Bado unawaza utaanzaje ujenzi? Anza na hii kwa mchanganuo huu

Mkuu, asante kwa kutupa muungozo huu wa bure, Ikikupendeza naomba utupatie pia mchanganuo wa idadi ya materials zilizo akisi gharama hizi.
Asante!
Hapo ndio kuna mtihani. Amewekaweka tu vitu visivyo na uhalisia. Hiyo nyumba huwezi kunyanyua mpaka level ya paa kwa milioni 7 tu maana hiyo hela labda itaishia kwenye msingi tu

Kuweni watu wa uhalisia ndugu zangu mambo ya uongo uongo yanaharibu credibility ya kampuni
 
Mkuu, asante kwa kutupa muungozo huu wa bure, Ikikupendeza naomba utupatie pia mchanganuo wa idadi ya materials zilizo akisi gharama hizi.
Asante!
🙏🏾Mkuu.
Nilijaribu hivo lakini ikawa maandishi too much mpaka yanaingiliana. So niliamua kuchagua eidha kuweka ‘quantity of material’ pekee au niweke price pekee.
Kwa alie serious anaweza kunitafuta
 
Gharama ni kubwa Sana yaani kwa sisi wabana matumizi hadi kupaua haitakiwi kuzidi mil.8 sasa hiyo yako inaenda hadi mil.14
Ikiwaa gharama kubwa lakini ‘realistic/relevant’ sio shida. Shida ni inapowekwa gharama kubwa au ndogo lakini haireflect uhalisia inamaana inakua ni upotoshaji.

Sasa itafuatana wewe unapunguza gharama kwa namna gani kwa kufanya vyumba viwe vidogo kama store au kwakuchakachua material. Mimi nimefanya kitu halisi kulingana na ramani husika.

Mfano kuna jamaa kigamboni walikua wanauza nyumba zilizokamilika (hadi full finishing) za vyumba vitatu kwa 17mln. Sasa ukiwatafuta mafundi waliozijenga ndio utajua cheap is not always the best option
 
Hapo ndio kuna mtihani. Amewekaweka tu vitu visivyo na uhalisia. Hiyo nyumba huwezi kunyanyua mpaka level ya paa kwa milioni 7 tu maana hiyo hela labda itaishia kwenye msingi tu

Kuweni watu wa uhalisia ndugu zangu mambo ya uongo uongo yanaharibu credibility ya kampuni
Nipo real sana hapo boss, sijaweka kwa maamuzi yangu tu. Ila gharama hizo zimetokana na hesabu ya material husika.

Tatizo mnakuja kuponda bila reference figures.

Ishu sio vyumba vitatu au vinne au vitano ishu ni ukubwa wa jengo kwa ujumla.

Kama hiyo Wewe unasema ni ndogo sana na kuna mwingine kasema ni kubwa sana (nafikili unapata picha hapo). Inawezekana wote mpo sahihi kwa reference zenu wenyewe.

Hiyo 7million kuishia kwenye msingi ni nyingi sana. Sijui Wewe unazungumzia nyumba ya ukubwa gani
 
Hapo ndio kuna mtihani. Amewekaweka tu vitu visivyo na uhalisia. Hiyo nyumba huwezi kunyanyua mpaka level ya paa kwa milioni 7 tu maana hiyo hela labda itaishia kwenye msingi tu

Kuweni watu wa uhalisia ndugu zangu mambo ya uongo uongo yanaharibu credibility ya kampuni
Unanyanyua hadi kupaua kwa bei gani ?
 
Ahsante kwa hamasa mkuu. Naomba ufafanuzi wa haya mambo mawili, naam yapo matatu.

1. Hiyo gharama ya bati umeweka ni bati za kampuni gani?

2. Pia mbao ni zile treated?

3. Kama gharama za maji na ufundi zitategemea na eneo, hali kadhalika tofali nazo zinatofautiana bei kati ya eneo moja na lingine kutokana na upatikanaji wa mchanga, maji na cement.
1. Hiyo bati ni migongo mipana gauge 28 nimetumia reference ya bei za sunshare (naamini ndio wengi wanaifaham kwa reference ya mdau humu jf).

2. Yes mbao ni treated.

3. Upo sahihi na kwa vyovyote gharama haziwezi kuwa exactly, bali zinaweza kupungua kidogo au kuongezeka kidogo
 
Makadirio yapo pouwa maana mimi kuna ambayo nilifanyiwa bila kupaua gharama ilifika milioni 11...
Hapo bati ni migongo mipana gauge 28 (reference price ni ya sunshare).

Mchanganuo wa material upo, nimeweka hivo ili raia wapate picha tu ndio maana nikaweka na layout ya floor plan.

Labour charge boss haitegemei sana idadi ya vyumba bali ukubwa wa jumla wa nyumba. Nyumba mbili tofauti za vyumba vitatu zinaweza kukupa gharama za ufundi zenye tofauti kubwa
 
Back
Top Bottom