Bado huamini katika uchawi na ushirikina? Waulize madereva

Bado huamini katika uchawi na ushirikina? Waulize madereva

Mshana sitaki kupingana na wewe kwa asilimia mia moja lakini napenda kutoa uzoefu wangu kidogo. Mazingira tunayokulia yana mchango mkubwa sana katika makuzi yetu na imani zetu. Nimezaliwa ktk mazingira yanayoamini ushirikina sana, nimekua nikiiaminishwa habari za uchawi kama vile nilivyokuwa naambiwa habari za dini. Nimekuwa nikijua wachawi muda wao ni usiku wa manane, wanalimisha watu usiku, wanachukua watu misikule nk. lakini ktk hayo yote baada ya kuwa na akili za kiutuuzima nimegundua katika karibu yote yalikuwa ni mambo ya kusadikika tu, hayakuwa na uhalisia.kuna uhusiano wa karibu sana kati ya imani za uchawi na umaskini, uchawi na kiwango cha elimu, jaribu kuangalia maeneo yenye imani sana za uchawi na maendeleo ya watu wa sehemu hizo.sifahamu umri wako, miaka ya 80 na tisini mwanzoni kwa wapenzi wa mpira wa miguu wanakumbuka simba na yanga na mambo yao ya uchawi, ilifika wakati hata mpira wa kuchezea ulikuwa unanuliwa na kulindwa na wazee wa hizi klabu mbili ili usirogwe( tulikuwa wajinga sana hasa FAT) na mbona haturogi basi hata kuchukua ubingwa wa Africa tu!! hivyo mambo mengi yanaonekana uhalisia wake kwa macho ya kiimani tu na sio macho yetu ya kawaida, ni kama unavyoamini kuna mbingu na kuna watu wanaiona lakini inaonekana kihalisia kweli??!!
 
Naamini uchawi upo ingawa sijawahi kulogwa au kukutana na kitu cha kichawi ila nakumbuka siku moja usiku hukooo Ifakara kwenye safu ya milima Udzungwa nilikuwa natembea usiku nikaona kitu kirefuuu ila sikujua ni nini kwa akili za haraka haraka za kiswahili nikahisi ni Jini hapa ndipo wengu wetu hukosea. Ukiona jambo unaleta moja kwa moja kwenye uswahili unaweza kuta mda mwingine ni mti tu ila sababu akili yako inawaza kwamba upo porini na ni usiku na kuna historia za kutisha eneo hilo basi unachukilia ndio kitu chenyewe sababu mda mwingine natembea usiku nahisi kuna mtu kasimama mbele nasita kwenda baada ya mda naenda nakuta na kumbe ni mti tu.

Hakuna mtu ambaye hajawahi kurongwa unaweza kurongwa na usijijue ila mambo yako mengi hayaendi unapanga hiki hakifanyiki pesa haikai ujue unachezewa ila hujijui
 
Mkuu Mshana - Nadhani hizi habari za madeveva kuwa wameona kitu barabarani kabla ya ajali ni kutaka kujitoa tu na lawama maana hiki ndio kimekuwa kisingizio kikubwa ambacho hamna anaeweza kumpinga kuwa hakuona machawi - yaani hakuna ushahidi kutoka pande zote mbili kuwa aliona au hakuona kwa hiyo dereva mzembe anaokoka
Unaamini unacho amini kuwa kipo
 
Usiseme ivo nakumbuka wakati nipo form 1 nlimwambia mamangu mkubwa kua siamini kama uchawi upo aliniziba mdomo ili watu wengine waisikie! Nikikuja kuamini baadae nilipoenda MBEYA kua uchawi upo na watu wengi wanateseka kutokana na uchawi. Lakini pia nimegundua kuwa Mungu anaokoa sana.... NDIO MAANA IMEANDIKWA WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA
ndg yangu Mbeya ni mbali sana.
nenda hapo ilala uone watu walivyo machizi kisa nyumba za urithi za wazazi wao ndipo utajua uchawi upo ama laaa
 
Mkuu Mshana - Nadhani hizi habari za madeveva kuwa wameona kitu barabarani kabla ya ajali ni kutaka kujitoa tu na lawama maana hiki ndio kimekuwa kisingizio kikubwa ambacho hamna anaeweza kumpinga kuwa hakuona machawi - yaani hakuna ushahidi kutoka pande zote mbili kuwa aliona au hakuona kwa hiyo dereva mzembe anaokoka
Unaamini unacho amini kuwa kipo
kwenye vitabu vya dini uchawi na ulonzi upo na umeandikwa.
tena Musa aliwaambia wana wa Israel "usimwache mwanamke mchawi akaishi"
lakin Mungu aliwaahidi watu wake hakuna uchawi utakao fanyika juu yao
 
Kama ni vitakatifu kwanini vinatofautiana ilihali mnasema ni vya mungu mmoja?
Think big pal! Ikulu ni Moja lakini ina main gates zaidi ya Moja na ndani yake kuna milango kibao ya kuingilia
Dar ni moja lakini kuna exit ngapi?
 
Think big pal! Ikulu ni Moja lakini ina main gates zaidi ya Moja na ndani yake kuna milango kibao ya kuingilia
Dar ni moja lakini kuna exit ngapi?
kaka mshana humu nina uhakika kuna wanywa virobo ma walevi ambao huja umu kupinga tu na kubishana ndio mioyo yao inapata akili.zaidi naweza waita misukule
Wasamehe bure
 
kaka mshana humu nina uhakika kuna wanywa virobo ma walevi ambao huja umu kupinga tu na kubishana ndio mioyo yao inapata akili.zaidi naweza waita misukule
Wasamehe bure
Heri kiroba maana hakileweshi kama hayo mauzauza yenu mnayoamini mpaka mnaitwa makondoo.
Na usukule ndio huo huo mnaaminishwa upumbavu mnakubali pasipo kuhoji.
 
Back
Top Bottom