Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Nyungu nishafanya sana hii maamuzi ni yako uachwe na boxer au uivue......

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu itakuwa ngozi yako ina afya sana.

Maana tukiachana na maswala ya ulozi ile kitu itakuwa inaondoa uchafu sana mwilini

Mtu unachemka jasho linatoka kama unapikwa yaani ilibaki kidogo ni amke nitimue mbio

Asee mvuke unachoma jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari. Njia sahihi na salaam ni kumuomba mungu tu tena Kwa imanii ya dhati mbona hutolala njaa.

Ukkdondosha chozi tu Kwa ajili yakee basi hitaji Lako unalipata linaweza lisiwe Kubwa lakini likakufanya uishii Maisha yako Kwa amani na furaha.

Hapo nilichokiona nii kuingia mikataba na majini.

Sikuu ya mwisho pataulizwa kipii kilichowapoteza Sana wanadamu patajibiwa majinii wamewapoteza Sana'a wanadamu mbalii na masanamu.

Binadamu tunapenda pesaa Mali pendo lakupindukia mpk muda mwingine tunafanya vituu vya ajabu. Yaani Kama umemuamini shetanii ujue mungu yupoo na anakuona

By the way hadith yako inafundisha na kuburudish

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu itakuwa ngozi yako ina afya sana.

Maana tukiachana na maswala ya ulozi ile kitu itakuwa inaondoa uchafu sana mwilini

Mtu unachemka jasho linatoka kama unapikwa yaani ilibaki kidogo ni amke nitimue mbio

Asee mvuke unachoma jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
😅😅😅 Uvumilivu ukakushinda.
Hii ni tiba ya mvuke. Baadhi huwa wanaitumia kujitibu kwa kufukiza majani ya mkaratusi hasa Eucalyptus maidenii + Lantana camara + mchaichai.
Inakuwa ni league kati yako na mvuke😅.
POLE.
 
Unajua kusimulia chifu kuna sehemu nimecheka sana afu nipo peke yangu nasoma hii story,nimecheka mpaka machozi daa mkuu we mkali wa kusimua yaani imekuwa kama naangalia movie fulani amazing asa hapo kwenye kilinge unapambana na mvuke,jamaa wanakawa wanatupia tu mawe kwenye sufuria na mzee unaachia kilio kama mtoto mdogo, na kile kichapo cha ufagio mpaka maji yanaisha yenye ujazo wa lita 20
Yote hiyo ni kutafuta tiba ya ufukara😂😂
 
Inaendelea........


Nilikaa pele kwenye majani ya migomba kama masaa 3 hivi hadi jua likaanza kuwa kali maana lile jumba lilikuwa liko wazii kwa juu.

Nilikaa pale nikaangalia juu nikawa naona jua linavyo nipiga huku nikiendelea kutoa manyoya ya kuku ambayo yalikuwa yameganda sehemu mbali mbali za kwenye mwili wangu nikaanza kujiuliza hivi kweli ndio nimeamua kupitia njia hii?

Sikuwaza sana wala sikujutia kutokana na maisha ambayo nilikuwa nimepitia hapo nyuma, maisha ya kuomba omba kwa watu na kufanya vibarua vya ajabu ajabu. Ada yenyewe ya masomo nilikuwa mpaka nikapige magoti kwa afisa elimu kama mtoto yatima ndio itolewe .

Wakati bado naendelea kuwaza nikasikia sauti ya yule kibaraka wa mganga ananiambia vaa nguo unifuate basi baada ya hapo nikapelekwa hadi kilingeni nikamkuta mganga akaniambia kaa kwenye kigoda kisha akaniambia vua shati na suruali upandishe hadi magotini.

Baada ya hapo akachukua kibakuli kilikuwa na unga mweusi pia akachukua wembe akaupasua akaanza kunichanja, Alianza kunipiga chanjo mbili mbili kila sehemu kuanzia utosini, kifuasi, nyuma ya shingo, kwenye viwiko vya mkono, kwenye magoti, panapo unganisha mkono na kiganja, pia mwisho wa miguu kwenye maungio ya mguu na kikanyagio.

Alipomaliza akaanza kunipaka ule unga mweusi alipomaliza akaniambia niondoke na nisije nikaoga mpaka kesho yake nirudi kupata maelekezo mengine niliondoka hadi pale tulipopewa chumba nikamkuta jamaa yangu amesha fika na amefanyiwa kama mimi niliyofanyiwa.

