Ujenzi rahisi kwa kutumia interlock blocks, jenga popote, jenga sasa

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
2,330
2,283
Interlock blocks au bricks ni aina ya tofali zinazofungamana kwenye ujenzi bila kutumia zege(motor) kuziunganisha,zinapigwa kwa saruji na udongo wenye mfinyazi kiasi. Tofali hizi zinatumia saruji kidogo sana(10%) tu ya udongo. Hizi tofali zipo miundo mingi sana lakini nitazungumzia aina ya Hydraform.
IMG_0431.JPG

Hydraform ndio waasisi wa teknolojia hii ya tofali lakini kulingana na soko kila sehemu wanatengeneza mashine.

Aina hii ni maarufu sana Tanzania
Mashine ya kupiga Hydraform inatumia hydrolic ambayo ina uwezo wa kupiga tofali zaidi ya 2000 kwa siku kwa kinu kimoja.

hydraform_220mm_block2_gif.gif()(D883A662DE8E5F4906C451AED35691A0).gif

Kuna mashine za mkono pia ambazo kwa kinu kimoja kinapiga tofali 400.
Uzuri wa Hydraform unapiga size unazotaka za urefu wa tofali na vipande vyake bila kuja kukata wakati wa ujenzi.
Urefu wa tofali huanzia nchi 18-24 na upana ni nchi 9 na 6 na kimo ni nchi 5.
Mfuko mmoja wa saruji unaweza kupiga tofali 80 mpaka 100 ikitegemea na aina ya udongo uliopo eneo lako.

URAHISI WA UJENZI WAKE HUU
1.Baada ya kuwa na tofali kinachofuata ni ujenzi au kupandisha boma lako. Tofali ya kwanza baada ya msingi ni kuset boma. Ujenzi wake ni rahisi kwa sababu hakuna haja ya motor kwenye kupandisha boma lako,utapachika tu ila utazingatia kanuni zote za ujenzi.

2.Hakuna haja ya plasta na skim baada ya ujenzi wako,hapo utaokoa saruji,mchanga,maji na gharama za fundi.

3.Kuhimili mitikisiko na vishindo hivyo si rahisi kuona nyumba hizi zikiwa na ufa sababu tofali zinapumua. Kama itatokea tetemeko au bomoa bomoa unaweza kuhama na tofali zako.

Faida ziko nyingi na kitaalamu ujenzi wa tofali za kufungamana unapunguza 40% ya gharama za ujenzi, mfano kama ulipanga kujenga kwa milioni 10 basi huenda ukatumia milioni 6 tu.

Karibu kwa mnaotaka kujenga,iwe ni kwa awamu kulingana na uwezo wako au kwa pamoja pia. Gharama zetu ni rafiki kabisa.

Kama una fundi wako karibu tukuuzie tofali. Kuna option mbili za kupata tofali.
1.Tofali moja tutakuuzia Tsh.650 kwa ndani ya Dar na maeneo ya jirani mikoani tutaelewana tu.
2. Tunaweza kukupigia tofali kwa Tsh. 250 ikiwa utanunua matirio yote mwenyewe.


IMG_20220713_141643.jpg


Kama una maoni au swali karibu uulize na utajibiwa iwezekanavyo.

MAWASILIANO YETU
Tupigie simu au WhatsApp 0625547181
Telegram t.me/ujenzirahisi
Facebook @ujenzirahisi
Instagram @ujenzirahisi
Tiktok @ujenzirahisi
KARIBU UJENZIRAHISI TUKUJENGEE UTAKAVYO,IWE NI KIDOGO KIDOGO AU KWA PAMOJA
 
Hizi tofali pia sio lazima uwe na sementi kama una udongo mzuri mfano wa kichuguu uhitaji sementi.
Kama hakuna kichuguu na uhitaji kutumia cement kupunguza gharama ,upate au utengeneze mashine ya kuweza kukandamiza psi 200 nguvu ya hydrolick zinakuwa imara pia. Hii mashine inakandamiza udongo mkavu kwa nguvu hio ya psi 200 hili tofali ni imara unajengea vizuri
 
Ongezea no 4.zinapunguza mda wa kujenga ndani ya wiki boma limesimama hii ni nzuri kwa wasio mda wa kusimamia ujenzi mfano wakaao nje ya nchi, au mikoani ndani ya mda wa likizo ya mwezi mmoja tu mtu anakabidhiwa nyumba yake, si unajua uaminifu hakuna we mtumie mtu akusimamie ujenzi ukutane na kituko, akiwa muungwana atajenga two in one yaani nae atajenga yake kupitia yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom