Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,806
- 11,968
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Misa Takatifu ya kumuombea Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere inayofanyika Kwenye Kanisa Kuu Katoliki Jimbo la Bukoba Mjini Mkoani Kagera leo tarehe 14 Oktoba, 2022
Misa hii inayoongozwa na Mhashamu Askofu Methodius Kilaini imehudhuriwa pia na viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais, Mawaziri, Wakuu wa mikoa, Spika mstaafu Mhe. Anne Makinda, familia ya Hayati JK Nyerere pamoja na watu wengine wenye mapenzi mema.
Askofu Methodius Kilaini-Msimamizi wa Kitume Jimbo la Bukoba
Amesema kuwa Mwalimu Nyerere alisimama msitari wa mbele katika kupambania haki na uhuru wa Afrika, alifundisha kwa maneno na mifano yake mema.
Amesema kwenye mwaka huu tunapokumbuka miaka 23 ya kifo chake na pia miaka 100 ya kuzaliwa kwa mwana huyu wa Kanisa, ni muhimu kukumbuka maneno aliyotoa kwenye mojawapo ya hotuba zake kuwa hakuacha kubeba vitabu viwili maisha yake yote ambayo ni kitabu cha azimio la Arusha na Biblia takatifu. Hii inaonesha kuwa alikuwa ni mtu aliyeishi siasa na maisha ya Mungu.
Alikuwa mtu wa kanuni za maadili na mcha Mungu, mwanasiasa mzuri ambaye watanzania wanamuita Baba wa taifa na Kanisa likimuita mwanadamu mwenye harufu ya Utakatifu.
Aliishi maisha ya kawaida na uduni, mtu aliyeapa kutokupumzika hadi Afrika yote ibaki huru, kuanzia Afrika Kusini ya ubaguzi wa rangi hadi Angola.
Nchini Tanzania aliunganisha makabila 130 yenye dini na rangi tofauti kuwa ndugu wanaopendana. Aliheshimiwa ulimwenguni kote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango, viongozi wengine wa Chama, Serikali, pamoja na Waumini wa Kanisa hilo wakiwa kwenye Misa Takatifu
Akiwa na umri wa miaka 63 aliamua kustaafu akiamini kuwa mamlaka ni Amana kutoka kwa Mungu. Hii ni tofauti kabisa na viongozi wengine wa kiafrika wa miaka hiyo.
Kuwa mtakatifu haimaanishi kuwa hautendi dhambi kabisa. Nyerere hakuwa malaika, alikuwa binadamu wa kawaida aliyetenda dhambi. Hata Mt. Petro alimkana Yesu, kisha akafanywa kuwa Mkuu wa kanisa. Alikuwa mkosefu, lakini alikiri makosa yake, mengine hadharani.
Tuendelee kumuombea apumzike kwa amani.
Philip Mpango-Makamu wa Rais
Nawaomba watanzania wote tuendelee kumuombea mama Maria Nyerere ili apate uzee mtakatifu na afya njema.
Tumesikia sifa nyingi hapa baba Kilaini akizielezea, toka uhuru alisisitiza sana uhuru na umoja. Tunamshukuru Mungu sana watanzania sisi bado ni wamoja, tuendelee kushikamana. Alisisitiza sana amani na kweli aliitafuta hapa nchini na tunajisifu kuwa kisiwa cha amani, na nchi zingine za Afrika. Tusibweteke.
Alisisitiza sana uhuru na kazi, hili ni jambo la muhimu sana. Lazima tuendelee kufanya kazi ili kuleta maendeleo. Ni lazima tufanye kazi, na lazima kazi iendelee.
Baba wa taifa alichukia sana rushwa, sasa sisi viongozi tunatenda haki, hatuwadai rushwa wanyonge? Nakumbuka baba wa taifa aliwahi kusema mtu anayechukua rushwa yafaa atandikwe viboko, Tanzania leo hakuna rushwa? Wanyonge wanapata haki yao? Ni jukumu letu sote, viongozi na wasio viongozi.
Alisisitiza sana kuhusu elimu na sisi tuliopata elimu tuliambiwa tunao wajibu wa kurudisha kwenye nchi yetu kile tulichopata. Nawaomba sana vijana wa kitanzania mnapokuwa chuo, mfanye bidii ya kusoma. Bado tunahitaji wataalamu wa kila aina.
Na sisi ambao tunatumika katika taasisi mbalimbali za Umma na Serikali kuu tufanye kazi kwa uadilifu, Msikwapue mali za umma, ni za wanyonge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini, Mapadri pamoja na viongozi mbalimbali