Bajeti ya mchakato wa katiba mpya iko wapi?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,240
Nimefuatilia hotuba yako ya bajeti ya 2023/24 lakini sikumbuki kusikia bajeti kwa ajili ya mchakato wa katiba mpya, je mchakato huo utafanyika kwa kutumia kifungu gani cha fedha?

Wananchi wanasubiri kwa hamu kubwa kuanza kwa mchakato huo ili hatimaye tupate katiba ya wananchi.
 
Katiba ya nini...?watu tunataka ajira sio makaratasi..by the way hii iliyopo inafaa sana
 
Pesa itapatikana tu ondoa shaka.

Muda wa KATIBA mpya umefika,

HAIZUILIKI.
 
Ilikuwa danganya toto, ni aibu kwa kiume kupigwa changa la macho
 
Nimefuatilia hotuba yako ya bajeti ya 2023/24 lakini sikumbuki kusikia bajeti kwa ajili ya mchakato wa katiba mpya, je mchakato huo utafanyika kwa kutumia kifungu gani cha fedha?

Wananchi wanasubiri kwa hamu kubwa kuanza kwa mchakato huo ili hatimaye tupate katiba ya wananchi.

Lakin mim nawalaumu sana wapinzani,Kwanin wakat wa katiba pendekezwa waliamua kutoka nje?angalau wangebaki bungen wakapambana ikapatikana hata kama ingekuwa na mapungufu yangekuja kurekebishwa sasa kitendo cha kutoka nje ilikuwa mistake kubwa sana
 
Katiba ni mfumo, ni sawa na msumeno kukata mbele na nyuma, ni nani yuko tayari kwa hilo?
 
Mods nimemuuliza Mwigulu ili ajibu na yumo humu ninyi mnaondoa jina lake, mna maslahi gani na Mwigulu?
 
KUSITA KUTENGENEZA KATIBA MPYA KUNATOKANA NA NINI? USHAHIDI WA YANAYOTOKEA KWENYE UCHAGUZI NI JIBU TOSHA LA HITAJI LA KATIBA, UFISADI UNAOSEMWA NA CAG, KUKIRI MKAPA KUWA WALIIBA ALAFU HAKUNA WA KUMFANYA KITU! JE TUNAJIPENDA ILA NCHI HAIPENDWI? KIPINDI HIKI DUNIANI KOTE NI KIPINDI CHA UHURIA, HAKI NA UWAZI! SASA KATIBA YA UJAMAA WA 1967 HAINA TIJA! HATUONI? WATU WAFANYEJE NDO IELEWEKE KUWA KATIBA YA UHURIA, DEMOKRASIA NA HAKI KWA SASA INAHITAJIKA TENA IMECHELEWA SANA!. MFANO. KUGOMBEA URAIS NA UBUNGE NDANI YA VYAMA NA BAINA YA VYAMA HUJITOKEZA WATU WENGI SANA KUTAKA HIYO NAFASI. SASA MTU ANAPOSHINDA KIMAGUMASHI WALE WASHINDANI HUJISIKIAJE? JE ITAKUWA AMANI? JE UNAPOONGOZA WATU WASIOKUCHAGUA UTAKUWA NA UJASIRI? HALAFU KUBWA NI KWAMBA MAMLAKA HUTOKA KWA WANANCHI KUMCHAGUA MTU WANAYEMUONA ANAFAA. KUJIWEKA KIMAGUMASHI NI KUWATWEZA WANANCHI! INAPASWA KUSHINDA NA KUSHINDWA KUNAKUWA PEUPE/ WAZI KABISA ILI AMANI IWEPO NA WASHINDANI WAPONGEZANE NA KUTAKIANA HERI NA HAPA NDIPO TUPATAKAPO KWA SASA NA AMANI YA NCHI BILA SHAKA ITADUMU, USTAARABU UTAKUWEPO NA UCHUMI UTAKUA
 
Nimefuatilia hotuba yako ya bajeti ya 2023/24 lakini sikumbuki kusikia bajeti kwa ajili ya mchakato wa katiba mpya, je mchakato huo utafanyika kwa kutumia kifungu gani cha fedha?

Wananchi wanasubiri kwa hamu kubwa kuanza kwa mchakato huo ili hatimaye tupate katiba ya wananchi.
Hakuna Bajeti Hakuna Katiba mpya ni DANGANYA YA CCM
 
Back
Top Bottom