Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

jooohs

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
1,182
2,000
Baada ya siku nyingi kupita leo nimemkumbuka rafiki yangu kipenzi ambaye alipatwa na matatizo makubwa katika safari yake yakusaka maisha miaka kama 5 iliyopita tukiwa kidato cha sita yaani kila nikikumbuka nabaki kulia tu.

Wakati naripoti shuleni nilikuwa nimechelewa kidogo baada ya kufika pale kutokana na jitihada zangu za masomo darasani nilitokea kuelewana na jamaa mmoja alikuwa anaitwa Agustino yeye alikuwa anasoma HGE mimi nilikuwa EGM masomo mengi tulikuwa tunaendana tukawa tunadiscuss pamoja

Kumbe jamaa huyo Agustino alikuwa amejisajili kama Private Candidate so alikuwa anatokea kitaa kuja shuleni baada ya urafiki kuzidi nikawa natoroka mara kwa mara tunaenda kukaa getto na kupiga story pamoja na masela wengine

Kifupi wakati ule nilikuwa na kama miaka 18 lakini kutokana na mwili wangu tulikuwa tukitembea nae unaona kama mimi nimkubwa maana alikuwa anamwili mdogo mdogo sana

Wakati natoka nyumbani nilikuwa bado sina mawazo kichwani ya kuwa na pesa nyingi nilichokuwa naona mbele yangu ni namna gani nitafaulu kidato cha sita michongo ya pesa niliowahi kufanya ilikuwa ni vibarua vya kawaida kitaa

Lakini jamaa yangu alikuwa ni mtu wa mishe mishe nyingi kila akikaa lazima apigiwe simu, tukiwa tunaongea lazima apige story za maswala ya pesa. Wallet yake akitoa hela unaona imejaa misimbazi nikawa najiuliza jamaa hizi hela anatoa wapi nikabaki kusema labda kwao watakuwa wanajiweza sana, japo ukimuangalia vizuri haonekani kama katokea kwenye rich family.

Getto alipokuwa amepanga lilikuwa limesheheni kila kitu,
Mtaani pale alikuwa amezoeleka na watu wengi chocho nyingi akawa ananionyesha sasa kuna siku weekend kaniambia nimsindikize akachukue pesa yake kwa jamaa yake mmoja.

Alinipitia pale shuleni tukaondoka kuelekea kwa huyo jamaa shule tuliokuwa tunasoma iko maeneo ya kijijini so tulukuwa tunapita njia za vichakani chakani kuna mashamba wanalima nyanya, na matikiti maji nyumba ziko mbali mbali sana.

Baada ya kuvuka kamto tufika kwa yule jamaa mimi ikabidi ni baki njee halafu jamaa mwenyewe kumuona umri ulikuwa kama umeenda hivi ,alikuwa na zaidi ya 50 year tulisalimiana wenyewe wakaingia ndani lakini kwa njee nilisikia kama mabishano ambayo sikujua wanazungumzia nini....

Kwa mwendelezo bonyeza link hizi.

Sehemu ya pili
Sehemu ya tatu

Sehemu ya nne
Sehemu ya tano

Sehemu ya sita
Sehemu ya saba

Sehemu ya nane
Sehemu ya tisa

Sehemu ya kumi
Sehemu ya kumi na moja

Sehemu ya kumi na mbili
Sehemu ya kumi na tatu

Sehemu ya kumi na nne
Sehemu ya kumi na tano

Sehemu ya kumi na sita
Sehemu ya kumi na saba
 

jooohs

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
1,182
2,000
Sasa baada ya muda kama dakika 15 hivi ya mazingumzo agustino akatoka njee akaniambia wamesha malizana tukapita tukakata miwa halafu tukaondoka njiani agustino akaniambia huyu mzee anapesa yake nyingi lakini ataki kumrudishia amekuwa akimzungusha na malipo kidogo kidogo

Lakini sikutaka kufatilia sana maana nilijua ni madeni tu ya kawaida nilirudi hostel yeye akapitiliza getoni kwake, ilipita kama mwezi jamaa akaja kuniambia anaenda mkoa fulani kumuona ndugu yake baada ya wiki moja atageuza nikasema sawa.

