KERO Madereva wenye dharau barabara ya Mbeya - Tunduma

KERO Madereva wenye dharau barabara ya Mbeya - Tunduma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na dharau nyingi zinazofanywa na madereva wanaotumia barabara ya kutoka Mbalizi kuelekea Tunduma.

Madereva hao wamekuwa waki-overtake bila kuchukua tahadhari, na mara nyingi wanafanya hivi kama chombo cha moto kinachokuja mbele yao ni pikipiki.

Unakuta dereva anataka ku-overtake na ukamuashia taa kumzuia au ukapiga honi, yeye hajali hilo anaendelea kukuletea gari, sasa mimi dereva wa pikipiki nipite wapi?

Madereva wanaoongoza ku-overtake bila tahadhari ni wale wa coastal za kutoka Mbeya kwenda Tunduma, madereva wa shuttle za Airport ya Songwe, madereva wa mabasi makubwa ya kampuni ya ABC, Shabiby, New Force, Golden Deer, na Abood, na madereva wa malori ya mafuta.

Madereva hawa wamekuwa chanzo cha ajali nyingi zinazotokea barabarani, vyombo vya usalama barabarani watimize wajibu wao ipasavyo kuwachukulia sheria stahiki madereva wa namna hii.

Pia madereva husika waache kutudharau sisi madereva pikipiki kwa sababu na sisi pia tuna haki kikatiba ya kutumia miundombinu ya barabara bila kusumbuliwa na madereva wengine.
 
Nafikiri hujawaona madereva Wenye dharau WA Dodoma chamwino Na V-eitiii zao , Hao WA mbeya -tunduma cha mtoto
 
Nafikiri hujawaona madereva Wenye dharau WA Dodoma chamwino Na V-eitiii zao , Hao WA mbeya -tunduma cha mtoto
Ninakubaliana na wewe mkuu, angekaa na hata wiki tu dodoma angeona jinsi madereva wa serikali na magari yanayobeba viongozi dodoma yanavyofanya vurugu hasa barabara kipande cha chamwino hadi mjini kati.
 
Pole sana, ila nawakumbusha tu waendesha Pikipiki......
1. Ukiwa unaendesha pikipiki BARABARA KUU, hakikisha unatembelea upande wa kushoto kabisa mwa barabara kule kwenye mstari wa njano; hii ni kwa sababu magari yanakimbia sana (yakupite kwa urahisi) hapo ndio utakuwa salama zaidi na hata ikitokea changamoto kama hiyo, unakwepa kwa urahisi.
2. Ukiona gari linakuja upande wako; mpige flashi x 2 na kama ni usiku washa na indiketa ili akuone huku ukibana kushoto ili akupite salama au akusubiri upite. Honi mara nyingine haisikiki hasa kwa hizi saloon car wanazojifungia wakipata kiyoyozi
3. Acha kabisa kuendesha pikipiki KATIKATI YA BARABARA KUU, labda kama umechoka kuishi. Kumbuka, baadhi ya magari yana kimbia pengine mara mbili ya hiyo pikipiki yako.
4. Mwisho; ACHA KABISA KUWA MBISHI UKIWA BARABARANI KWA KUJIAMINI KUWA UPO SAHIHI, ANGALIA USALAMA WAKO KWANZA!!!
 
Hawa madereva wenye upumbavu hu sio kwa bodaboda tu. Hata magari,unakuta mtu ana IST anaovateki na wewe unakuja wala hajali mpaka umpishe. Hawa ndio huwa wanagongwa na malori njia za mikoani maana wanaenda na huu upumbavu wao.
 
Back
Top Bottom