Bado unawaza utaanzaje ujenzi? Anza na hii kwa mchanganuo huu

Black Thought

Senior Member
Feb 25, 2015
160
406
Bado unajiuliza unaanzaje ujenzi?
Unaweza kuanza na ramani kama hii ya vyumba vitatu (master, self, na plain bedroom) kujenga.

KUJENGA BOMA
tofali (jumla) ...... Tsh. 3,100,000
mchanga ......... Tsh. 300,000
saruji ................ Tsh. 1,500,000
kokoto ..................Tsh. 400,000
Nondo ........................... 1,178,000
ringi (stirrups) ............ 150,000
binding .......................... 30,000
misumari ..................... 35,000
mbao (kukodi) .............. 150,000
mbao (kununua) ........... 52,000
maji ........................... 500,000
Ufundi ...............................________
JUMLA ....................... = Tsh. 7,395,000

Note: Gharama ya maji inaweza kubadilika kulingana upatikanaji wake sehemu unayojenga. Na gharama ya nondo inaweza kupungua kulingana na stability ya eneo unalojenga.

KUPAUA
bati ................ Tsh. 2,300,000
kofia ............. 600,000
valley .............. 320,000
misumari ............... 136,000
misumari ya bati ...... 140,000
mbao 2X2 ...........720,000
mbao 2X4.............1,368,000
kench waya .......... 14,000
Ufundi .... _______
JUMLA = Tsh. 5,598,000

Gharama za ufundi zitategemea sehemu unayojenga na fundi uliemtumia.

Note: Ujenzi huu ni wa Viwango vinavyokubalika sio low standards, mfano (mortar) kwa kawaida mfuko mmoja wa saruji unajenga tofali 45 za msingi, lakini unakuta baadhi ya mafundi (wahusika) wanajenga mpaka tofali 60 kwa mfuko n.k

KAMA UTAHITAJI KUJUA GHARAMA ZA UFUNDI Au KUPATA RAMANI KAMILI KULINGANA NA KIWANJA CHAKO NICHEKI WHATSAPP 0717682856

F1CCCD70-C180-4015-9199-28DF7DC2F846.jpeg


0D4CB717-4466-45E1-95E6-A4437D089D88.jpeg


47E5CDA5-0A8C-4F5A-9301-C1910EA0DF4F.jpeg
 
Mara nyingi huwa tunaweka idadi ya material tu, but wengi hupenda kuona gharama. Ila mchanganuo wa idadi ya material upo kwa atakae Hitaji
Mkuu, asante kwa kutupa muungozo huu wa bure, Ikikupendeza naomba utupatie pia mchanganuo wa idadi ya materials zilizo akisi gharama hizi.
Asante!
 
Mara nyingi huwa tunaweka idadi ya material tu, but wengi hupenda kuona gharama. Ila mchanganuo wa idadi ya material upo kwa atakae Hitaji

Ahsante kwa hamasa mkuu. Naomba ufafanuzi wa haya mambo mawili, naam yapo matatu.

1. Hiyo gharama ya bati umeweka ni bati za kampuni gani?

2. Pia mbao ni zile treated?

3. Kama gharama za maji na ufundi zitategemea na eneo, hali kadhalika tofali nazo zinatofautiana bei kati ya eneo moja na lingine kutokana na upatikanaji wa mchanga, maji na cement.
 
Gharama ni kubwa Sana yaani kwa sisi wabana matumizi hadi kupaua haitakiwi kuzidi mil.8 sasa hiyo yako inaenda hadi mil.14
Makadirio yapo pouwa maana mimi kuna ambayo nilifanyiwa bila kupaua gharama ilifika milioni 11

Kupaua angeweka wazi ni kampuni gani ya bati zitatumika kama ni Alafu (ambayo bei imechangamka kidogo ) au kampuni zingine za mabati

Na kizuri zaidi angeweka labour charge mfano kwa nyumba ya

1.ya vyumba viwili ni sh ngapi
2: vyumba vitatu?
3:vinne

Na material angechanganua misumari kilo ngapi bei ambayo total yake ni sh ngapi
 
Back
Top Bottom