Veronica France Amuomba Msamaha Baba Askofu Mwamakula na Viongozi wa CHADEMA, Naye Akubali Msamaha Wake

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,288
9,923
Kwenye Ukurasa wake wa Face Book wa Veronica France amepost ujumbe wa Kuomba Msamaha kwa Maneno ya kuudhi aliwahi kuyatamaka kwa Askofu na Viongozi wa Chadema Mbowe na Lusu

Akionyesha kuwa anajutia yote aliyoyafanya Veronica aliandika hivi

"Baba askofu, nachukua hatua hii muhimu katika maisha yangu kukuomba msamaha katika maeneo yote niliyowahi kukukosea kwa makusudi au kwa bahati mbaya🙏,najua tunatofautiana ktk itikadi na mitazamo,lakn nilikuwa nakukosoa katika namna isiyo ya kiungwana na kistaarabu ya matusi,kejeli,nilipungukiwa hekima mbele za Mungu na mbele yako,lakin sasa najutia na nanyenyekea sana mbele za Mungu na mbele zako,naomba radhi sana naomba unisamehe kama kijana au mdogo wako vyovyote vile.

Nilipotoa Lugha ya matusi, kejeli na kashfa, naomba unisamehe,alfajiri ya Leo nimejitafakari sana na nimechukua maamuzi haya bila kusongwa wala kishauriana na mtu, bali mimi na moyo wangu. Sometimes sitakiwi kufanya siasa za chuki na uadui, hata unapokosea sistahili, naomba sana unisamehe, nilitamani kuandika kwenye wall lakn nikaona usipo nitamkia msamaha hapa haita saidia.

Nelson Mandela aliwahi kusema "forgiveness is an attribute of strong people" and only warrior can ask for a forgiveness, hivyo, nifikishie msamaha wangu pia kwa Tundu Lissu, nilipomkejeli kwa ulemavu wake na situation aliyopitia,Naomba sana niombee radhi sana,anisamehe kama mdogo wake, nifikishie msamaha kwa Freeman Mbowe, tunajenga nyumba moja,na bado nasafari ndefu ya kujifunza🙏🙏🙏nitakushkuru sana kama utaguswa na kunisamehe hata usiponijibu au kuandika lakini rohon kwako tu ukinisamehe nitakushkuru sana🙏🙏🙏🙏asante sana na Mungu wangu wa Mbinguni akubariki.

Emmaus Bandekile Mwamakula"

Kufuatia hatua hiyo Baba Askofu Mwamakula naye alipost Kwenye Ukurasa wake wa Faceboo kuukubali msamaha wake.

Baba Askofu Alisema Hivi
"MAJIBU YA ASKOFU KWA VERONICA FRANCE!

Mpendwa Veronica France! Naona ulinipigia. Wakati huo nilikuwa kwenye phone conference. Lakini pia huwa situmii call hii ya messenger. Nadhani utakuwa unaelewa ni kwa nini situmii 'calls za messengers'!

Wito wangu wa Uaskofu una majukumu mengi sana ikiwemo kuwaombea watu. Tunapoomba tunaamini kuwa Mungu anasikia na pia hujibu maombi kwa wakati wake.

Sisi kama wanadamu tunatakiwa kuchukuliana na kusameheana pale tunapokoseana. Ni vizuri watu wakaelewa kuwa yote yaliyotendwa dhidi yangu binafsi, ninayahesabu kama gharama na sadaka yangu katika wito huu. Na hakuna wito usiokuwa na gharama.

Mungu aliwatumia watu walioniumiza ili kusudi niimarishwe zaidi. Ni kwa sababu hiyo, ingawa kuna wakati niliumia sana, lakini sikuwahi hata kidogo kuwachukia watu walioniumiza. Wengi niliwaombea na wachache sikushughulika nao.

