Humo humu JF, kwa ajili ya kuhisi? Nimekuambia mimi ni Pagan uwezi kunikuta Jukwaa la Dini nachangia chochote kule hakuna Mapagan wenzangu, hata mimi nahisi wewe utakuwa Tambwe Hizza tuWe ritz, acha kudai kuwa jukwaa la dini hauingii, mimi nahisi unatumiaga ID ya F.F
CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam. Kama dhana hii itaendelea! Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana. Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!
heheheheeeeeeeee. Ritz hapo umehisi wrong! Huyo tambwe hizza simjui. Poa mkuu. Endelea na kazi iliyokuleta jf. 🙂Humo humu JF, kwa ajili ya kuhisi? Nimekuambia mimi ni Pagan uwezi kunikuta Jukwaa la Dini nachangia chochote kule hakuna Mapagan wenzangu, hata mimi nahisi wewe utakuwa Tambwe Hizza tu
heheheheeeeeeeee. Ritz hapo umehisi wrong! Huyo tambwe hizza simjui. Poa mkuu. Endelea na kazi iliyokuleta jf. 🙂
kumbe? Mimi nilihisi ndie Faiza Fox, maana amepotea jamvini. Akirudi Faiza Fox, utashangaa Ritz haonekani.Asikubabaishe huyo RITZ ndiye Tambwe Hizza mwenyewe.

Mkuu! Naona wengi wanajichanganya,mimi sitetei mambo DC aliyofanya! Ieleweke hivyo,na tafadhali isomeni post vizuri. Kumbukeni ni lazima kuiheshimu imani ya mtu! Kama wangetumia busara yote yangefika huku? Mimi nasisitiza CDM watuombe radhi! La sivyo kitakachofuatia watakijutia na kuomba radhi wakati huo watakuwa wamechelewa! Jamani mbona mambo yapo wazi? Tatizo kubwa la JF ni ushabiki. Ma great thinker wako wapi? Bandubandu humaliza gogo na kidogokidogo hujaza kibaba,hizi ni lawama CDM wanajikusanyia. Sijasahau kadhia ya uchaguzi mwaka jana kwa CDM kuwadharau Waislam kwa kumchukua mgombea mwenza darasa la saba,hii ni dharau ya hali ya juu! Na dharau nyinginezo,haya hayajengi na hayawezi kufanywa na watu makini.

Let us be scientific. Kama kuna reasobable suspicion kuwa uhalifu unataka kufanyika/zinapangwa mbinu za kufanya uhalifu na wahusika ni Askofu, sheikh, etc wamevaa mavazi ya dini , huwezi kuacha kumkamata kama sheria inavyotaka eti kwa sababu kavaa kofia ya uaskofu au kanzu etc. After all katika hali ya kumkamata mtuhumiwa, lazima purukushani zitokee, and common sense tells that a cloth just laid on the head without fixing support is likely and very likely to fall out. Tufikiri mbali zaidi tusilete udini maana kinachojitokeza zaidi hapa ni issue ya dini.
Mbunge wa CAF alikuwa Mwanamke alidhalilishwa kweli na Vyombo vya Usalama
1. Alipekuliwa na kuchekiwa na Polisi Mwanamme isivyopaswa na aliomba Mwanamke ampekue
2. Aliwekwa Rumande na Wanaume hata kubadili nguo ilikuwa shida
3. Alipigwa na kulazwa jela na wanaume kwa Wiki Moja
Kama ni upendo kwanini hawakukemea hali hiyo? Ina Maana hakudhalilishwa utu wake? au kwao yeye hafau sababu ni Mkristo?
Au ndio hiyo double standard ambayo nchi yetu chini ya CCM inataka kuibadilisha?
Kama hivyo vyombo vya kidini vanaanza kuangalia Mtu kwa udini ni dhambi hata kwa Mwenyezi Mungu...
Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislamu alisema Naibu mufti akiwa mjini Tabora, Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna. taarifa ya habari Radio Imani.
Mm ni muislamu kwanza na-declare interest lakini siungi mkono kitendo cha hawa wanaojiona viongozi wa dini yetu kuwa wanatoa matamko ya kipuuuzi km haya, Chadema ni ya waislam na wakristo i.e watanzania. Dini hairuhusu muislam kufanya vikao vya uhalifu (wizi) kisa eti kavaa hijabu. Ina maana leo sheikh mkuu akimbaka mtoto wa miaka tisa akiwa kavaa kanzu na kibaraghashia tutaacha kumshika? DC kwanza hajavuliwa hijabu hawa viongozi wetu wanatumiwa na wanasiasa mafisadi kiasi cha kufanya cc waumini wao kuwadharau.
CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam. Kama dhana hii itaendelea! Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana. Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!
Mkuu hatetewi mama ila suala la kumvua hijab/mtandio ambao unaambatana na imani ya dini yake ndilo suala hapa. Hao masheikh hawajaingilia siasa wamesema kuhusu vazi. Mambo haya huanza taratibu na kisha huwa makubwa na mara nyingine hupigwa fwatwa. Kumbukeni yaliyompata Mrema.