Baba askofu Kilaini akiri kupokea milioni 80.5

Baba askofu Kilaini akiri kupokea milioni 80.5

tetemekoo

Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
35
Reaction score
11
Baba Askofu Methodius Kilaini akiri kua alipokea milioni 80.5 kutoka kwa Rugeemanila. Ila atoa rai kwamba wezi halisi wakamatwe na kushughulikiwa na siyo yeye!
==================
ASKOFU KILAINI AKIRI KUPOKEA MILIONI 80.5
10624820_1087373171277100_4372083134749819901_n.jpg

Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba Methodius Kilaini amekiri kupokea milioni 80.5 kutoka kwa James Rugemalira na akisema hii si mara yake ya kwanza kupokea fedha toka kwa mfanyabiashara huyo kwakuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamiii. Na michango amesema michango inayopelekwa kwake haina siri hivyo washikwe wezi halisi sio yeye

Chanzo: EATV
 
We hela unazopokea katika shughulizako kilasiku unajua zinakotoka? Au na wewe ni mwizi acha ujinga.

Mbona wafanyakazi wake wanaoliopwa ujira wao hawakuingizwa kwenye hii sakata????!!
Au mwezi huo hakulipa mishahara wala hakufanya transactions nyingine???!!

Huyu unayemtetea aliuza nini au alitoa huduma gani labda??!!
 
Eeee, mjadala umetusaidia kujua kuwa tetesi zilizokuwa zinaenea mtaani ni ukweli mtupu; mhhhh, laana hiyo!!
 
Suala la kujua hapa ni mambo mawili
  • Wachotaji wa pesa hizo
  • Wanufaika wa pesa hizo

Wenye makosa na wizi ni wale waliozichota pesa hizo toka Acc ya ESCROW, wanaufaika wengi hata hawakujua pesa zinatoka wapi na zimepatikanaje ila walichojua ni wahisani ndio wanasaidia miradi ya maendeleo yaliyokusudiwa.

kilaini_clip.jpg

[h=1]Askofu Kilaini, Nzigirwa wazungumzia tuhuma[/h]Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea Sh80.5 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira akisema si mara yake kwa kwanza kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamii.

Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni kutoka katika akaunti ya escrow.

Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi wengine wa dini walioingiziwa fedha katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh40.4 milioni).

Akizungumza kwa simu jana, Askofu Kilaini alisema Rugemalira hupendelea kuchangia kwa uwazi miradi ya kijamii na si yeye peke yake aliyempatia mchango, bali kuna watu wengine wengi ambao wameshampatia na kazi yake ni kuipokea na kuifikisha sehemu husika.

Hata hivyo, kabla hajafafanua zaidi hoja yake, simu ilikatika na baadaye hakupatikana tena.

Hata hivyo, jana askofu huyo alinukuliwa na Gazeti la Mawio toleo la jana akisema fedha alizozipokea kutoka kwa Rugemalira ni kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoendeshwa na Kanisa Katoliki.

"Ndiyo nimepokea fedha kutoka kwa James na hii siyo mara ya kwanza, kwani mara nyingi amekuwa akichangia miradi mbalimbali ya kijamii," alisema Askofu Kilaini.

Alipotakiwa na gazeti hilo kuwataja wengine waliochangia kanisa lake na kama nao wamechanga kutoka kwenye fedha za akaunti ya escrow, alisema yeye hayumo kwenye michango hiyo.

Alipoulizwa anawezaje kusema hayumo kwenye orodha ya waliopewa fedha kutoka akaunti ya escrow wakati anakiri kuwa aliingiziwa mamilioni ya shilingi na Rugemalira, alisema michango inayoletwa kwake haina siri, hivyo wezi halisi ndiyo wakamatwe.

"Michango inayoletwa kwangu haina siri, shikeni wezi halisi," alisema.

