Baba askofu Kilaini akiri kupokea milioni 80.5

Baba askofu Kilaini akiri kupokea milioni 80.5

Nadhani hawa walipokea kama michango/sadaka za maendeleo ya Kanisa . Watz wanatakiwa wawe na moyo wakutoa sadaka nzito kama hizo za Ruge.. !
Makanisa yanazo akaunti benki. Hii ya kuweka michango ya kanisa kwenye akaunti ya Kilaini badala ya akaunti ya kanisa nayo inatia mashaka.
 
Kiongozi lazima awe informed, kama anachukua kila lijalo hii inatia mashaka sana!

Pesa tunazopewa toka wahisani toka huko Ulaya na nchi nyinginezo tunajua chanzo chake? Tangu lini ukaanza kumkamua mhisani source ya mapato ya pesa wakati alishachangia mengi siku za nyuma?

Nilizoea kusikia kwamba wachaga wa zamani waliozoea kuiba walihakikisha kiasi fulani wanapelekea pesa sadaka kanisani kama sehemu ya kutubu dhambi zao, mimi pengine naona hao walioamua kuelekeza pesa hizo kwenye shughuli za maendeleo wana uzalendo kuliko walioamua kujijengea majengo ya kifahari na kwenda kuserebuka na vimwana mahotelini.
 
Wewe wajua,aisee,caritas wanaoperate underground,watumishi wake wanalipwa mishahara minono vibaya,chanzo cha mapato ni misaada!just like usaid!
 
Suala la kujua hapa ni mambo mawili
  • Wachotaji wa pesa hizo
  • Wanufaika wa pesa hizo

Wenye makosa na wizi ni wale waliozichota pesa hizo toka Acc ya ESCROW, wanaufaika wengi hata hawakujua pesa zinatoka wapi na zimepatikanaje
ila walichojua ni wahisani ndio wanasaidia miradi ya maendeleo yaliyokusudiwa.


Sasa wameshajua kuwa zilikuwa za wizi, kinachotakiwa ni kurudisha maadamu wameshajua na watusaidie Watz kujua na mengine yaliyokuwa nyuma ya pazia kama yapo.
 
Kama muumini wa R.C, Michango yote kwa ajili ya maendeleo ya kanisa, hupitia kwenye njia zinazoeleweka kulingana na Taratibu za kanisa Katoliki lilivyojiwekea. Hakuna pesa za kanisa zinaeopitia acc. Ya padri wala Askofu. Michango hupitia acc ya kigango, Parokia au acc. Ya jimbo endapo mchango huo unalazimika kupitia njia ya kibank. Kama ni sadaka au zaka pia hukusanywa ktk mazingira ya uwazi. Baba Askofu una mengi ya kujibu waumin wako tuweze kua na iman tena na wewe.
 
Hela za Escrow zilipita Mkombozi Bank (Catholic Bank) pia wamepewa Maaskofu na mapadre wa Roman Catholic.

What if zingepita Amana Bank and wapewe Masheikh na maimam??
amini nakwambia.. katika makumi kadhaa ya watu waliopewa hizi fedha hakuna MUISLAMU HATA MMOJA.
sipati picha kama jambo hili lingekuwa ni kinyume chake. pasingekalika
 
Mkuu,mapdre na maaskofu katika kusihi kwao hawajitengi na jamii iliyowazunguka,wanao marafiki na wafadhili binafsi.Mfano hata parokiani kwetu Paroko wetu anapokea misaada mingi tu kutoka nje ambayo huja katika jina lake.Kupokea kiwango kikubwa kwa wakati mmoja si hoja,tatizo litakuja kama baba askofu alifahamu wizi huu.Rugemalira alikuwa ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kanisa la Cathedral Bukoba Mjini,Rugemalira amechangia ujenzi wa kanisa la Makongo Juu karibu nusu ya gharama.

Sawa kiongozi,umezungumzia michango na ujenzi wa makanisa,ni sawa kabisa,lakini je hizo fedha huingizwa kwenye account binafsi au ya parokia au ya jimbo?tena si inapaswa itangazwe hadharani?
 
