Bajeti ya wizara ya kilimo awamu ya tano ilikuwa 250 bilion awamu ya sita 950 bilion. (Mkulima yupi amefaidika?)

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,827
21,456
Kuna clip ya Kibajaji nimekutana nayo mtandaoni ,eti bajeti ya wizara ya kilimo sasa ni bilioni 950.

Nimejiuliza Kibajaji amechukua figure za maandishi kwenye bajeti ya kilimo au fedha hizo zimeonekana wapi na zimefanya kazi gani?

Kibajaji hajui kuwa fedha zinazosomwa bungeni ni maandishi tu na hazipo popote?
Je, Tsh 950 zilizotengwa na bunge kwa ajili ya wizara ya kilimo zimefana nini na wapi na fedha hizo zilitolewa lini?

Kibajaji anaelezea kupatikana kwa soko la maparachichi huko China, wachina ni madalali wa uongo, hilo soko litaanza lini, ni akina nani watauza hayo matunda China, bei ya hayo matunda ni kiasi gani huko China, yatauzwa kwa muda gani?

Mbegu za hayo matunda zinapatikana wapi na kwa bei gani, yatasafirishwaje hadi China na kwa gharama gani? Maswali ni mengi kuliko majibu.

Kibajaji wewe ni mchumia tumbo, bei ya kahawa umeisoma wapi kuwa ni Tsh 2,000 kwa sasa? Au kahawa imekuwa tamu awamu ya sita na ilikuwa chungu awamu ya tano ikakosa bei?

Wanasiasa wanaofanana na akina Kibajaji na Musukuma tusipowaangalia kwa umakini wanawapotosha watanzania na wanatumiwa na wachache wanaolamba asali.
 
Ni jambo jema sana serikali inafanya. Na iungwe Mkono kwa hili. Hata hivyo, Tunahitaji kujua matumizi ya hizo hela na faida iliyopatikana.
 
Swali hapa ni hizo namba zimebadili kwa namna gani maisha ya wahusika.

Maana hapa unaweza kuta zinaishia kwenye akaunti za watu tu.
 
Ni jambo jema sana serikali inafanya. Na iungwe Mkono kwa hili. Hata hivyo, Tunahitaji kujua matumizi ya hizo hela na faida iliyopatikana.
Bajeti ya serikali ya mwaka 2022/23 iliyosomwa mwezi July 2022 hazijatolewa hata sent tano na serikali .
Hizo 950 bilion zilitolewa lini na zimepelekwa mkoa au wilaya ipi kufuata wakulima?
 
Bajeti ya serikali ya mwaka 2022/23 iliyosomwa mwezi July 2022 haitolewa hata sent tano na serikali .
Hizo 950 bilion zilitolewa lini na zimepelekwa mkoa au wilaya ipi kufuata wakulima?
Maswali yako ni ya msingi. Ujibiwe kwa ufasaha.
 
Bajeti ya serikali ya mwaka 2022/23 iliyosomwa mwezi July 2022 hazijatolewa hata sent tano na serikali .
Hizo 950 bilion zilitolewa lini na zimepelekwa mkoa au wilaya ipi kufuata wakulima?
Ungeleta na ushahidi kuwa wizara ya kilimo haijapokea hata mia ,vinginevyo ni umbea unauleta hapa
 
Wanagawana fedha Za Bajeti ya kilimo wanasema fedha zimepelekwa kwa wakulima bilion 950
 

Attachments

  • IMG_6511.MP4
    8.1 MB
Ndio maana sheli kila kona.

Taifa limegeuka kuwa kituo cha mafuta rasmi.
Sheli bubu hizo watu wanapiga dili zao nyingine sio sheli mkuu, usione shell ukajua ni shell ya mafuta hivyo ni vituo vya kazi zao za kipigaji, umewahi kuona gali la mafuta likipekuliwa ndani lina nini?
 
Bil 250 mbegu ya mahindi ilikua TSH 10,000 Kwa 2kg, mbolea TSH 45000. Bil 950 mbegu ya mahindi 15000 Kwa 2kg, mbolea laki 1.1 bila ruzuku na 70 elfu Kwa ruzuku.
 
Back
Top Bottom