Habari wana JF, mimi ni new member ningependa mnikaribishe katika Jukwaa letu.
Mimi Ni kijana wa miaka 30’s, kwa mda wa miaka 3 nimekua nikisumbuliwa na Nguvu za giza na Mizimu ya ukoo ambayo imepelekea kuharibu dira ya maisha yangu, nilianza na kuumwa homa za ajabu ajabu, mwili kuchoka, dalili za homa ya Presha.
Nilihangaika sana ikiwemo kwenda kwa waganga wa kienyeji, nikawa napata nafuu lakini baada ya mda hali inarudi palepale, nikajaribu na makanisani ikawa ni vita kali, nako nikawa napata nafuu ila hali inarudi pale pale ikiwa kuhisi mwili unaumwa, kuchoka, macho kuhisi yana kiza na Moyo kuuma sana.
Nilihangaika pia na maombi binafsi ya kujiombea mimi mwenyewe pamoja na watumishi wa Mungu, nikafanikiwa kupunguza hii hali kwa kiasi chake nikapata nafuu.
Kuja kwenu wanaJF ninaomba ushauri kwa sababu nimefungwa upande wa uchumi, akili yangu imefungwa.
Inafika hatua ya kukata tamaa na kuona kila kitu hakiendi na pia kila ninapopata ishu ya kazi au dili lolote hua inafika sehemu mambo yanaharibika, nimekua na roho ya kukataliwa, kila ninapoenda ninadharauliwa na kubezwa, nilishaenda sehemu nikahisiwa mimi ni Mwizi, kiukweli ni kama nina mikosi au gundu.
Siku Moja niliwasiliana na ndugu wa baba ambao wao ni wasukuma, wakaniambia hio kawaida kuna mizimu inabidi kwenda kutambika kwa sababu ukoo wetu tangu enzi ni wa mambo hayo ya kimizimu.
Nipo kwenye dilema nikubaliane na mambo ya kutambika au niendelee huku niliko upande wa Makanisa, japo kiukweli napata vita kubwa kila napopigana na hizi nguvu makanisani.
WanaJF kiukweli nimefika hatua nachanganyikiwa, kila kitu hakiko sawa, nakosa kujiamini kwa kila jambo nalotaka kufanya, ninaomba ushauri wenu na mawazo yenu.
Najua Jukwaa hili lina watu wenye maarifa na maono. Nitashukuru sana
Cc MshanaJR