Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Baba yangu aliniambia hanikumbuki, niliumia sana

Kama baba yako anaweza kukuruka mahali popote isipokuwa kwa maslahi au usalama wako huyo sio baba yako wala asipoteze muda wake
Alikuruka kulinda ndoa yake, ungekuwa umemfuata kazini mchana, angekupokea ila asingekupeleka kwa mkewe, mngemalizana kiume na nduguzo ungewajua, lakini bado una nafasi. Mfuate tena ila pitia kwa rafiki yake wa karibu, usiende direct.
 
Hata mimi yule mwanamke anayekatalia mtoto wangu siku akiniletea namkataa hata awe nani

Watoto wakati mwingine msiwalaumu wazazi wanaowakataa mjikite kujua tatizo lilianzia wapi
 
Sina hakika kwasasa una umri gani but kwakua na wewe ni mtoto wa kiume utakuja yajua haya mambo baadae; laiti ungemfata mzee kazini kwake hili wala lisingetokea, hujui huyo mzee alifanywa nini na mkewe huko chumbani, huenda hadi kadi ya bank alinyang'anywa. Mengine ni siri ya kambi tu, otherwise Mungu atakusaidia jipe moyo
Ila wanawake bwana[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] mimi niwe na mtoto nje halafu mwanamke aniletee za kuleta namtandika vibao na talaka juu
 
Ila shukuru sana Mama wakambo alikupokea vizuri ilo linatosha pambana uwe diamond wa baadae akishatumbuliwa huko atakutafuta tu usijali kaza moyo
 
Labda maza alishamwambia babako we siyo mtoto wake maana wamama wengi pia huwa wanazingua sana ila kwakua mwanaume siku zote ni mbebeshwa lawama mwishoni bila kujulikana chanzo lazma jamii yote imuone mbaya tu.
kweli kabisa
 
Hakuna mwenye nafuu hata mmoja binadamu wote ni wakatili maana mi mwenyewe niliachwa hospitali.

Sijawahi kumjua baba wala Mama.

Nikisikia mtu anasema mama anauchungu na mwana natamani nimtukane tusi la nguoni.
So alikulea nani?? unaujua ule wimbo wa nani kama mama[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hapa shida ni huyu jamaa aliyekupeleka direct nyumbani, ilitakiwa kama muelewa angefanya utaratibu wa kuwasiliana na babako kwanza kabla hajakupeleka home, ukitilia maanani ulimwambia hujawahi kutana na babako, naek aliona kabisa wewe ni mtoto wa huyo jamaa yake. Kukupeleka nyumbani pale alitaka kuwe na mtafaruku tu.
Pole sana, mimi nadhani wewe mfuate tena huyu mzee kama yupo ila nenda kwa staha.
 
Pole kwa maswahibu.

Hapo wenye makosa ni wote kasoro wewe. Mama, baba na hata msamaria mwema.

1. Mama yako alipaswa kukueleza fika kuwa wewe ni mtoto wa nje kwa hiyo tendo uchukue tahadhari. Yeye akakuacha umeenda kichwa kichwa na umri wako mdogo!!! Masikini ukalala ndani kwa amani bila kujua kitakachotokea.

2. Msamaria mwema alitakiwa kumtafuta baba yako nje ya nyumbani kwake sio kukupeleka direct kwake. Imagine hapo ulipo unarudi home unamkuta mtoto uliyemficha miaka 14 yupo ndani.... Si lazima kuchimbike?

3. Baba yako kwa kutokutafuta baada ya kukuondoa pale. Hilo ni kosa kubwa. Ina maana alikupotezea mazima bila kujali wewe ni mwanae.

Ukipata wakati nenda umtafute umsalimie tu na kumjulia hali. Tuwe kama waisrael hakuna damu au nafsi itakayoachwa nyuma yenye asili ya israel.
 
Baadae lizee linajirudi baada ya mtoto kufanikiwa na yeye kufulia. Mijitu inajitokeza kumshauri kijana amsamehe baba yake Kama vile ni kitu rahisi..manina
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] ingekuwa wewe ungesamehe?
 
Ungeishia kwa hayo maneno wawili ya kwanza (Pole mkuu) ingetosha sana kumfariji. Hayo yaliyofuata hayana msingi wowote na wala hayamsaidii katika uzi huu. Umeangalia mno upande mmoja. Mara nyingine chanzo kinaweza kuwa wabeba mimba; usilifumbie macho hilo. Nina ushahidi juu ya hilo.
Tupe ushahidi huo
 
Sioni sababu yoyote inayoweza kumfanya au kumhalalishia huyu baba kumfanyia mwanae huu ukatili. Ni roho mbaya tuu na kukosa utu

Mungu hatakuacha Ze_big_chill 🙏
 
Back
Top Bottom