Bado huamini katika uchawi na ushirikina? Waulize madereva

Bado huamini katika uchawi na ushirikina? Waulize madereva

Natamani mtu aniloge kwa muda flani af aniachie ili nijue inakuaje.....

Maana mengi yanabaki stori tu, fulani aliona hiki, yule ilikua hivi.... sielewagi ndo maana haya makitu mi ata siyakubali kama yapo.
Chagua nikuloge kwa bluetooth au WiFi?
 
Mada iliyopita tumezungumzia kuhusu uchawi na ushirikina kwenye mahakama zetu... Hapa tunaangalia eneo lingine muhimu BARABARA ZETU

Avae, ukimaliza hii naomba uchambue na ya biashara, ningependa kujua zaidi habari za 'chuma ulete', 'misukule', 'ku-vina' n.k.
 
Mshana Jr umenikumbusha mwaka 2003, niko zangu natoka Mwanza kwenda wilayani nilikokuwa nafanyia kazi. Kufika Mhunze kabla sijavuka daraja katikati ya barabara nikakuta sahani ya kioo imewekwa juu ya vikombe viwili na vyenyewe vya kioo (kama zile bilauri za kioo) pembeni yake kuna kikombe na kibakuli (vyote vya kioo). Uzuri niliviona bado nikiwa mbali nikapunguza mwendo nikapita zangu pembeni! Huu mchezo nikagundua nilifanyiwa na Mzee mmoja wa Tanga ndo tulikuwa kwenye mchakato wa kumtemesha mzigo (maana iliagizwa maafisa tuendeshe wenyewe ili kubana matumizi) sasa akawa anataka kutuwahi kabla hatujamtumbua jipu! Mauzauza barabarani yapo ingawa ajali nyingi na madereva wanachangia (sasa fikria kwenye muktadha huo kama ningekuwa mafuta si nilikuwa naanguka Mimi?)
 
10366277_554986098020195_275535888793539630_n.jpg


road devils/ blood sucker finders!
kiumbe huyu anauwezo WA kunywa damu za binadamu Lita 500 KWA dakika 10 tu baada ya ajali./ binadamu mmoja huwa na takribani Lita 9 pekee!/ calculate!
 
Yes tatizo hilo ninalo sana na haswa pale unapokuja na hoja za uongo na za kitoto...

Na kutuwekea picha za uongo za kutisha ili tuamini kwamba ni ukweli, hapo umefeli mkuu

Ni sawa na kuamin mermaid( nguva) ni mwanamke mzuri...hahahaha
Achana na kuchekacheka na kusema ni hoja za kitoto na picha za uongo nimekuomba uthibitishe usikimbie hoja
 
kiumbe huyu anauwezo WA kunywa damu za binadamu Lita 500 KWA dakika 10 tu baada ya ajali./ binadamu mmoja huwa na takribani Lita 9 pekee!/ calculate!
Huweza kujibadili ktk maumbo 33,
ana nguvu za kulaza USINGIZI MZITO.anapokuwa na kiu Kali.
 
miaka kadhaa iliyopita nilikua nasafiri na mzee wangu kwenda singida kutokea Arusha kabla barabara haijatengenezwa,
sasa safari ilikua ya usiku kutokana na kuchelewa kuondoka Arusha,
sasa wakati tunakimbilia Dareda ghafla nikaona baiskeli inaongoza njia, nikamwambia mzee utagonga, akasema bora kugonga kuliko tufe,
yaani alipita moja kwa moja na hakuna baiskeli iliyodondoka,
na tulisimama kuangalia kama ilidondokea pembeni ila hatukuona chochote,
nikamuuliza kama ule ni uchawi akaniambia yale mambo ameshayazoea na huwa hakwepi wala kusimama.
 
