Baba mdogo anakula kitimoto hadharani

Baba mdogo anakula kitimoto hadharani

Was salaam.

Ni hivi upande wa baba wapo mseto lkn %95 ni wakristo, %5 ndiyo siye,

Baba mdogo kaja nyumbani kutusalimia na ana wiki sasa,

Shida ba mdogo anapenda kula kitimoto balaa,

Yaani chai yake ni kitimoto na pepsi,

Shida anakuja nacho ndani, kama leo kamtuma boda amletee na muda boda kaja ba mdogo anaoga na akaniambia nikampokelee

Na kumuambia asilete ndani nitaanzaje??

Hawezi kuona tunamnyanyapaa??

Au hatumtaki??

Je anafanya kusudi?? maana anaelewa kuwa hatutumii,

Naombeni ushauri nitumie njia gani kumfikishia kuwa hatupendezewi na hii tabia?

NB. Mama hajui maana si mtu wa nyumbani.
Hongera kwa kuwa na hekima na heshima kwa mzazi wako.Muhimu hapa duniani ni hili mengine haya tumeletewa tu Kama hustarabu Ila yasikuangaishe sana,kwangu Imani ni Imani na binadamu mwenzangu ni muhimu zaidi na Wala Imani haiwezi kufanya nimuone tofauti Cha msingi ni utu tu.Mshukuru mungu walau unapata mzazi wa kukutembelea hiki ni kitendawili kwa familia nyingi za kiafrika pale ambapo unaondokewa na baba au mama na bado ndugu wakakujali Cha msingi ongea na baba umwambie kiheshima juu ya Imani yako na mshauriane tu kikawaida.Kwa vijana wa sasa unaonekana una hekima sana Imani isikutenge na ndugu tumeikuta tutaiacha.siku njema
 
Ni kweli,mtu kafunga safari ndefu kaja kutusalimia tu,
 
Back
Top Bottom