Unataka kuanza ujenzi? Hii option nafuu zaidi

Black Thought

Senior Member
Feb 25, 2015
160
406
Hesabu hii ni kwa ujenzi wa Nyumba simple ya vyumba vitatu (kimoja master)
Ikiwa na upana wa mita 9.5X10.4

KUJENGA BOMA
tofali (jumla) ...... 3,130pc
mchanga ......... 16m3
saruji ............... 113 mifuko
kokoto ................. 9 m3
Nondo ................ 71pc
ringi (stirrups) ...... 594pc
binding (waya) ...... 10kg
misumari ............... 10kg
mbao (kukodi) ......... 67pc
mbao (kununua) ...... 25pc
maji ........................ ____________
Ufundi ...............................________
JUMLA ................ = Tsh. 7,817,800 (makadirio kwa dar)

Material yanahusisha ujenzi wa tofali zote, mikanda yote juu na chini na zege la kufunika baraza/veranda.
Gharama za maji na mchanga zinategemea sana sehemu unayojenga.
Gharama za nondo zinaweza kupungua kulingana na stability/uimara wa ardhi ya kiwanja.

KUPAUA
Bati (Gauge28 Alaf)... 42pc = Tsh. 1,344,000
misumari ............. ..20kg = Tsh. 60,000
misumari ya bati ..9pkt = Tsh. 63,000
mbao 2X2 ........ 65pc = Tsh. 195,000
mbao 2X4.... 72pc = Tsh. 426,000
kench waya ...5pc = Tsh. 10,000
flash covers ... 8pc = Tsh. 104,000
synroof ……60lita = Tsh. 690,000
fabric wp membrane 30m = Tsh. 105,000
Ufundi .... _______
JUMLA = Tsh. 2,994,000


Note: Ujenzi huu ni wa viwango vinavyokubalika na ni kwa hatua ya kuinua boma na kuezeka tu bila kuhusisha ‘finishing’. Nyumba hii inakua wazi upande wa nyuma, hivi hakuna gutter.

Pamoja na finishing yote kukamilika inakadiriwa kuwa kati ya 35-40mln

D5CF9EEC-C1DC-4F69-8AB6-77B502A18EDA.jpeg
 
Back
Top Bottom