SEEING IS BELIEVING!
Kama sitaona kwa macho yangu kitendo cha kichawi, SITAAMINI UCHAWI KAMWE. Ila naheshimu imani za watu, wanaoamini uchawi upo na waamini!
Cha kushangaza kila mtu anayeamini uchawi nikimuuliza umewahi kuona kwa macho yako anadai hapana, siongelei kuona kibuyu kimefunikwa ardhini, naongelea vitu kama 'mtu anapaa na ungo, mbuzi anaongea', uchawi kwangu ni kama a traditional psychology, unacheza tu na akili za watu! Ni suala la imani.
wewe nakuonea sana huruma, ngoja siku yakikukuta ndo utatia akili, mimi nimepoteza mtoto kwa hujuma za wachawi, siwezi kueleza mkasa wote ulivyokuwa maana nitajikuta naanza msiba upya, ila hapa nilipo nimeamua ni bora nikae karibu na Mungu,Kwa maana ya kufanya ibada,
Nataka ujue kuwa shetani yupo na wachawi wapo, wachawi ndo wakala wakuu wa shetani,
Usitake kujifanya unajua wakati ubongo wako ni sufuri tupu, uwe unatuliza akili ili ufundishwe usiyoyajua,
Shetani alikuwa malaika wa sifa mbinguni na jina lake aliitwa Lucifer, Mungu alimpenda sana Lucifer maana Mungu hupenda kuimbiwa nyimbo za sifa na kuabudiwa.
Baadae shetani akajaa kiburi na kujiona kuwa ana uwezo kama Mungu ndipo alipopanga mapinduzi ili yeye ndo awe Mungu, kwa kuwa Mungu ana uwezo mkubwa sana aliweza kuyajua mawazo ya shetani ndipo akaghadhabika na kumtupa shetani duniani pamoja na theluthi tatu ya malaika waasi (waliokuwa upande wa shetani )malaika hao nao wakalaaniwa pamoja na shetani na kugeuka kuwa mapepo au majin,
Unapotaka kila jambo ulione ndipo uamini basi wewe utakuwa juha sana,
huwezi kumuona mchawi achilia mbali shetani na Mungu, mchawi hufanya mambo yake ktk ulimwengu wa roho sasa utamwonaje?
Na wala Mungu huwezi kumuona maana ni roho ila yupo, ikitokea kwa mfano ukamuona Mungu kwa macho ya kawaida, mambo mawili ya kutisha yanaweza kutokea kwa tofauti, unaweza ukafa papo hapo au ukaishi milele, kwanini? Ni Kwa sababu Mungu ni mtakatifu mno, hapa duniani hakunaga binadamu mtakatifu, wanapeana utakatifu kimazoea tu wakidhani Mungu ana silika ya mwanadamu la hasha!
Nilikuwa na rafiki yangu aliyekuwa mjuaji kama wewe, akafiwa na mwanae ktk mazingira tata, akashauriwa aende Kwa mganga wa jadi, alipoenda akamuona bibi mmoja jirani yake kwenye tv ya kichawi kuwa ndo alimuua mwanae (waganga wanaujua uchawi )akaomba apewe dawa ya kuona wachawi, bahati mbaya akapewa bila kinga yoyote,
Aliipaka dawa machoni ili awaone wachawi usiku wa manane, kando ya nyumba yake palikuwa na mti mkubwa wa mwembe.
Siku ya tukio saa 7 usiku aliwaona wachawi na akapiga kelele kwa hofu maana baadhi yao aliweza kuwatambua, wachawi wale walikuwa wakifanya kikao kwenye ule mwembe.
Na alipopiga kelele walimwona, kesho yake alipotoka kazini tu akaugua mshipa wa ngiri wakati walipompeleka hosp hawakuona ugonjwa, siku tatu baadae akafariki.
Siku ya pili baada ya kumzika akaanza kumtokea mkewe, ikabadilika mwanamke akimbie nyumba, baada ya wk hivi akaanza kunitokea na mimi usiku wa manane, alikuwa akija na kugonga dirishani akitaka nimpatie shuka, siwezi kueleza yote, ila baadae alitoweka jumla hadi Leo.
Wachawi wapo na ni watu hatari sana, wana vyama vyao, mwenyekiti wao, serikali yao na kila kitu, na wapo dunia nzima hadi marekani,
Unaweza kumwona mtu ana maisha magumu na amechakaa kumbe ni mchawi hatari na kila mwezi anaenda Washington marekani kwenye kikao na wachawi wenzake, nina mengi ya kukueleza ila ngoja niishie hapa kwanza, ila maadam upo duniani ipo Siku yatakukuta na utoto ukutoke.
 
Babu yangu ni Dereva kampuni ya TBL,haya mambo ni sehemu ya changamoto anazokumbana nazo njiani,anasema kanuni yake huwa hapishi chochote, Kuna siku aliona kichaa ghafla mbele yake,akamgonga,akapunguza mwendo kucheki nyuma eti anaona kagonga kimnyama cha ajabu. Kuna siku moja huko Dareda alikuwa analikaribia darajaakapunguza mwendo,mara akaona madaraja matatu ghafla,ilikuwa ngumu sana ikabidi apaki apige kwanza dua barabara ikawa clear akaendelea na safari. Hizi mambo usiombe zikukute.
ni kweli maeneo fulani kabla haujafika Dareda siyo salama.
 
Achana na kuchekacheka na kusema ni hoja za kitoto na picha za uongo nimekuomba uthibitishe usikimbie hoja

Haina haja ya kudhibitisha coz ni picha za uongo..

Hizo nyingi ni habari za udaku mkuu labda wewe ndio udhibitishe kwa kutoa source ambayo inaaminika sana sio hivyo viblog vinavyotaka umaarufu
 
Naamini uchawi upo ingawa sijawahi kulogwa au kukutana na kitu cha kichawi ila nakumbuka siku moja usiku hukooo Ifakara kwenye safu ya milima Udzungwa nilikuwa natembea usiku nikaona kitu kirefuuu ila sikujua ni nini kwa akili za haraka haraka za kiswahili nikahisi ni Jini hapa ndipo wengu wetu hukosea. Ukiona jambo unaleta moja kwa moja kwenye uswahili unaweza kuta mda mwingine ni mti tu ila sababu akili yako inawaza kwamba upo porini na ni usiku na kuna historia za kutisha eneo hilo basi unachukilia ndio kitu chenyewe sababu mda mwingine natembea usiku nahisi kuna mtu kasimama mbele nasita kwenda baada ya mda naenda nakuta na kumbe ni mti tu.
 
Kipindi nipo mdogo nilikua naona mauzauza kama kuna watu nawaona wamesimama ila wenzangu hawaoni baada ya kuhangaika mda mrefu basi Mama angu au dada zangu unipeleka nikawaonyeshe hao watu wenzangu wanaona miti mimi naona watu basi tukifika pale kweli ni miti kwa hiyo mda mwingine mauzauza ni mind yakk tu maana mara nyingi mimi nakutana na vitu ambavyo nikifikiria upya naona kumbe ni woga tu hata iyo siku niliyokutana na kitu kirefu nilikimbia sana bila kusimama mpaka nikafika ila nikaja kufikiria kwa nini sikujipa mda kukiangalia iko kitu kiundani nikathibitisha kama ni Shetani au vipi ila mimi nilivyoona tu nikafunguka moja kwa moja.
 
Achana na kuchekacheka na kusema ni hoja za kitoto na picha za uongo nimekuomba uthibitishe usikimbie hoja
Unanikera sana mkuu kupoteza muda wako kubishana na watu wajinga wasiotaka kujifunza au pengine ni wachawi hatari sana wanajifanya hawajui kitu, hebu waruke hao vilaza tupanuane mawazo sisi wenyewe tunaoamini ktk ulimwengu wa roho.
 
Unanikera sana mkuu kupoteza muda wako kubishana na watu wajinga wasiotaka kujifunza au pengine ni wachawi hatari sana wanajifanya hawajui kitu, hebu waruke hao vilaza tupanuane mawazo sisi wenyewe tunaoamini ktk ulimwengu wa roho.
Aisee nimeshaachana naye nimegundua tatizo liko wapi ujuaji mwingi usio na base
 
Unanikera sana mkuu kupoteza muda wako kubishana na watu wajinga wasiotaka kujifunza au pengine ni wachawi hatari sana wanajifanya hawajui kitu, hebu waruke hao vilaza tupanuane mawazo sisi wenyewe tunaoamini ktk ulimwengu wa roho.

Ficha ujinga wako...Hii ni open forum ambayo ni kawaida kupata mawazo tofauti na Yale unayoyajua au unayofikilia..
Sasa unapanuaje mawazo kwa akili zilezile zinazoamini usichokijua

Kama halikuwa hataki kupingwa basi hakutakiwa kuwasilisha mbele za magreat thinker hiyo habari yake
 
Ficha ujinga wako...Hii ni open forum ambayo ni kawaida kupata mawazo tofauti na Yale unayoyajua au unayofikilia..
Sasa unapanuaje mawazo kwa akili zilezile zinazoamini usichokijua

Kama halikuwa hataki kupingwa basi hakutakiwa kuwasilisha mbele za magreat thinker hiyo habari yake

Mwana! great thinker are not mere words, ukipinga kwa hoja zinazojenga ndio utahesabiwa kuwa great thinker sio kwa hoja zilizokosa mashiko... Ni rahisi sana kuongelea kuhusu GTs bila kujua maana yake halisi
 
Last edited:
Back
Top Bottom