Ni kweli mkuu unachokisema ,Elimu yetu haitujengi kukabiliana na changamoto za moja kwa moja baada ya mafunzo ,Nyerere kidogo aliona mbali akaja na shule kama Moshi Tech,Tanga Tech,Arusha tech shule zenye mitaala ya agriculture nk ,shule hizi zilikua zinampa mtu fursa hata ya kujiajiri mwenyewe anapo maliza kidato cha nne ,sasa mtu kama huyu akifika chuo chenye mazingira mazuri kama alivyosoma O level lazima atakua mzuri tu ,ndio maana sasa hivi ni bora umwajiri mtu aliyepita VETA kusomea mathalani umeme ,kuliko aliyesoma mathalani UDOM ama UDSM ,