Ukielewa jinsi upana wa vita yangu ilivyokuwa, huwezi kusononeka, bali utamtukuza Mungu pamoja nami kwa kunipigania. Hakuna vita isiyokuwa na majeruhi au hata vifo. Katika vita yangu, Wainjilisti 2, Wachungaji 7 na Askofu 1 walitukimbia. Tulipoteza sharika (parishes) 6 na tulidhurumiwa haki ya kupata viwanja vya kujenga Kanisa maeneo ya Mbweni na jengo 1 liliporwa kwa nguvu katika eneo ambalo kwa sasa sitaji. Vita nyingine dhidi yetu iliendeshwa kupitia kwa baadhi ya maofisa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Matusi ya mitandaoni dhidi ya Askofu yalikuwa yanapelekwa kwa waumini kwa lengo la kutaka kuwafedhehesha ili walihame Kanisa. Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha Kanisa linavurugwa ili Askofu asiwe na Kanisa kabisa. Baadhi ya watu waliwatumia baadhi ya maaskofu wa Kanisa moja kubwa nchini kuvuruga mahusiano yetu na partners wetu nje ya nchi.

Wewe hukuelewa upana wa vita hii dhidi yangu na laiti ungelielewa, basi leo ungekuwa katika kustaajabia ukuu wa Mungu kwetu. Katika vita yote hiyo Askofu aliendelea kuishi na Kanisa bado lipo ingawa nguvu kubwa ilitumika kupitia kwa baadhi ya watu waliokuwa katika nafasi za mamlaka ambao walikuwa wanatumiwa kutaka kulifuta Kanisa letu kutoka katika uso wa jua.

Mimi binafsi sioni kama nina hadhi ye yote ya kuombwa msamaha na wewe, lakini kwa kuwa nafsi yako imewiwa kutaka kufanya hivyo, basi ni sharti nikutangazie msamaha kwa dhati ili nafsi yako ipate amani. Kutangaza msamaha au kutoa ghofila ni moja ya majukumu yetu ya kila Jumapili. Kama Askofu asipotangazia watu msamaha atakuwa ameikana imani.

Kuhusu Mhe. Tundu Lissu na Mhe. Freeman Mbowe, naweza kuwaambia lakini kikubwa ni jamii kuelewa kwani mara nyingi wafuasi ndio huumia viongozi wao wanapofedheheshwa.

Kama wewe ukiweka public hata kwa sentensi chache katika ukurasa wako kuhusu kuomba msamaha, nami nitaueleza umma kuwa kweli ulinitafuta kwa jambo hilo na nimekusamehe. Vinginevyo, nikiandika bila ya wewe kufanya hivyo, watu wengi watajua kuwa ni drama tu.

Napenda nikuhakikishie kuwa hili ulilolifanya hapa litakufungulia wewe milango ya baraka na kukupatia kibari kwa wakuu wa nchi. Lakini pia usifadhaike utakapoona baadhi ya uliokuwa nao wakianza kukujeli na kukufedhehesha. Wewe ni shujaa kwa kuwa umefanya kitendo ambacho wengi wetu tunashindwa! Kuomba msamaha hadharani tena mtandaoni ni ujasiri na unyenyekevu wa hali ya juu.

Tunaamini kuwa huu ni ushuhuda kwetu sisi, Kanisa letu na hata nchi yetu. Wale waumini na Wachungaji wetu ambao walitukimbia kwa kuambiwa uwongo au kutishwa watapata kitu cha kujifunza na wale waliobaki pamoja na sisi wataimarisha zaidi kiimani.

Ushuhuda wako ni uponyaji kwetu, uponyaji kwa Kanisa letu na uponyaji kwa taifa letu. Ni ushuhuda uliokuja katika wakati muafaka kwani sisi Askofu tunaendesha Kampeni ya kuundwa Tume ya Ukweli na Maridhiano ili watu wasameheana. Wewe umeonyesha njia.

Ninatumia nafasi hii kuwasihi Mheshimiwa Lissu, Mheshimiwa Mbowe na Watanzania wote ambao walikwazwa na wewe kwa namna moja ama nyingine kukusamehe kwa kuwa hata sisi Askofu tumekutangazia msamaha.

Ninakutakia amani ya Mungu ipitayo ufahamu wote. Wafilipi 4:8.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 24 Mei 2023; 01:35 pm"

Aboudquarim Malisa naye amejitokeza
 
Baba, Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula,naungana na Veronica kukuomba Msamaha.

Huku mitandaoni tunaongea sana, na mara zote tunakazia au kukomalia mambo ambayo hatuyajui, Nisamehe kwa hayo.

