za vyama vyao.


Na sio kuja kupigania haki za uislam na waislam.

Ni demokrasi ndiyo imewaweka hapo.

The Root Problem ya bakwata ni kafir nyerere.

Hapa hatulalamiki bali tunakuelezea uhalisia.

Its very unfortunate unadhan kuwa tunalalamika.


Nimekupata Mkuu.

Chanzo cha tatizo ni kafir Nyerere na ameshakufa tayari,Muslim successors wake wameikuta BAKWATA iko kwenye system na inawasaidia kwenye siasa zao hivyo wameamua kuilea ili iendelea kuwakandamiza waislamu.

Mnaona poa tu maana hii ni outcome tu lakini source ni kafir Kambarage.

Then nini hatima yake sasa?

Kwa maana nyingine;

1 BAKWATA itaendelea kuwepo ikikandamiza waislamu mpaka atakapopatikana mteule wa kuutetea uislamu na waislam wa nchi hii.

2 Mwinyi na Kikwete wasilaumiwe kulea chombo kikandamichacho waislamu maana mateso ya waislam wenzao hayawahusu na hawakuchaguliwa kutetea uislamu hivyo waislam waendelee tu kumlaan marehemu kafir.

Hii issue imejaa unafiki mwingi Sana miongoni mwa waislam wenyewe.

Anyway endeleeni kuvumulia tu pengine mwisho wa BAKWATA utakuja automatically.

Kwa sasa endeleeni tu kumlaani Nyerere.
 
MAPINDUZi ni muhimu ila tuu dola isiingilie uamuzi wa waislam
 

Nimekupata Mkuu.

Chanzo cha tatizo ni kafir Nyerere na ameshakufa tayari,Muslim successors wake wameikuta BAKWATA iko kwenye system na inawasaidia kwenye siasa zao hivyo wameamua kuilea ili iendelea kuwakandamiza waislamu.

Mnaona poa tu maana hii ni outcome tu lakini source ni kafir Kambarage.

Then nini hatima yake sasa?

Kwa maana nyingine;

1 BAKWATA itaendelea kuwepo ikikandamiza waislamu mpaka atakapopatikana mteule wa kuutetea uislamu na waislam wa nchi hii.

2 Mwinyi na Kikwete wasilaumiwe kulea chombo kikandamichacho waislamu maana mateso ya waislam wenzao hayawahusu na hawakuchaguliwa kutetea uislamu hivyo waislam waendelee tu kumlaan marehemu kafir.

Hii issue imejaa unafiki mwingi Sana miongoni mwa waislam wenyewe.

Anyway endeleeni kuvumulia tu pengine mwisho wa BAKWATA utakuja automatically.

Kwa sasa endeleeni tu kumlaani Nyerere.


Thank you.

I can see umenisoma vyema shukran kwa hilo.

Hili la bakwata sisi waislam hatukuanza leo kulipigia kelele.

Infact tumeanza kulipigia kelele tokea uhai wake kafir nyerere laanatullah.

Alichokifanya nyerere ni kuwaweka vizuizin wapiganaji na wazungumzaji wa hoja hizo.

Japo mambo haya yalikuwa yanafanywa kwa siri lln hiv sasa usiri huo haupo tena.

Unaona sasa kuna viwanja kama hivi ambavyo watu wanakuwa free kuongea fact bila khiyana yoyote.

Waislam walipogundua hila hizo wakaona isiwe tabu.

Kwa kuwa upo utaratibu wa kuanzisha vyombo vingine kisha vikasajiliwa na kutambulika haina shida.

Bado hatujachelewa vyombo vingine vingi tumeanzisha na tutaanzisha kuratibu mambo yetu kwa niaba ya vizaz vyetu vya leo na kesho.

Kipindi cha EAMWS KULIKUWA HADI NA PROGRAM ZA KUANZISHA VYUO VIKUU NA HOSPITALS N.K.

KUMBUKA HIYO ILIKUWA NI MIAKA YA 60's.

Lakn baada ya hila ya kuivunja jumuiya ile na nyerere kuanzisha bakwta.huwez amin bakwta imeshindwa kumiliki hata shule ya vidudu.

Hayo mambo hayakuja bahati mbaya.

Usitarajie eti nyerere laana ya mungu iwe juu yake alikuwa na mapenz na uislam na waislam kiivyo ya kupitiliza hadi eti afikie hatua ya kuanzisha chombo cha kuja kupigania maendeleo yao.

Kwa akili ya kawaida hiyo inagoma kbs kuingia akilin.

Hatuna shida na bakwta kwa sasa.

Tumeipuuza na wala hatuhitaji backup ya wanasiasa kulisimamia suala hilo.

Hakuna marefu yasiyo na ncha.

Kama muasisi wake nyerere laanatullah kafa bila shaka hata hili jinamiz lake litakufa tuh.
 
ok. basi hebu nieleweshe kidogo basi juu ya kile kilichotokea vatcan wakati wa kupiga kura za kuruhusu ushoga na mashoga. makadinali 62 walipiga kura ya ndio na 118 wakapiga ya hapana. na nasikia mwakani wajiandaa vema kupitisha ushoga kwa kishindo na hata wewe utaolea na mwanaume mwenzako kwenda kushughulikiwa. sasa kwa sababu siyajui mambo ya upande wenu kama ulivyosema, hebu basi nidokezee kidogo juu ya ulawiti wa watoto unaofanywa na makasisi kwenye madhabahu maana mimi sijui kitu. nitashukuru sana kwa kunielewesha juu ya hilo.


Masuala ya Dini ni Mazito sana.Wenye dini wenyewe ndio wanayaelewa.Kuna Dini inamheshimu M-bakaji mmoja ambaye alinajisi katoto ka Miaka Tisa huko Uarabuni,Vilevile kuna madhehebu yanaabudu NG'ombe.Kwa ujumla suala la Imani ni Zito na huwezi kulielewa kama upo upande wa Pili.Kinachotakiwa ni kufuata matakwa ya Dini yako na kuwaacha wenzako waendelee na ya kwao.
 
huelewi nini hapo sasa. wewe umesema sijui kikwete sijui mwinyi walikuwa marais, sasa hata kama ni waislam wataenda kinyume na mfumo? tumia akili. leo hii hata kama utakuwa muislam ukiwa waziri mkuu wa Uingereza lazima u-obey taratibu za kimalkia ambayo ndo kiongozi mkuu wa anglikana. naona wewe ndo mwenye mawazo ya ki-secondary.
tatizo hapo sio mtu bali mfumo uliopo.

Mbona sioni mahali uliopoweka huo mchele wako sasa?

Kama huna hoja acha ku-quote wanaume ovyo,nenda JF Photo huko ndo kunakufaa hii mada imekuzidi kimo
Kwa nini uhangaike na pumba?

Na kama unaona ni pumba chukua ukalishie nguruwe maana umenikomalia kweli ilhali hakuna chochote cha maana ulicho-comment kwenye mada.

Au unataka ligi tu?

Nimekuambia unikosoe nilipopotosha umekazana kupakazia tu.

Hivi una akili kweli wewe?

Acha nikupuuze.
 
Back
Top Bottom