Askofu Nzigirwa

Kwa upande wake, Askofu Nzigirwa ambaye alirithi kiti cha Kilaini, cha Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam ameeleza kushtushwa kwake na ripoti ya PAC iliyomtaja yeye na Kilaini kuhusika katika uchotwaji wa Sh306 bilioni za escrow.


Hata hivyo, kiongozi huyo alisema anaandaa taarifa itakayofafanua kwa kina namna ambavyo fedha hizo zinazodaiwa zilitoka katika akaunti ya escrow zilivyoingizwa katika akaunti yake pamoja na hoja na maswali mengi yanayoulizwa na wananchi hasa waumini wa Katoliki kuhusiana na tuhuma hizo.

"Hizo taarifa zimenishtua sana. Bado nashangaa inakuwaje mimi naambiwa nimechota fedha kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow," alisema Nzigirwa alipokuwa akizungumza na gazeti hili jana.

Nzigirwa alisema anachofahamu hadi sasa fedha zilizoingizwa katika akaunti yake hazihusiki na escrow lakini atafanya uchunguzi ili kupata undani wa fedha hizo na majibu yote yatakuwa katika taarifa atakayoitoa kwa vyombo vya habari siku yoyote kuanzia leo.


Chanzo: Mwananchi
 
Mimi ni mkatoliki,na ninavyojua hela ya sadaka au zaka itolewapo haiendi mfukoni au kwenye account binafsi ya Paroko au Baba Askofu,tena hailipiwi bank,hupelekwa kwa uwazi altareni na hubarikiwa kisha huingizwa katika makusanyo ya sadaka katika adhimisho la misa takatifu husika,hii kuingiziwa kwenye account binafsi nahisi utakuwa ni utaratibu mpya umeanza hivi karibuni,lets call a spade a spade by its name,lets stop going around the bush,if its rushwa lets say it rushwa.Full stop
 
LOL!!!! Anayepokea mali ya wizi naye ni mwizi tu.

Kosa lo lote lile hata iwe dhambi mbele ya Mungu ulitende kwa kujua na kutaka. Unajua hili ni kosa halafu unalitenda, hilo ni kosa na ni dhambi mbele ya Muumba.

Waliokirimiwa pesa zilizotokana na ESCROW nijuavyo mimi mtu makini kama Askofu Kilaini isingekuwa rahisi kukubali kupokea angejua kwamba ni za wizi toka umma, alipokea kama msaada toka kwa mhisani ye yote bila kujua chanzo cha pesa hizo kama ni halali au la. Hakuna anayemwuliza mhisani umepataje pesa unazonipa.

Hilo jambo tunaona limeongelewa kifalsafa sana na kamati ya Zitto na kupeleka zigo kwa waibaji si wanufaikaji.
 
Unataka alama ipi tena wakati kuna ushahidi na mhusika mwenyewe kathibitisha kwamba alipokea mgao!?
Weka ushahidi aliposema amepokea mgao. Naomba katika ushahidi wako, neno 'mgao' lionekane wazi.
 
Hela za Escrow zilipita Mkombozi Bank (Catholic Bank) pia wamepewa Maaskofu na mapadre wa Roman Catholic.

What if zingepita Amana Bank and wapewe Masheikh na maimam??

Roho inauma hazikupita amana bank eeh?
 
Mbona wafanyakazi wake wanaoliopwa ujira wao hawakuingizwa kwenye hii sakata????!!
Au mwezi huo hakulipa mishahara wala hakufanya transactions nyingine???!!

Huyu unayemtetea aliuza nini au alitoa huduma gani labda??!!

Umeambiwa kwamba huwaanatoapesa kwaajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa imaniyake.we we unajua kwanini alitoapesahizo kwa askofu, au unahisi vitu tu kichani kwako. Mimi simtetei huyu askofu lakini nachukua tahadhari kwakuwa najua hata majizi huwa yanatoa sadaka nyingitu na hakuna mchungaji au padri anaejua huyomtoa sadaka amezipata wapi.
 
Back
Top Bottom