Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Okay Inaendelea....

Ilichukua muda nikiwa pale njee nikitafakari yale niliyoyaona mule ndani kwenye kile chumba wakati agustino akiendelea kupigiwa ramli.

Basi ndipo agustino akatoka na kunioneshea ishara kuwa nizame kilingeni bila kusita nikaamka pale nikaingia moja kwa moja mule kilingeni nikakaa huku nikiwa ninenyoosha miguu yule mganga akaniambia kuwa weke 5000 ndani ya yale maji nikafanya kama alivyoelekeza.

Baadae akachukua udi akawasha akachukua kibakuli kilikuwa kama na mawe yanafanana na mayai akayashika mkononi akaanza kuyazungusha kwenye kiganja cha mkono halafu mkono mwingine akachukua mkia kama wa mbuzi akaanza kuchovya kwenye dishi la maji ananyunyiza nyunyiza wakati huo akaniambia ninyanyuke chini ni kae kwenye kigoda ambacho kiko mbele yake.

Kisha mfanyakazi wa mganga akaleta njiwa mganga akachukua ile njiwa akavuta kichwa hadi kikatoka kwa kutumia mkono kisha akaanza kuongea maneno ya ajabu sauti yake ikabadilika kabisa ikawa kama ya mzee aliyekabwa na kitu kooni licha ya kuwa na umri kama 40 hivi halafu akaanza kuongea kama wakongo man huku akitafuna meno balaa yani anatafuta unasikia sauti ya meno yakisagika ndani ya mdomo yule kijakazi wake ndio akawa anatafasiri.

Sijawahi kwenda kwa mganga sehemu nyingine ila nadhani wengi wao watakuwa wanapiga ramli kwa njia hii .

Jamaa aliyekuwa anatafasiri ndio akaanza kuniambia dhumuni langu lililo nipeleka pale kuwa nikutafuta pesa na kama nikitoa kafara za damu na kufata masharti lazima lengo langu litatimia tena nitakuwa mtu ambaye ni tajiri sana maana nyota yangu inangaa sana ,baada ya pale na blaa blaa nyingi mganga akarudi katika hali yale.

Baada ya hapo mganga akasema kabla ya kufanya kitu chochote inabidi kwanza tufanyiwe madawa ili kuondoa mikosi yule jamaa yangu agustino akaitwa tukaambiwa tukanunue kuku Jogoo mwekundu kila mmoja, kitambaa Cheusi na chekundu, mkaa, Wembe kama sisi ni wageni tutoe pesa wakanunue wao ili kesho asubuhi tuwahi kazi ianzee kiukweli sikuwa na pesa kila kitu jamaa yangu alinilipia baadae akaturuhusu kuondoka
Pia alitupatia dawa flani hivi yakuogea na kunywa usiku na asubuhi kabla hatujaenda Kwake

Tulivyorudi kwenye lile getto ndio nilikuja kujua kuwa ni kama nyumba ya wagonjwa na matatizo mbali mbali ya wanao enda pale kwa mgangaa tulitafuta kimgaahawa tukaenda kula huku tikipiga story za kujipa moyo kesho yake tukawahi asubuhi na mapema kwa yule mganga ila tulikuta watu kadhaa wameshafika.

Jamaa yangu ndio alikuwa wa kwanza kuingia baada ya watu kadhaa kuhudumiwa baada ya hapo alipelekwa kwenye kale kachumba kadogo kaliko kuwa pembeni asee baada kama ya dakika moja nilisikia anatoa kelele za vilio vya maumivu nikawa najiuliza hivi hiko chumba wanafanywa nini baadae akatolewa ameloa jasho vibaya akapelekwa kwenye lile pagara ambalo halijamalizika .

Zamu yangu ikafika nikaingia kilingeni mganga akasema ili kuondoa mikosi uliyokuwa nayo lazima upigwe nyungu, wengine wanaitwa kufukizwa, nikapewa dawa nikanywa halafu nikachukuliwa kupelekwa kwenye kale kakilinge kengine roho ikaanza kudunda huku nikijiuliza kupigwa nyungu ndio nini.

Nilivyofika jamaa kaniambia toa nguo zote nikabaki na boksa niliona ndani ya kile chumba kuna kahema kadogo sana kamatengenezwa na kitambaa kama cha mwamvuli nikaambiwa ingia humo halafu ukae kwenye kigoda kisha akaniambia ufumbe macho yaani usije ukafungua maana ukifungua tu matatizo utakayoyapata usije kulaumu mtu

Kweli nikafumba macho kwa nguvu zote huku nikiwa nimekaa kwenye kile kigoda kisha nikahisi kama wameingiza sufuria usawa wa miguu yangu kisha nikasikia jamaa ameingiza kitu kama jiwe kwenye lile sufuria nilitaka kufumbua macho lakini kwa vile vitisho niliogopa baada ya hapo niakaanza kusikia kama kunajoto limeongezeka kutoka kwenye lile sufuria

Baada ya sekunde kadhaa nikasikia kama jiwe lingine limewekwa na joto linaongezeka aseee mwili ukaanza kuchemka jasho likaanza kunitoka hadi masikioni ,likawekwa tena jingine nikasikia mvuke umetoka unaanza kunichoma asee maji ya kawa ya moto zaidi mvuke ukawa mwingi nikatamani niinuke pale lakini nikaona niharibu dawa asee sijawahi kuchomwa staili ile tokea na zaliwa

Uvumilivu ulinishinda na jamaa nasikia bado anaongeza nikaanza kupiga kelele nililia kama mtoto mwili ulikuwa umeloa kila sehemu nilitoka jasho sidhani kama nitatoa jasho kama lile hadi naingia kaburini maumivu yalipozidi nikasikia jamaa ametoa kile kihema ndio ikawa hafadhali mwili wote ukabali kutoa maji kama mvua baada ya dakika akaniambia vaa nguo unifate kweli nikafanya hivyo nilisikia nimekuwa mwepesi kama karatasi

Tulizinguka tukaenda kwenye kile kipagara kinavyumba vingi nikaenda kumkuta jamaa mwingine ameshikilia kuku akaichinja damu ikamwagika kwenye dumu lenye maji kama lita ishirini lilikuwa limechanganywa na madawa kadhaa kuku yule nae akatumbukizwa mule jamaa tena kaniambia simama kisha utoe nguo zote nikabaki na boksa.

Alikuwa na ufagio akawa anatumbukiza mule kwenye yale maji yenye dawa akitoa ananichapa nao tena kwa nguvu huku akiongea maneno fulani ambayo nilikuwa siyasikiii aseee nilichapwa mpaka yale maji yote yakaisha akabaki kuku mwenyewe kisha nikaambiwa kaa kwenye majani ya migomba waliokuwa wemetandika kwenye kile chumba nilikaa pale kama masaa matatu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya ustaarabu wa kunitag ukipost tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Anathet plz unitag ila hujaelezea pale kwenye kodolo lenye damu ukafunga mlango ukaondoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui nifanyaje kifurushi changu kina nusu saa tu na mzigo bado

Sent using Jamii Forums mobile app
Naweka alama hapa nitarudi badae

Sent using Jamii Forums mobile app
.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom