Bakhresa group punguzeni udini

Bakhresa group punguzeni udini

Status
Not open for further replies.
Bakhresa group au Azam kama wengi wanavyoifahamu kampuni hii, ina udini sana!

Sehemu zao zote walikowekeza ili upate kazi kipaumbele ni lazima uwe unaabudu Islamic; kwanini?!

Anzia kwa madereva wa maroli na gari ndogo ili upate kazi lazima uitwe Juma, Hamia, Hamis, Abdul, Aisha na majina fanani na hayo!

Viwanda vyote vya juice, biscuits na chocolate lazima uwe na sifa hiyo.

Hii si sawa kabisa!Hivi hawa akina John, Eliakim, Annastazia na wengine wengi wakiamua kususia bidhaa zako itakuwaje?

Hata Rwanda sasa wameanza kulalamikia jambo hilo. Mfagizi tu wa OFISI eti lazima awe Islamic! Na hata sasa nasikia una boti inayotoa huduma kiislamu pekee!

Tambua bidhaa zako hazinunuliwi na waislamu pekee na acheni ubaguzi!
Kwa hili nadhani itabidi walione mapema Na walipatie ufumbuzi maana ni wazi hili lipo hata counter zao za pale ferry booking office pia azam TV utakutana zaidi Na sura za kipemba tu
 
Hata mimi sisimamii upande wowote maana Bakhressa hata sura simjui. Nazungumzia uzoefu wangu kama mwajiri.

Nasema kuwa sheria ya kazi haimbani mwajiri binafsi aajiri nani na kwa misingi gani. Na pia siko hapa kushindana na mtu bali ni katika kuweka mambo sawa kwa manufaa ya wengine.

Ukitaka kunitukana ni hiyari yako.Mkuu siwezi kukutukana, naomba unisamehe maana moyoni ushahisi nimekutukana. Ila kwangu mimi kila post niliyo iweka hapa nimepata like za kutosha kuonyesha kukubalika kwa hoja hizo.uzito wa hoja huwa haupimwi kwa like, kama ambavyo watu wanaweza kufanana akili ndivyo hivyo pia wanaweza kufanana ujinga. Nakupenda na nakuheshimu sana ndugu yangu.

Pole sana kwa kukosa kazi kwa Ndugu Bakhressa.
 
Kwa hawa ulotaja alikuwa hana namna experience waliyonayo upande ule mwingine hawezi pata mtu
 
Hata mimi sisimamii upande wowote maana Bakhressa hata sura simjui. Nazungumzia uzoefu wangu kama mwajiri.

Nasema kuwa sheria ya kazi haimbani mwajiri binafsi aajiri nani na kwa misingi gani. Na pia siko hapa kushindana na mtu bali ni katika kuweka mambo sawa kwa manufaa ya wengine.

Ukitaka kunitukana ni hiyari yako. Ila kwangu mimi kila post niliyo iweka hapa nimepata like za kutosha kuonyesha kukubalika kwa hoja hizo.

Pole sana kwa kukosa kazi kwa Ndugu Bakhressa.
Mkuu siwezi kukutukana hata moyoni, naomba unisamehe maana inawezekana moyoni umehisi nimekutukana
Kuhusu wingi wa like ni kwamba like haziamui uzito wa hoja, kama ambavyo watu hufanana akili ndivyo hivyo pia huweza kufana ujinga. Nakupenda na kukuheshimu sana ndugu yangu.
 
Yaani hao walishikwa mkono na viongozi wa serikali .
Kampuni yake Kila kitu chake umpangie, vyenu vya Umma (SU) mmevibinafsisha vyote, wafanyakazi tukabaki kama vifaranga vya kuku vilivyofiwa na mama yao na kudhulumiwa juu, majengo yamebaki magofu, watu wanajitolea kuficha aibu ya nchi mnaanza midomo, mbona Mengi kajaza wachaga hamsemi, akiwa upande wa pili midomo juu, mkuu pambana na hali yako
 
Usitetee usichokijua,mkristo anayeajiriwa kwenye viwanda vya bakhresa ni lazima awe mtaalam au na kipaji,wafanyakazi wa chini wote ni waaslam,tena ukiwa shombe hata huandiki maombi,nywele zako ndiyo CV ya kukupa kazi.Povu ruksa
wabongo mna manenoo. nimewashindwa aisee. vipi kwa mzee mengi hakuna ubaguzi?
 
Sio kweli wewe ndo mdini unataka kuifanya Azam iwe Vatican na hilo haliwezekani Nazi wanatoa kulingana na sifa zako za taaluma husika sio Dini
Hivi nao watangazaji wa Azam wote ni Waislam ?
 
Mimi nilifanya interview na kushinda katika process ya kusign contract wakanifukuza walipogundua mimi ni Mkristo.

Natumia jina la Athumani, so they thought ni muislamu, walipogundua ni mkristo wakanifukuza

Tena katika mikataba yao kuna kipengele cha dini gani? As the qsn.
Hata polisi mahakaman,shule kote umeuliza dini gani tuanzie huko serikalini kwanza halafu time ipp na azam
 
Hujadanganya upo sahihi kabisa yani hawa wote hadi Mohamed mo, yan hata ukiomba field wanataka uwe Muslim na kama wa kiume uwe na hata mzuzu ndio wanakuamin, bint uwe umepiga baibui full hapo utapata. Ila uende smart tuuu na u Jackson wako, barua yako inafutiwa meza au kufungiwa vitafunwa
Mkaombe kazi CRDB na IPP huko mtapata, utaalamu huna unataka nani atolewe uajiriwe wewe?
 
Mleta thread una maana..'interview ni kujua kiarabu na juzuu kadhaa,halafu uwe na baraghashia na kanzu mpya,ama unatupia na suruali fupi...na makobanzi..

au sijaelewa?
 
Haya mambo ni kweli yapo, ila yana mizizi mikubwa sana na wala tusihukumu juu juu.
Waanzilishi wa kampuni hii ni muslim, na kama ujuavyo kuwa nchini kwetu kazi tunapeana kindugu au kwa kufahamiana ( ipo na wala usikatae) hivyo basi imetokea "wale kwa wale" ndo wanapeana kwa kuwa "wanafahamiana". Sio kweli kwamba kila muislam lazima apate ajira kama ataomba, ila wataopata ni "waislamu wenye ndugu zao mahala pale", mimi ni muislam na nilishawahi kukosa kazi kwa bakhresa na sikulalama, ni kwa sababu sina "anaenijua".

Tukienda mbele na tukirudi nyuma, kila kampuni huwa na sera zake ambazo wanahisi zitarahisisha "workflow" na kuongeza "efficiency" kwa namna waitakayo wao na hivyo kupelekea upande fulani unaoendana na sera zao kuangaliwa zaidi kuliko upande mwingine.

Mimi ni food technologists & nutritionist, niliwahi kukosa kazi world vision kisa tu sina cheti cha ubatizo na barua ya mchungaji, sikulalamika..! nikaelewa tu kuwa ni sera za taasisi na pengine mazingira ya kazi yangekua magumu kwangu kama nisingekuwa "yule wanayemhitaji".

By the way, sio kila kitengo huwa kina michezo hii, penye credit watu wapewe credit, Last time kuwa pale quality control department ilikuwa na wakenya wengi tu ambao sio 'waislam', hivyo tusiupe sana udini nafasi.

Natumai siku nyingine utafungua uzi mwingine kuelezea "ukabila na udini" kwenye kiwanda cha bwana "dk. Machache" kule "boo-night", naomba msumeno wako ukate kotekote.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom