Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Ulitakiwa utumie akili vizuri kwanza jinsi ya kumface na uwaze kuwa waliachana na mama yako kwa situation gani pia familia yake mpya inajua kama ana mtoto kama ameficha huko akijua mke wake kupitia wewe nini kitatokea kwa familia yake na kwako cha kufanya ulitakiwa uende ofisin kwake au sehemu nje ya nyumban kwake
 
Kufupisha tena bila kuficha baba ni mpumbavu sasa yaani anamtosa mtoto wake kisa kuogopa mke. Sisi wanaume wa Afrika huwa tunaoa sio kuolewa.

Huenda kuna sababu nyingine iliyo mfanya huyo mzee amkatae mtoto ambayo ni kubwa kuliko ya kumuogopa mke wa sasa.

Ninampa pole tu kijana kwa yalio mtokea tena wakati wa kipindi anahitaji msaada.
Mi naona ni Ile approach iliyotumika ndio haikuwa sahihi. Tunaotoa ushauri hapa wengi ni wazazi na linapokuja swala la mtoto gafra kuibuka tu nyumbani na kudai eti mi mwanao mbele ya mke wako, hapo lazima upate ukakasi kwanza tuongee ukweli.
Jamaa bado ana nafasi ya kuonana na babaake Ila kwasasa aendelee kutengeneza maisha yake, ipo siku tu watamtambua hata kama ni kwenye mazishi ya mzee wake.
 
Sasa kama mzazi amesema hamkumbuki na kumpeleka kabisa stendi ili asimuone tena unataka mlokole amshauri mleta mada akamloge huyo mzee ili amkubali?
Wewe ndio umewaza hivo. Angalia comment nzima ya mtoa mada halfu urudi kuandika upya.

Maana yake iwapo baba sio katili basi unaruhusiwa kutomtegemea Mungu?
 
Jitu limekukataa bado unaliwaza, wengine mna mioyo kweli, baki na mama na wajomba hao ni wa muhimu kuliko huyo Fala, tafuta pesa akutafute na wewe umwambie humjui.
Yaan mm hata nione uzi namtafuta baba sijui sijawah muona namskia yupo mara mama alinitelekeza hua napatwa vipele ..sikutafuti ng'o..ila wana mioyo...
 
Hii kitu ni noma sana, unakuta sasa bado hata wewe utakuja teleza ukapata mtoto wa ujanani na ukamsahau kabisa, huwa hatujifunza unakuta na wewe mdau unakua una watoto nje ya ndoa na wala hujali wale watoto kabisa, mimi sitakuja kufanya hivi peke yangu siwezi namuomba Mungu watoto wangu wawe wa ndoa tu nisijichanganye ili niwape malezi bora wanangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakuombea uwe baba bora, na hata ikitokea umeteleza tafadhali wajibika kwa makosa yako.
 
Huo ni udhaifu wa Baba . UtamuogopaJe mkeo kiasi hicho mpaka ushindwe kuzungumza na nwanao ?! Ndiyo maana nayakubali makabila ya kwetu Tarime . Mwanamke hawezi kuleta fujo kwenye mambo haya.

Huyo mbaba ni weak
Hata mimi sijui wanaume wengine wameumbwaje. Yaani mimi ni mkatae mwanangu wa damu yangu kumuogopa mtu ambe sina undugu wowote wa damu, hapana haiwezekani, urafiki wa mume na mke unaweza isha ila sio undugu wa baba na mtoto.
Huenda kuna sababu nyingine ilimpelekea kufanya hivyo ila bado atakuwa na mapungufu mengi huyo mzee, nazungumzia nikiwa na uchungu kama mzazi.
 
Kaka nakuambia wala isikutishe sana! Mm baba alichana na mama! Mwaka 2001 nikiwa darsa la kwanza! Aliinihitaj na nikafika alipokuwepo! Amini nakuambia alininunulia soda akaniambia anapeleka abiria! Hakurud had aliposikia nipo udsm! Mwaka 2017 nikiwa mwaka3 udsm akanipigia akisema mm ni baba yayko! Niliishia kwambia sawa! Kwa hyo! Akasema nataka kukuona! Nikawambia nipo pale uliponiacha! 2018 nikiwa arusha akanifuata! Akaniambia hujaoa! Nikamwambia kwa kiwanja kip ulichoacha leo Mungu ameniinua kidgo naanza kumjengea mama nimemtafutia kiwanja kwa kuwa alirud kwao sasa namjengea nyumba! Mungu ni mwema usikate tamaa mzee amebak na picha yangu kwa profile picha ya wasap na phone displays! Wala sibabaiki! Msimlaum Diamond
 
Hukutumia akili. Mama yako naye hakukushauri vyema.

Jambo kama hilo ni zito huwezi toka tu ukafika kwenye familia ya mtu kuwa mm mwanao sasa nipokee.

Utlist mama yako angetengeneza njia hata kutumia wazee watu wazima kwenda kwa mzee mwenzao kumweleza yeye ndo angeona hilo suala alihandle vipi. Na ungejua ni kwann hakujishughulisha na ww.

Ikiwa ni mzee mpumbavu ndipo angekukataa. Japo mpaka ss kama hajakutafuta nje namuona mjinga kama kweli ni baba yako.
 
Hebu pambana mkuu, hasira zote zielekeze kwenye kufanya kazi ujiimarishe kiuchumi. Ifanye akili yako iwaze kuwa huna baba.
Pambana uwasaidie mama yako na wadogo zako(kama wapo).
 

Vizazi vizalia na masalia. Je, kuna asili iliyopotea?

Sent using Jamii Forums mobile app
kabisa,asili ilishapotea na kuirudisha ni kazi,na pia ku maintain iliyopo pia ni kazi. everything upside down.
 
Story yako imenihuzunisha sasa bila aibu anakuweka profile ili iweje wakati hakuwa na time na wewe. Endelea na maisha yako Mungu hatakuacha
 
Back
Top Bottom