Pia, nachukua nafasi hii kuomba msamaha kwa wote tulioparuana na kukwazana humu Jf.
Kwa niaba ya Baba Askofu natangaza msamaha kwako lakini usirudie
 
Kwenye Ukurasa wake wa Face Book wa Veronica France amepost ujumbe wa Kuomba Msamaha kwa Maneno ya kuudhi aliwahi kuyatamaka kwa Askofu na Viongozi wa Chadema Mbowe na Lusu

Akionyesha kuwa anajutia yote aliyoyafanya Veronica aliandika hivi

"Baba askofu,nachukua hatua hii muhimu katika maisha yangu kukuomba msamaha katika maeneo yote niliyowahi kukukosea kwa makusudi au kwa bahati mbaya🙏,najua tunatofautiana ktk itikadi na mitazamo,lakn nilikuwa nakukosoa katika namna isiyo ya kiungwana na kistaarabu ya matusi,kejeli,nilipungukiwa hekima mbele za Mungu na mbele yako,lakin sasa najutia na nanyenyekea sana mbele za Mungu na mbele zako,naomba radhi sana naomba unisamehe kama kijana au mdogo wako vyovyote vile...

Nilipotoa Lugha ya matusi,kejeli na kashfa,naomba unisamehe,alfajiri ya Leo nimejitafakari sana na nimechukua maamuzi haya bila kusongwa wala kishauriana na mtu,Bali mimi na moyo wangu.Sometimes sitakiwi kufanya siasa za chuki na uadui,hata unapokosea sistahili,naomba sana unisamehe,nilitaman kuandika kwenye wall lakn nikaona usipo nitamkia msamaha hapa haita saidia...

Nelson Mandela aliwahi kusema "forgiveness is an attribute of strong people" and only warrior can ask for a forgiveness, hivyo,Nifikishie msamaha wangu pia kwa Tundu Lissu,nilipomkejeli kwa ulemavu wake na situation aliyopitia,Naomba sana niombee radhi sana,anisamehe kama mdogo wake,nifikishie msamaha kwa Freeman Mbowe,tunajenga nyumba moja,na bado nasafari ndefu ya kujifunza🙏🙏🙏nitakushkuru sana kama utaguswa na kunisamehe hata usiponijibu au kuandika lakini rohon kwako tu ukinisamehe nitakushkuru sana🙏🙏🙏🙏asante sana na Mungu wangu wa Mbinguni akubariki...

Emmaus Bandekile Mwamakula"

Kufuatia hatua hiyo Baba Askofu Mwamakula naye alipost Kwenye Ukurasa wake wa Faceboo kuukubali msamaha wake.

Baba Askofu Alisema Hivi
"MAJIBU YA ASKOFU KWA VERONICA FRANCE!

Mpendwa Veronica France!
Naona ulinipigia. Wakati huo nilikuwa kwenye phone conference. Lakini pia huwa situmii call hii ya messenger. Nadhani utakuwa unaelewa ni kwa nini situmii 'calls za messengers'!

Wito wangu wa Uaskofu una majukumu mengi sana ikiwemo kuwaombea watu. Tunapoomba tunaamini kuwa Mungu anasikia na pia hujibu maombi kwa wakati wake.

Sisi kama wanadamu tunatakiwa kuchukuliana na kusameheana pale tunapokoseana. Ni vizuri watu wakaelewa kuwa yote yaliyotendwa dhidi yangu binafsi, ninayahesabu kama gharama na sadaka yangu katika wito huu. Na hakuna wito usiokuwa na gharama.

Mungu aliwatumia watu walioniumiza ili kusudi niimarishwe zaidi. Ni kwa sababu hiyo, ingawa kuna wakati niliumia sana, lakini sikuwahi hata kidogo kuwachukia watu walioniumiza. Wengi niliwaombea na wachache sikushughulika nao.