Basi tulilala hivyo hivyo kesho yake asubuhi tukawahi kwa mganga baada ya kwenda tuliingia pamoja na agustino kisha tukapatiwa dawa ya kwenda kuogea halafu mganga akatuambia tumebakiza mambo machache tu tukamikishe yaliyotupeleka pale.

Akatuambia siki ile ile tunatakiwa kwenda kati kati ya barabara yaani njia panda majira ya saa saba usiku tufanyiwe dawa halafu itakuwa imebaki hatua moja ili tuweze kuondoka basi tuliondoka tukaenda tukaoga tukapumzika ili ikifika mida mida ya usiku tuanze kwenda kwa yule mganga.

Baada ya muda kufika tulienda kwa mganga akatukabidhi kijakazi wake alitoa zile kaniki nyeusi ambazo tulikuwa tumekwisha zinunua akatuambia tuvae kisha tukaanza safari haikuwa mbali sana kama mita 250 tukawa tumefika.

Baade tulikaa kati kati ya bara bara akatuchanja utosini akafanya madawa yake pale halafu akatoa kijembe kidogo sana unaweza kukishika na mkono mmoja tu akachimba udongo kisha akatuambia kila mmoja achote mchanga tukaweka kwenye mfuko kila mtu tofauti halafu kwenye lile shimo akatoa dawa flani akafukia mule.

Baada ya hapo tukaondoka tukarudi hadi kwa mganga ,tulikuta mganga anashughulikia mama mwingine na watu kadhaa walikuepo sisi yule jamaa akatuambia tuondoke halafu kesho asubuhi turudi tena

Kesho yake asubuhi tukaenda mganga akatuambia imebaki hatua moja pia mizimu na mababu lazima ipate zawadi ambayo ni damu ili ipate furaha itutekelezee jambo letu vizuri tukasema hakuna tatizo tuko tayari basi mganga akatuambia lazima mlipie gharama shillingi 50000 kwa wale vijakazi yeye malipo yake tutarudisha mambo yakiwa sawa basi jamaa yangu bila kusita akatoa pesa yote pale pale.

Kisha wakasema leo usiku ndio tunaenda kumaliza kila kitu tutoe na pesa wakanunue nazi na udi kwa ajili ya kazi yetu baada ya hapo wakatuambia tuondoke turudi usiku maana kazi itaanzaa saa sita usiku.

Basi tulikuwa na furaha tukijua kuwa tunaenda kumaliza kila kitu ili turudi tuendelee hata kupiga msuli maana nakumbuka jamaa alikuwa kwenye begi amabeba mastering history awe anapitia pitia lakini hakuwahi igusa hadi tunatoka pale kwa mganga

Basi usiki kwenye mida ya saa 5 tukajisogeza pale tulikuta jamaa wameandaa vitu kadhaa wamaweka kwenye gunia basi tukaanza safari nilikuwa nadhani tunaelekea njia panda laahaula baada ya kutembea sana kama kilo mita moja tukajikuta tuko eneo la makaburi daa nikaanza kuogoba basi tulivyofika jamaa wakatuambia tubadili nguo yaani zile kaniki nikikumbuka nacheka sana tulikuwa kama bongo movie kisha jamaa akatoa kile kijembe akachimba mbele ya kaburi moja .

Akaniambia chota mchanga na mkono wa kulia basi nikachota nikauweka kwenye kile kimfuko cha kule njia panda halafu akaniambai nilale juu ya lile kaburi pia na jamaa yangu akaambiwa afanye hivyo hivyo basi wakawasha udi kuzungula lile kaburi.

Daa wakangomani ni hatari asikwambie mtu nilisikia wanaanza kuongea lugha nisiyo ielewa wakawa kama wanakemea mapepo yaani zaidi ya walokole wanavyokemea kisha walikuwa na kikamba kama kombeo cha kupasulia nazi wanaingiza nazi ndani yake wakati huo mimi nimelala chali halafu wanapasua nazi juu ya kaburi usiki unasika kama baruti

Kwa kuhesabu haraka haraka walipasua kila mmoja nazi kama saba kisha tukaondoka wakatuambia tuondoke bila kuongea kitu chochote tukafika hadi kwa mganga wakatuambia tuondoke tusiongee jambo lolote hadi kesho asubuhi turudi pale tupewe maelekezo ya mwisho.

Kweli tuliondoka hatukuongea neno lolote kila mmoja alijikausha hakuna ambaye hata alikohoa, asubuhi na mapema tukafika pale kwa mganga tukakuta mabaharia wengine wako pale wanaonge tu habari za madini baadae tuliitwa maana Sisi tulikuwa ni kama tumesha maliza basi.

