Bado huamini katika uchawi na ushirikina? Waulize madereva

Bado huamini katika uchawi na ushirikina? Waulize madereva

Mada iliyopita tumezungumzia kuhusu uchawi na ushirikina kwenye mahakama zetu... Hapa tunaangalia eneo lingine muhimu BARABARA ZETU.

Madereva katika hili ndio wanaweza kuwa mashahidi wazuri sana kwakuwa ni wahanga wakubwa na hivi vitu wanakutana navyo sana, hasa madereva wa daladala, mabasi ya mikoani na magari ya mizigo

Uchawi wa barabarani uko wa aina nne
1. Uchawi unaomhusu mmiliki wa gari husika... Hii mara nyingi ni kwa ajili ya kutoa kafara kwa ajili ya kulinda au kuongeza utajiri wake, baadhi hujui kabisa kuwa gari lake siku hiyo litapata ajali na watakufa watu kadha. Madereva wanaostuka huacha kazi ghafla

2. Uchawi unaohusisha vilinge na njia za wachawi.... Hawa watu huwa hawapishi kitu au mtu, kwahiyo ukiingia kwenye anga zao ujue wa kuumia ni wewe, ndio maana ajali nyingi za barabarani dereva atakwambia aliona mnyama au mtu au kitu akajaribu kukikwepa ndio ajali ikatokea... Kamwe hutakiwi kukwepa

3. Uchawi unaohusisha roho zinazotangatanga, mapepo mizimu na mashetani, hizi huwa ni tamaa tu ya kuua kunywa damu au kuleta maafa na majonzi katika jamii

4. Uchawi unaomhusu dereva mwenyewe au mfanyakazi wa gari, maisha magumu na tamaa ya mali husababisha watu wafanye mambo ya ajabu, dereva anaenda kwa mganga na kupewa sharti la kupindua gari watu wafe mambo yake yanyooke, lakini pia wengine huambiwa kuwa anakosa kazi kwasababu ya fulani hivyo hutegeshewa Phantom na kupindua gari, akisalimika kifo anabaki na ulemavu

Ya barabarani ni mengi tusiyoyajua, magari mengi yamezindikwa, Madereva wamezindikwa wafanyakazi wamezindikwa tiketi zimezindikwa.. Unapofika salama ni kumshukuru Mungu na ndio maana tunasisitizana sana kufanya ibada Sala na maombi kwa imani zetu kabla ya kuanza safari.
Nafikiri Tz tunaongoza kwa ushirikina! Kila kitu kuzindika?!!
 
Ya barabarani ni mengi tusiyoyajua, magari mengi yamezindikwa, Madereva wamezindikwa wafanyakazi wamezindikwa tiketi zimezindikwa.. Unapofika salama ni kumshukuru Mungu na ndio maana tunasisitizana sana kufanya ibada Sala na maombi kwa imani zetu kabla ya kuanza safari.[emoji2827]
 
Hivi kwanini tunasema eti ulaya hakuna hivi Vitu? Hivi ni uvivu wa kusoma na kufikiri au? Wenzetu hawakuishia kubisha tu bali walifanya kwa vitendo, walitegesha powerful automatic cameras na wakapata majibu ya kushangaza kwenye zile sehemu zinazosemwa vibayaView attachment 313555View attachment 313556View attachment 313557
Hakuna cameras zinaweza piga picha spirits. Acheni kudanganya watu.eti very powerful camera....🤣 Ni uongo.hizi ni picha toka kwenye movies
 
Back
Top Bottom