Ukielewa jinsi upana wa vita yangu ilivyokuwa, huwezi kusononeka, bali utamtukuza Mungu pamoja nami kwa kunipigania. Hakuna vita isiyokuwa na majeruhi au hata vifo. Katika vita yangu, Wainjilisti 2, Wachungaji 7 na Askofu 1 walitukimbia. Tulipoteza sharika (parishes) 6 na tulidhurumiwa haki ya kupata viwanja vya kujenga Kanisa maeneo ya Mbweni na jengo 1 liliporwa kwa nguvu katika eneo ambalo kwa sasa sitaji. Vita nyingine dhidi yetu iliendeshwa kupitia kwa baadhi ya maofisa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Matusi ya mitandaoni dhidi ya Askofu yalikuwa yanapelekwa kwa waumini kwa lengo la kutaka kuwafedhehesha ili walihame Kanisa. Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha Kanisa linavurugwa ili Askofu asiwe na Kanisa kabisa. Baadhi ya watu waliwatumia baadhi ya maaskofu wa Kanisa moja kubwa nchini kuvuruga mahusiano yetu na partners wetu nje ya nchi.

Wewe hukuelewa upana wa vita hii dhidi yangu na laiti ungelielewa, basi leo ungekuwa katika kustaajabia ukuu wa Mungu kwetu. Katika vita yote hiyo Askofu aliendelea kuishi na Kanisa bado lipo ingawa nguvu kubwa ilitumika kupitia kwa baadhi ya watu waliokuwa katika nafasi za mamlaka ambao walikuwa wanatumiwa kutaka kulifuta Kanisa letu kutoka katika uso wa jua.

Mimi binafsi sioni kama nina hadhi ye yote ya kuombwa msamaha na wewe, lakini kwa kuwa nafsi yako imewiwa kutaka kufanya hivyo, basi ni sharti nikutangazie msamaha kwa dhati ili nafsi yako ipate amani. Kutangaza msamaha au kutoa ghofila ni moja ya majukumu yetu ya kila Jumapili. Kama Askofu asipotangazia watu msamaha atakuwa ameikana imani.

Kuhusu Mhe. Tundu Lissu na Mhe. Freeman Mbowe, naweza kuwaambia lakini kikubwa ni jamii kuelewa kwani mara nyingi wafuasi ndio huumia viongozi wao wanapofedheheshwa.

Kama wewe ukiweka public hata kwa sentensi chache katika ukurasa wako kuhusu kuomba msamaha, nami nitaueleza umma kuwa kweli ulinitafuta kwa jambo hilo na nimekusamehe. Vinginevyo, nikiandika bila ya wewe kufanya hivyo, watu wengi watajua kuwa ni drama tu.

Napenda nikuhakikishie kuwa hili ulilolifanya hapa litakufungulia wewe milango ya baraka na kukupatia kibari kwa wakuu wa nchi. Lakini pia usifadhaike utakapoona baadhi ya uliokuwa nao wakianza kukujeli na kukufedhehesha. Wewe ni shujaa kwa kuwa umefanya kitendo ambacho wengi wetu tunashindwa! Kuomba msamaha hadharani tena mtandaoni ni ujasiri na unyenyekevu wa hali ya juu.

Tunaamini kuwa huu ni ushuhuda kwetu sisi, Kanisa letu na hata nchi yetu. Wale waumini na Wachungaji wetu ambao walitukimbia kwa kuambiwa uwongo au kutishwa watapata kitu cha kujifunza na wale waliobaki pamoja na sisi wataimarisha zaidi kiimani.

Ushuhuda wako ni uponyaji kwetu, uponyaji kwa Kanisa letu na uponyaji kwa taifa letu. Ni ushuhuda uliokuja katika wakati muafaka kwani sisi Askofu tunaendesha Kampeni ya kuundwa Tume ya Ukweli na Maridhiano ili watu wasameheana. Wewe umeonyesha njia.

Ninatumia nafasi hii kuwasihi Mheshimiwa Lissu, Mheshimiwa Mbowe na Watanzania wote ambao walikwazwa na wewe kwa namna moja ama nyingine kukusamehe kwa kuwa hata sisi Askofu tumekutangazia msamaha.

Ninakutakia amani ya Mungu ipitayo ufahamu wote. Wafilipi 4:8.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 24 Mei 2023; 01:35 pm"
Veronica France ni account nyingine ya mdaiwa wa marehemu.
 
Kwenye Ukurasa wake wa Face Book wa Veronica France amepost ujumbe wa Kuomba Msamaha kwa Maneno ya kuudhi aliwahi kuyatamaka kwa Askofu na Viongozi wa Chadema Mbowe na Lusu

Akionyesha kuwa anajutia yote aliyoyafanya Veronica aliandika hivi

"Baba askofu, nachukua hatua hii muhimu katika maisha yangu kukuomba msamaha katika maeneo yote niliyowahi kukukosea kwa makusudi au kwa bahati mbaya,najua tunatofautiana ktk itikadi na mitazamo,lakn nilikuwa nakukosoa katika namna isiyo ya kiungwana na kistaarabu ya matusi,kejeli,nilipungukiwa hekima mbele za Mungu na mbele yako,lakin sasa najutia na nanyenyekea sana mbele za Mungu na mbele zako,naomba radhi sana naomba unisamehe kama kijana au mdogo wako vyovyote vile.

Nilipotoa Lugha ya matusi, kejeli na kashfa, naomba unisamehe,alfajiri ya Leo nimejitafakari sana na nimechukua maamuzi haya bila kusongwa wala kishauriana na mtu, bali mimi na moyo wangu. Sometimes sitakiwi kufanya siasa za chuki na uadui, hata unapokosea sistahili, naomba sana unisamehe, nilitamani kuandika kwenye wall lakn nikaona usipo nitamkia msamaha hapa haita saidia.

Nelson Mandela aliwahi kusema "forgiveness is an attribute of strong people" and only warrior can ask for a forgiveness, hivyo, nifikishie msamaha wangu pia kwa Tundu Lissu, nilipomkejeli kwa ulemavu wake na situation aliyopitia,Naomba sana niombee radhi sana,anisamehe kama mdogo wake, nifikishie msamaha kwa Freeman Mbowe, tunajenga nyumba moja,na bado nasafari ndefu ya kujifunzanitakushkuru sana kama utaguswa na kunisamehe hata usiponijibu au kuandika lakini rohon kwako tu ukinisamehe nitakushkuru sanaasante sana na Mungu wangu wa Mbinguni akubariki.

Emmaus Bandekile Mwamakula"

Kufuatia hatua hiyo Baba Askofu Mwamakula naye alipost Kwenye Ukurasa wake wa Faceboo kuukubali msamaha wake.

Baba Askofu Alisema Hivi
"MAJIBU YA ASKOFU KWA VERONICA FRANCE!

Mpendwa Veronica France! Naona ulinipigia. Wakati huo nilikuwa kwenye phone conference. Lakini pia huwa situmii call hii ya messenger. Nadhani utakuwa unaelewa ni kwa nini situmii 'calls za messengers'!

Wito wangu wa Uaskofu una majukumu mengi sana ikiwemo kuwaombea watu. Tunapoomba tunaamini kuwa Mungu anasikia na pia hujibu maombi kwa wakati wake.

Sisi kama wanadamu tunatakiwa kuchukuliana na kusameheana pale tunapokoseana. Ni vizuri watu wakaelewa kuwa yote yaliyotendwa dhidi yangu binafsi, ninayahesabu kama gharama na sadaka yangu katika wito huu. Na hakuna wito usiokuwa na gharama.

Mungu aliwatumia watu walioniumiza ili kusudi niimarishwe zaidi. Ni kwa sababu hiyo, ingawa kuna wakati niliumia sana, lakini sikuwahi hata kidogo kuwachukia watu walioniumiza. Wengi niliwaombea na wachache sikushughulika nao.

Ukielewa jinsi upana wa vita yangu ilivyokuwa, huwezi kusononeka, bali utamtukuza Mungu pamoja nami kwa kunipigania. Hakuna vita isiyokuwa na majeruhi au hata vifo. Katika vita yangu, Wainjilisti 2, Wachungaji 7 na Askofu 1 walitukimbia. Tulipoteza sharika (parishes) 6 na tulidhurumiwa haki ya kupata viwanja vya kujenga Kanisa maeneo ya Mbweni na jengo 1 liliporwa kwa nguvu katika eneo ambalo kwa sasa sitaji. Vita nyingine dhidi yetu iliendeshwa kupitia kwa baadhi ya maofisa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Matusi ya mitandaoni dhidi ya Askofu yalikuwa yanapelekwa kwa waumini kwa lengo la kutaka kuwafedhehesha ili walihame Kanisa. Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha Kanisa linavurugwa ili Askofu asiwe na Kanisa kabisa. Baadhi ya watu waliwatumia baadhi ya maaskofu wa Kanisa moja kubwa nchini kuvuruga mahusiano yetu na partners wetu nje ya nchi.

