Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,061
- 144,492
Katika jitihada za kuondoa picha ya kuwa na Bunge la chama kimoja,na kuondoa dhana inayojengeka kwa kasi sasa kwamba demokrasia sasa imekufa, watachofanya hawa mabwana ni kutuletea kitu kinachoitwa "Mgombea Binafsi" ingawa yatakuwa ni yale yale tu maana mifumo ni ile ile.
Katika hili, baadhi ya wapinzani waliofanyiwa figisu katika uchaguzi huu wanaweza kushawishiwa kutumia fursa hiyo katika chaguzi ndogo zitazojitokeza siku zijazo na huu pia utakuwa ni mkakati wa "'divide and rule". Hivyo, baadhi ya wapinzani waliokosa ubunge leo hii, kesho wanaweza kurudi Bungeni kwa njia hiyo.
Hoja kuu watayotumia ni uamuzi wa CHADEMA na ACT kukataa kupeleka majina ya wabunge wa Viti Maalum na watasema hii njia itasaidia kuwapa fursa wanaobanwa na vyama vyao hasa kina mama-propaganda.
Time will tell.