Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,218
- 219,394
Akizungumza kwenye kumbukumbu ya miaka 3 tangu kufariki kwa Maalim Seif, ambaye ni Gwiji la Siasa za Zanzibar, Baba Askofu Mwamakula amesema kwamba kwenye utawala wa Mkapa hakukuwahi kuwa kesi wala tatizo kwa viongozi wa kidini kutoa waraka wa kukosoa matendo maovu ya serikali, amedai hana kumbukumbu kuhusu enzi za Mwl. Nyerere, bali aliheshimu sana viongozi wa dini.
Askofu Emmaus Mwamakula amesema kwamba; si kwamba kwenye tawala hizo hakukuwa na matamko au waraka wa viongozi wa dini, bali viongozi wa wakati ule walitumia matamko hayo na kuyafanyia kazi badala ya kuwakamata, kuwavua Uraia ama hata kuwafunga viongozi wa dini.
Toa maoni yako.