Wewe hukuelewa upana wa vita hii dhidi yangu na laiti ungelielewa, basi leo ungekuwa katika kustaajabia ukuu wa Mungu kwetu. Katika vita yote hiyo Askofu aliendelea kuishi na Kanisa bado lipo ingawa nguvu kubwa ilitumika kupitia kwa baadhi ya watu waliokuwa katika nafasi za mamlaka ambao walikuwa wanatumiwa kutaka kulifuta Kanisa letu kutoka katika uso wa jua.

Mimi binafsi sioni kama nina hadhi ye yote ya kuombwa msamaha na wewe, lakini kwa kuwa nafsi yako imewiwa kutaka kufanya hivyo, basi ni sharti nikutangazie msamaha kwa dhati ili nafsi yako ipate amani. Kutangaza msamaha au kutoa ghofila ni moja ya majukumu yetu ya kila Jumapili. Kama Askofu asipotangazia watu msamaha atakuwa ameikana imani.

Kuhusu Mhe. Tundu Lissu na Mhe. Freeman Mbowe, naweza kuwaambia lakini kikubwa ni jamii kuelewa kwani mara nyingi wafuasi ndio huumia viongozi wao wanapofedheheshwa.

Kama wewe ukiweka public hata kwa sentensi chache katika ukurasa wako kuhusu kuomba msamaha, nami nitaueleza umma kuwa kweli ulinitafuta kwa jambo hilo na nimekusamehe. Vinginevyo, nikiandika bila ya wewe kufanya hivyo, watu wengi watajua kuwa ni drama tu.

Napenda nikuhakikishie kuwa hili ulilolifanya hapa litakufungulia wewe milango ya baraka na kukupatia kibari kwa wakuu wa nchi. Lakini pia usifadhaike utakapoona baadhi ya uliokuwa nao wakianza kukujeli na kukufedhehesha. Wewe ni shujaa kwa kuwa umefanya kitendo ambacho wengi wetu tunashindwa! Kuomba msamaha hadharani tena mtandaoni ni ujasiri na unyenyekevu wa hali ya juu.

Tunaamini kuwa huu ni ushuhuda kwetu sisi, Kanisa letu na hata nchi yetu. Wale waumini na Wachungaji wetu ambao walitukimbia kwa kuambiwa uwongo au kutishwa watapata kitu cha kujifunza na wale waliobaki pamoja na sisi wataimarisha zaidi kiimani.

Ushuhuda wako ni uponyaji kwetu, uponyaji kwa Kanisa letu na uponyaji kwa taifa letu. Ni ushuhuda uliokuja katika wakati muafaka kwani sisi Askofu tunaendesha Kampeni ya kuundwa Tume ya Ukweli na Maridhiano ili watu wasameheana. Wewe umeonyesha njia.

Ninatumia nafasi hii kuwasihi Mheshimiwa Lissu, Mheshimiwa Mbowe na Watanzania wote ambao walikwazwa na wewe kwa namna moja ama nyingine kukusamehe kwa kuwa hata sisi Askofu tumekutangazia msamaha.

Ninakutakia amani ya Mungu ipitayo ufahamu wote. Wafilipi 4:8.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 24 Mei 2023; 01:35 pm"
Lakini pia usifadhaike utakapoona baadhi ya uliokuwa nao wakianza kukujeli na kukufedhehesha. Wewe ni shujaa kwa kuwa umefanya kitendo ambacho wengi wetu tunashindwa! Kuomba msamaha hadharani tena mtandaoni ni ujasiri na unyenyekevu wa hali ya juu.
 
Attachments

  • FB_IMG_1684904521584.jpg
    FB_IMG_1684904521584.jpg
    58.2 KB · Views: 5

Back
Top Bottom