Makanisa yanazo akaunti benki. Hii ya kuweka michango ya kanisa kwenye akaunti ya Kilaini badala ya akaunti ya kanisa nayo inatia mashaka.

Kiongozi wa kanisa katoliki huwa na account binafsi maana kuna wahisani ndani na nje ya nchi hutoa pesa kwa jina la Askofu, hilo halina ubishi. Pesa zikishaingia kwenye account yake anazielekeza kwenye account ya shughuli iliyokusudiwa na mhisani.

Account ya kanisa ni ile inayotokana zaidi na pesa za waumini kanisani na ipo chini ya kamati ya pesa ya jimbo na mhasibu mkuu wa jimbo.

Watumishi wa kanisa hulipwa posho zao, hivi wako huru kuwa na account zao iwe ni palepale jimboni ilivyozoeleka zamani, lakni siku hizi wengi hupendelea kuwa na account binafsi bank kuwa huru wanapozihitaji kwa matumizi binafsi, maana kutegemea account yake ya ofisi ya mhasibu jimboni utakuwa weekend ofisi imeungwa hawezi kwenda kuchota.
 
Baba Askofu zirudishe tu hizo fedha kwa mwenyewe kulinda heshima yako.Haina haja ya kuanza kutetea wezi utajidharirisha.
 
Wewe ni Mkatoliki pori ambaye unataka kuaminisha watu kuwa Kanisa Katoliki ni stationery. Kuna mambo ambayo Knisa Katoliki Kuanzia Actic na Anatactic tunafanana kama Ibada ya Misa Takatifu na Sakrament 7 za Kanisa. Lakini mengine kama zaka na mavuno ni mambo ya Kanisa Mahalia. Kwanza Altareni sadaka na zaka havipelekwi. Altareni kuankuwepo Msalaba unaface waamini wakati wote wa Misa. Sadaka na matoleo vinaletwa na kumbewa na kupelekwa mahali pake kwa baadhi ya parokia na parokia zingine haviletwi na kuombewa. Zaka maksanisa mengi wanapenda mtu apelike mweyneywe kwa padre au katekista au mtu mwingine aliyeaminiwa na unapewa stakabadhi. Uzuri wa Kanisa Katoliki tuna imani na mapadre wetu na hapa sipimi uaaminifu wa padre mmoja baada ya mwingine. Lakini majority receive funds and other gifts and account for them. Ndio maana wanansema tulilemazwa Wakatoliki kwa mtindo huu mapaka tukaona parokiani au mission ni mahala pa kuapata nguo, vyakula na elimu na tukawa hatutoi. Hili ndio linaanza kubadilishwa na watu wenye moyo wanatoa kama Rugemalira katika kusaidia Kanisa
Sawa mi ni mkatoliki pori,hapa unajidhihirisha hujawa mkristu kamili mwenye staha,huo msaada ulitangazwa?ni wa binafsi kwa kazi ipi?kama ni wa Jimbo sawa,na waumini wangetangaziwa makanisani kuwa Jimbo limepata msaada,lisemeeni kanisa,msililinde hta kama pale mambo hayaendi sawa,usiwe na akili za akina lusinde wewe.
 
Mbona wafanyakazi wake wanaoliopwa ujira wao hawakuingizwa kwenye hii sakata????!!
Au mwezi huo hakulipa mishahara wala hakufanya transactions nyingine???!!

Huyu unayemtetea aliuza nini au alitoa huduma gani labda??!!


tatizo zimetoka katika account ya tegeta!!!!! zisingekuwa zimetoka tegeta watu wasingehoji
 
Mimi ni mkatoliki,na ninavyojua hela ya sadaka au zaka itolewapo haiendi mfukoni au kwenye account binafsi ya Paroko au Baba Askofu,tena hailipiwi bank,hupelekwa kwa uwazi altareni na hubarikiwa kisha huingizwa katika makusanyo ya sadaka katika adhimisho la misa takatifu husika,hii kuingiziwa kwenye account binafsi nahisi utakuwa ni utaratibu mpya umeanza hivi karibuni,lets call a spade a spade by its name,lets stop going around the bush,if its rushwa lets say it rushwa.Full stop

Sawa tuseme ni rushwa, sasa ni kwa ajili gani mpaka ampe Askofu?
 
