Baba achinjwa na familia yake akidaiwa kuwa kikwazo cha kutumia mali za familia

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano akiwemo Mkazi wa Kijiji cha Kiliwi wilayani Kwimba, Hoka Mazuri (48) na wanaye wawili kwa tuhuma kumuua mumewe, Mange Washa (49).

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amewataja watoto wa mwanamke huyo wanaoshikiliwa kwa mauaji hayo kuwa ni, Masunga Mange na Paskali Mange.

Mutafungwa amedai, ili kufanikisha lengo lao bila kushtukiwa wanafamilia hao walimlipa mkazi wa Bugembe wilayani humo, Shija Masalu (28) na Makoye Lusana (53) Sh800, 000 ili wamuue baba wa familia hiyo ambaye taarifa zinadai alikuwa kikwazo wanapohitaji kutumia mali za familia hiyo.

Amesema Desemba Mosi mwaka huu Saa 1:00 usiku baada ya kulipwa fedha na familia hiyo, Masalu na Lusana walimvamia Mange Washa akiwa amelala wakamkata kichwa na kukitenganisha na kiwiliwili kisha kutokomea kusikojulikana.

"Mauaji ya Mange yalipangwa na mke wake akishirikiana na watoto wake wawili kutokana na ugomvi wa mali uliyodumu kwa muda mrefu, kwani mmoja wa wana familia hiyo, Masunga Mange alifukuzwa na baba yake (Marehemu) kwa kuhusika na wizi wa mifugo ya familia yake na ya wakazi wengine wa kijiji hicho.

"Baada ya mauaji hayo Hoka Mazuri na wanaye wawili waliwahadaa watoto wengine ambao walikuwa wamelala nyumba nyingine jirani kwamba, baba yao amekatwa mapanga na mtu asiyejulikana, wakati wanaujua ukweli kuwa wao ndiyo waliopanga na kuratibu mauaji hayo," ameongeza.

Amesema watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa chini ya jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine, Kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo kupitia doria zake linawashikilia watu 104 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na kilo 29 za Bangi, na miche 40 ya bangi, mirungi kilo 62.6, lita 4,270 za pombe aina ya Gongo, mitambo 14 ya kutengenezea pombe hiyo na gramu 2.3 za dawa za kulevya aina ya Heroine.

Pia, amesema watuhumiwa wengine 18 wanashikiliwa kwa tuhuma za makosa ya uvunjaji wa nyumba na maduka kisha kuiba mali zikiwemo televisheni, simu na pikipiki.

"Pia tumekamata vifaa mbalimbali vilivyoibwa katika mradi wa ujenzi wa daraja la JPM Kigongo-Busisi na nyavu haramu za kuvulia samaki ndani ya Ziwa Victoria," amesema Mutafungwa.

Katika tukio lingine, Kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Jiwe Kuu kata ya Kitangiri wilayani Ilemela mkoani hapa, Merry Seni (21) kwa tuhuma za kutoa ujauzito wenye umri wa miezi saba na kutupa kichanga hicho.

MWANANCHI
 
Hii ni Afrika bhana ukiwa nazo ni kasheshe, ukizikosa ni kazeze
Sio Afrika tu mkuu.

Sema haya mambo tunayaona kama yameanza leo kwa sababu ya hii teknolojia ya habari ila ni matukio ambayo yapo miaka na miaka na sio Afrika tu, huko Duniani ni balaa.

Matukio ya watoto kuua wazazi wao kisa mali ni matukio yaa Dunia nzima sio Afrika tu.


Dogo alimuua baba yake kisa kampungizia pocket money yake.
 
Nakumbuka 2008 watoto wa baba yangu mdogo walimuua baba Kwa Mali za watu hata sio zake .

Alikuwa na ml 20 za kujenga kanisa walijua tu kuwa Mzee atakuja kutoka Nairobi so wakatega na saa wakamsubiria wakamkita na akafaa baada ya wiki mbili Kwa maumivu makali .

Na walipofikishwa mahakamani hawakuwekwa jela kwasababu kipindi hicho wao walikuwa wakubwa Tena wanahela bado ni mapolisi so hakuna njia ya wao kufikishwa mahakamani so ndio ikaisha hivyoo.
 
Itafika kipindi wanaume tunaojielewa hatutaoa kabisa ni mwendo wa kuzalisha tu ila kuishi na Mwanamke 0 distance Hapana
Wanyiramba sifa ya wanaume wanyiramba .

1.hawajali hata kama wameoa wao hupenda Malaya sana.

2.wavivu kutunza familia zao na pia hupenda kutokula miilo yenye kuleta afya

3.wanapenda kuvaa nguo nzuri Ili hali watoto hawana chakula chenye afya Wala hawana ada wapo wapo tu ila wanapenda sex balaa na video viumo vya nyiguu
 
Back
Top Bottom