Mganga sikuio ni kama alikuwa na furaha sana tulionge story za kawaida kisha akatuambia naona kabisa mnaenda kutimiza malengo yenu dawa zote na kila kitu kimeenda sawa sasa ni hivi akatoa ule mchanga ulikuwa katika kila kimfuko akanipatia mimi na agustino pia kisha akatoa mbegu za maharage akanipatia mimi mbili na agustino mbili akazifunga kwenyw karatasi nyeusi .

Kisha akatuambia hizi mbegu mtaondoka nazo kila mmoja kwa wakati wake atanunua jogoo mwekundu halafu mida ya saa saba usiku utaenda upandikize kwa kutumia huu mchanga maji usimwagilizie itakuwa ni damu ya yule kuku kisha utahesabu siku saba utaenda kuangalia kama imeota angalizo nalo wapa usionekane na mtu yoyote yule.

Pia akatuambia baada ya siku saba ukikuta hazija ota usijisumbue kurudi kwangu maana mambo yako yatakuwa yamesha haribika mizimu itakuwa imekukataa sito weza saidia kitu chochote.......






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua kusimulia chifu kuna sehemu nimecheka sana afu nipo peke yangu nasoma hii story,nimecheka mpaka machozi daa mkuu we mkali wa kusimua yaani imekuwa kama naangalia movie fulani amazing asa hapo kwenye kilinge unapambana na mvuke,jamaa wanakawa wanatupia tu mawe kwenye sufuria na mzee unaachia kilio kama mtoto mdogo, na kile kichapo cha ufagio mpaka maji yanaisha yenye ujazo wa lita 20
Yote hiyo ni kutafuta tiba ya ufukara
Inaendele mkuu karibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja sana. Naona mzigo unazidi kunoga

Thanks

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaaah maisha haya

Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha n Utata kweli

Barnes
Nimeweka kituo
Keshoooo naamka nayo
Ukiendelea nitag pls

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
Dadeki mateso yote hayo kama vile mwizi
Aloo hii story tamu,Sina mashaka nayo naamini Jamaa anasimulia kitu alichopitia kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Asubuhi ntaamka nayo hii Inshallah

Sent using Jamii Forums mobile app
umegusa mulemule kasoro wewe walikuacha na boxer..
huwa zinavuliwa zote
Nyungu nishafanya sana hii maamuzi ni yako uachwe na boxer au uivue......

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseee
Endelea na Wewe Mkuu Story yako humu humu
Mkuu tafadhali sana Tag lako ni muhimu sana ili kuufatilia huu uzi

One plus+
Story nzuri inavutia kusoma ina ujumbe mzuri
Akiendelea mnitag wakuu tafadhalini sana.
Basi kila fundi na ufundi wake
Tayari ni me subscribe..amka uendelee na story mana imenoga.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Unitag mkuu ukiendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
Tupo pamoja
aisee najua baadhi humu watakuwa wamepitia haya
Tunasubiri kuusikia mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatari. Njia sahihi na salaam ni kumuomba mungu tu tena Kwa imanii ya dhati mbona hutolala njaa.

Ukkdondosha chozi tu Kwa ajili yakee basi hitaji Lako unalipata linaweza lisiwe Kubwa lakini likakufanya uishii Maisha yako Kwa amani na furaha.

Hapo nilichokiona nii kuingia mikataba na majini.

Sikuu ya mwisho pataulizwa kipii kilichowapoteza Sana wanadamu patajibiwa majinii wamewapoteza Sana'a wanadamu mbalii na masanamu.

Binadamu tunapenda pesaa Mali pendo lakupindukia mpk muda mwingine tunafanya vituu vya ajabu. Yaani Kama umemuamini shetanii ujue mungu yupoo na anakuona

By the way hadith yako inafundisha na kuburudish

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamn bado tu new epsode

Sent using Jamii Forums mobile app
Uvumilivu ukakushinda.
Hii ni tiba ya mvuke. Baadhi huwa wanaitumia kujitibu kwa kufukiza majani ya mkaratusi hasa Eucalyptus maidenii + Lantana camara + mchaichai.
Inakuwa ni league kati yako na mvuke.
POLE.
Mkuuu nasubiria episode...
Jamaan huuu Uzi kuna mahali nacheka mpaka machozi yanatoka...


Kwamba hudhani kama utakuja kutoka najasho lile hahaha
Mkuu ukiendelea tusituane
ila tunainjoi mkuu au sio?
Mwanaaa
Hivyo sindo vile vilikua vitu vya Mzee wako
Hatari sana...



Cc: mahondaw
-

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom