Bajaj ya wajawazito - Ahadi imetimia!

Bajaj ya wajawazito - Ahadi imetimia!

Pomole

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2011
Posts
257
Reaction score
8
Hapa ni ktk uzinduzi wa bajaj ya kubebea akina mama wajawazito wakati wa uzazi.Gharama yake ni dola 5900 (8.5milioni).Nikikumbuka vema hii ilikuwa ahadi ya mgombea wa ccm kuwa akichaguliwa ataleta bajaj kuondoa kero na vifo vya wajawazito.Wengine tunaiona kama guta,sijui wana jamii forum-tunalipokeaje hili!Itakidhi haja



attachment.php
 
Hivi kweli mwanamke na mimba akiwa na uchungu wa kuzaa ndiyo anabebwa hadharani namna hiyo?
hiyo dola 5900 si ingetosha kununua hata Toyota Noah used, badala ya udhalilishaji huu?
kwa kweli watanzania tumejaliwa kupata Rais kituko.
 
mi nilishangaa sana nilivyoiona hiyo guta tangu jana...hope tutastaajabu mengi miaka hii
 
kwa hesabu ya harakaharaka kwa pikipiki 400 zimegharimu kiasi cha bilioni3.4 wabunge wetu wako kama mia 300 ivi na kila mmmoja anapewa millioni 90 kwa ajili ya gari ivo ukipiga hesabu ya haraka unaona wanatumia bilioni 27.hivyo viongozi wetu wameona ni heri wanunue bajaji ya milioni 8.4 ambayo itahudumia zaidi ya wajawazito mia na huku wakinunua vx ambayo itahudumia mbunge mmmoja,
tafakari
 
Kwa unafki huu,itatugharimu maisha kupata viongozi! Karne hii bajaji? Kazi tunayo
 
attachment.php

Naona muda wa kula ban unaninyemelea ngoja ni sepe....
 
etiiiiiiiiiiiii................. haya mambo yametokea tanzania?................. ndiyo JK aliyoahidi??? naomba mnionyeshe njia ya tahrir square................. please!!!!!!!!!
 
Hii ni akili au matope? Sijaui hata walianzaje kuwaza kuwaweka wajawazito kwenye pikipiki, selfishness ya hawa watu imefika level za ajabu kusema ukweli.
 
Yaani viongozi wamejisahau kabisa sasa nadhani hayo ma Vx yamewalemaza.
Kwenye barabara za vumbi mbavu za mbwa vijijini kwenye magari ya kawaida tu ni mateso, na mimi ni kijana mwenye nguvu zangu, ndo itakuwa mjamzito? Si atameza vumbi lote kwenye hiyo kitu! Na pikipiki shock yote ya barabara atakuwa anaipata ile yenyewe.
Hii inatia kinyaa kweli.
 
Mvua ikinyesha sijui itakuwaje...ama kweli

siyo mvua tu, ................imajini milima ya pande za kimara bila four wheel hufiki popote na pale ndio mjini!................. vijijini itmudu nini?.......... these people are crazy...........crazy, crazy, crazyyyyyyyyyyyyyyyy....................
 
Naomba tu ninyamaze... naona hasira hata kuchangia!
 
Hako ni kamradi kengine ka kuchota pesa za walipa kodi, Hivi pesa za kufanyia service/maintenance za hizo bajaji zitatoka fungu gani?
TUTAFAKARI PAMOJA
 
Naomba kujua zitakuwa zinaendeshewa barabara zipi, na usalama wa mgonjwa au ndo badala ya kujifungua kwa uchungu wa kawaida watakuwa wanajifungua huko wanafungwa POP za kuvunjika miguu kwa ajali. Ama kweli TZ tumefikwa na JANGA JINGINE LA KITAIFA.
 
hakyanani kuna watu hawfikiriii hata kwa kuwasingizia... we na akili zako mgonjwa umbebe kwenye pikipiki ya miguu miwili na kitela cha pembeni... it is very risk... huwezi kuwa na akili timamu hata kufikiri hili kuna vitu havina option ... kitu kama ambulace ni kitu kinachotakiwa kiwe salama kwa 100% and risk free.. we niambie hicho kibajaji kiwe kwenye main road... upepo wa gari tu utakisukuma.
grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr ah nimechoka
 
aaaaaaaaaaaagggggh sijui nisemaje,aaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhhhhhh tumechoooka sasa miaka 50 ya uhuru na huo upuuuuzi
 
Hii bajaj nimeitanguliza kama trela,nitakuja baadae na guta inayofanya kazi ya kubeba wagonjwa na serikali inaitambua!Niliikuta wilaya moja ya pwani-stay tunned
 
Hivi hizo bajaj zina uwezo wa kuhimili mikiki na mihangaiko ya uchungu wa mama anapotaka kujifungua???

......................................................
 
Namshukuru muheshimiw kwa kutimiz ahadi, ni msaada mkubwa hasa kwa watu wa vijijini ambo walitegemea vichanja au baiskeli kufika hospitali...,....smthng its better than nthng....
 
Back
Top Bottom