Was salaam.
Ni hivi upande wa baba wapo mseto lkn %95 ni wakristo, %5 ndiyo siye,
Baba mdogo kaja nyumbani kutusalimia na ana wiki sasa,
Shida ba mdogo anapenda kula kitimoto balaa,
Yaani chai yake ni kitimoto na pepsi,
Shida anakuja nacho ndani, kama leo kamtuma boda amletee na muda boda kaja ba mdogo anaoga na akaniambia nikampokelee
Na kumuambia asilete ndani nitaanzaje??
Hawezi kuona tunamnyanyapaa??
Au hatumtaki??
Je anafanya kusudi?? maana anaelewa kuwa hatutumii,
Naombeni ushauri nitumie njia gani kumfikishia kuwa hatupendezewi na hii tabia?
NB. Mama hajui maana si mtu wa nyumbani.