Sawa kiongozi,umezungumzia michango na ujenzi wa makanisa,ni sawa kabisa,lakini je hizo fedha huingizwa kwenye account binafsi au ya parokia au ya jimbo?tena si inapaswa itangazwe hadharani?
Inashangaza watu wanatumia nguvu kubwa kumtetea mwizi kilaini.
 
Kuwa mkatoliki si kujua yote yafanyikayo katika kanisa katoliki.
  • Pesa walizojengea Vyuo vikuu vilitolewa sadaka lini kanisani?
  • Pesa zilizotumika kujengea Zahanati zilikabidhiwa kwenye altare ipi?
  • Pesa zilizotumika kujengea vinu vya kufua umeme huko jimboni Njombe na Kikwete kufungua bakuli lilipitishwa wapi na wewe ukiwa mhasibu wake?

Ungeniambia unafanya shughuli za uongozi katika kanisa katoliki usingeuliza au kuleta kauli kama hiyo. Sadaka (offering - offeritorio) au Zaka ya kanisa huwezi kuweka kwenye mtiririko katika mfuko wa wahisani ambayo hutoa pesa za maendeleo kwa lengo maalumu iwe ni shule, afya, nak.

Ningekuelekeza mengi lakini naona kwa vile umeoshaonyesha upeo huo nisije kukuchanganya bure. Unajua idara ya CARITAS?

CC
ukombozi

Naijua sana,nimefurahi kwa kuanza kusema mimi ni mkatoliki kwani kwa jinsi povu linavyowatoka ningekuwa nimetoka ule upande mwingine ningetafuta pa kujificha,ila kama mnaona hii ya Askofu wetu kupewa mgao ni sawa,basi msiwalaumu akina ngeleja,chenge,tibaijuka.
 
Mimi ni mkatoliki,na ninavyojua hela ya sadaka au zaka itolewapo haiendi mfukoni au kwenye account binafsi ya Paroko au Baba Askofu,tena hailipiwi bank,hupelekwa kwa uwazi altareni na hubarikiwa kisha huingizwa katika makusanyo ya sadaka katika adhimisho la misa takatifu husika,hii kuingiziwa kwenye account binafsi nahisi utakuwa ni utaratibu mpya umeanza hivi karibuni,lets call a spade a spade by its name,lets stop going around the bush,if its rushwa lets say it rushwa.Full stop
Katoliki ipi wewe mcharuko?Hizo millioni zote upeleke ktk Altare,tena Bukoba?Mbona upo mbali sana nyuma ya wakati?Kwa taarifa yako hata Padre wetu aliwahi pewa hela km msaada kwa account yake binafsi.Mapadri na masista wengi tuu pamoja na kuwekewa sheria kuna vitu hupewa binafsi na wao kuamua virudisha ktk jimbo husika,au kutumia ktk miradi ya jamii waliyoanzisha kwa majina yao.Hapa ni UHAYA umejaa kuliko UDINI.Km hamjui kuwa scenario zinazidiwa na rangi,ukabila, udini,wizi, ukoo etc basi ndio mjifunze hapa.Ruge anasupport miradi ya kwao ambayo Kilaini kaianzisha.Tibaijuka nae na wengine ni uhaya.Nia mbaya dhidi ya Katholiki imewavutia kui paint vibaya.Ila kwanini hamkuweka Bank nyingine zilizoDeposit hela MKOMBOZI?NA BANK nyingine zilizopokea hela toka MKOMBOZI?Kamati za kiswahili za kijinga sana.Tanesco na ESCOW na account zao ni mkombozi?Akina chenge na wengine account zao ni mkombozi.
 
Huyu askofu alipohamishwa hapa Dar watu walimlaumu cardinal Pengo kwamba anamuenea wivu, kumbe alistahili huenda mambo yangekuwa mabaya kama angekuwa hapa Dar, jimbo la Dar lingechafuka na kushindwa kujisafisha.Na hili ndiyo limegundulika yapo mangapi maovu yamejificha.Baba askofu kuwa na huruma na Watanzania watakimbilia wapi?? kama viongozi wa kanisa mnaanza kuwa sawa na ma ccm??
 
Back
Top Bottom