Alikaa kama wiki mbili nakumbuka ilikuwa juma mosi mida kama ya saa 8 hivi mchana akanipigia simu nilikuwa na tecno jeneza kisimu flani hivi kigumu, akaniambia nichomoke hostel na jamaa yangu mmoja alikuwa anaitwa Muddy twende tukampokee amekuja na vitu vingi tumsaidie kupeleka getto wala sikusita nikamwabia muddy agustino amesema tukampokee tuliondoka mpaka centre tukachukua boda hadi stendi baada ya muda kidogo akafika

Alikuwa amekuja na mabegi 4 makubwa sana yaani ni makubwa kweli kweli pamoja na mazaga zaga mengine kwenye mfuko akaniambia nikaite tax nikaenda kufata wakaelewana bei kisha tukamsaidia kupakiza kisha akatuachia 10000 akatuambia tuchukue mizigo iliyobaki tuipakie kila mmoja kwenye boda turudi nayo getto kweli tulifanya hivyo

Tulivyorudi tukamkuta ameshafika getto tukaanza kupiga yale mazaga zaga aliyokujanayo biscuit, pop con,ndizi baada ya hapo akasema kesho tumpeleke town tukiirudi kuna kitu anataka kutueleza maana sisi tumekuwa masela wake watiifu sana

Kweli kesho yake tukachukua usafiri mpaka mjini breki ya kwanza akasema tumpeleke atm kiukweli niliona kama maajabu how comes kijana mdogo anakadi ya bank maana mimi mpaka muda ule nilikuwa naenda bank kulipa ada tu sikuwahi kanyaga bank kwenye ishu yoyote ile. Alitupeleka hotelini tukapiga msosi tukapita pita mjini akatununulia baadhi ya vitu nayeye kanunua kisha tukarudi getto.

Tulivyofika getto ndio jamaa akaanza kufunguka kuhusu biashara anayofanya mazingira ya pale kabla hajaendelea kutupa story ndio akatuambia sogezeni begi moja niwaonyeshe daa akachukua funguo ndogo akafungua kijikufuli flani hivi kuangalia ndani nikasikia marashi ya kufa mtu, juu kulikuwa na taulo kama la kuogea akatoa lile taulo baada ya hapo akatoa kitenge kikubwa kilichokuwa kimefuniika mzigo baadae akamalizia karatasi ya nailoni daa kutoa niliona vitu kama mifagio ya kijani.

Harufu ya bangi ikatoka kali kifala chumba kizima tukabaki kushangaa na jamaa yangu muddy kisha yule agustino akaanza kusema hii ngoma imekauka sana akachukua maji akaanza kuirushia rushia maji huku akituambia hii njia ni safe sana askari hata awe mjanja kiasi gani hawezi kushitukia mchezo akaanza kutuambia yeye ndio supplier wa bangi ule mtaa mzima na anatengeneza faida kubwa kwani anakotokea zinalimwa kama mchicha bei ndogo akija huku anapata faida kubwa sana.

Jamaa aliendelea na ule mchezo kuna wauzaji wengine alikuwa anawapelekea mali kauli kama yule mzee kisha tunaenda kufata pesa baada ya siku kudhaa tulikuwa tukienda kwa yule babu tunakuta ameikata kata ile mifagio imekuwa kama chenga halafu anaitengeneza na rizila inakuwa kama sigara tulikuwa tukifika tunachukua kwanza kama stiki tatu tatu tunavuta stimu zikipanda tunasepa yaani nilijikuta kwenye uvutaji wa bangi bila kujua.

Kuna siku alituita akatuambia katika maisha yake amejaribu kila njia ya kupata pesa nyingi lakini dili zake bado hazijakaa sawa ila kuna ndugu yake amemuelekeza kuna mganga mkongomani yuko mahali ukitaka utajiri ni ndani ya siku kadhaa tena hana masharti magumu akatuambia lazima aende ndipo na mimi nikamwambia tufanye likizo na mimi nije niendee nikajaribu bahati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MC44

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
1,357
2,000
Tuendelee.
Ilipita siku kadhaa safari ya kwenda kwa yule mganga ikawadia.

Hapo shule tushalegeza maana nilianza kufikiria pesa. Ukichangay a na bangi tulikuwa tunavuta ikawa ndio basi tena.

Kufika kwa mkongo anatueleza shida yetu kabla hatuja mweleza.

Na masharti yake ikawa ni kulala chini na kutoosha kichwa.

Kweli yale masharti niliyaweza na nikaanza biashara ya vitenge.

Asikuambie mtu mambo yalinyooka sana.

Nilianza na mtaji wa laki 6 Augustino alinipa ndani ya miezi mitatu nilikuwa na mtaji wa milioni 5.

Biashara ikachangamka sana na shule tukaacha.

Mara nikaanza kuona mambo ambayo siyaelewi jamaa akaniambia turudi kwa mkongo....kufika kule mganga kasema nilikosea sharti.
Inatakiwa nisafishe kwa damu ya mwanadamu.

Hapo nikawaza sina mke wala mtoto.

Nina mama na baba na ndugu zangu wa chache nikianza kutoa kafara itakuwaje.

Nikaamua rasmi acha nifilisike watu wawe salama.

Wazoefu wa biashara bila uchawi nipeni uzoefu nisimane tena.

NB:-HII STORY HATA SIO YANGU, NIMEIKAMILISHIA TUU.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom