Hii issue ya kitimoto naona kama mnaibeba tofauti au kimakosa. Kwa nielewavyo Mimi, japo waislam kitimoto ni Haram kwenu, lakin under certain circumstances mnaweza kula. If that's the case, sio kama yakufaa ujisikie vibaya baba ako mdogo kukwambia umpokelee (as long as inakuwa imefungwa vizuri, na hajakwambia ule).
Lakini pia nishawahi kumuuliza Sheikh mmoja kuhusu waislam kula kwenye mahotel ya Kitalii au yanayotoa huduma ya kitimoto, akaniambia vyombo vikishatumika huwa vinaoshwa, so sio tatizo wao kupata huduma sehemu. If that's the case, sioni ajabu baba yako mdogo kutumia vyombo vyenu maana huwa vinaoshwa.
Nina uncle alioa mwanamke wa Kiislam, kila mmoja aliendelea kubaki na dini yake. Yule Aunt alikuwa hatumii kitimoto, ila mara kadhaa nishawahi kushuhudia akimuandalia uncle.
Sijajua kama nitakuwa wrong or what, ila huwa nahisi kuna baadhi ya mapokeo kwenye hizi dini zetu hatujayaelewa.