Tatizo la elimu yetu ni kubwa kuliko tunavyo fikiri ,kizazi cha wanafunzi waliopita Ilboru,Mzumbe,Tabora boys,Tabora girls,Msalato,Kilakala,Kibaha,Moshi tech,Tanga tech ,Ifunda ,Old Moshi ,Pugu Nk ndio hivyo kinaisha na walau wao walipata elimu nzuri hasa japo kutumia elimu nzuri ni jambo lingine kabisa ,kizazi chetu cha kuwafaulisha wasiojua kusoma na kuandika ndio kinashika hatamu sasa sijui tatafanyaje maana hao wasiojua kusoma na kuandika ndio wanao tegemewa kuwa madaktari,Mainjinia ,Wanasheria ,Walimu nk ,naona ufanywe mpango wa kurudisha zile shule maalumu ikiwa pamoja na za ufundi na kilimo ,