Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Natamani kuvunja ndoa yangu.

Habari zenu wakuu, natumai mko poa. Nimekuja na nia ya dhati kutafuta ushauri kuhusu jambo langu ambalo linanitatiza.

Mimi ni msichana mwenye umri chini ya miaka 30. Nina mtoto mmoja wa kiume. Nimekuwa katika ndoa na mume wangu kwa takriban miaka miwili sasa.

Sababu za maamuzi yangu ni kama ifuatavyo:

1. Uchepukaji uliokithiri: Huyu mume wangu amekuwa akinihadaa sana. Sijawahi kuona kitu kilichoniumiza zaidi ya kugundua kuwa anatoka na wanawake wengine. Ameomba msamaha kila mara ninapomfumania, lakini bado anarudia tabia hiyo. Kesi zetu zimekuwa nyingi kwa wazazi na nadhani wamechoka kutusuluhisha.

2. Ulevi uliopitiliza: Mume wangu ni mlevi sana. Kurudi nyumbani asubuhi ni jambo la kawaida kwake. Nimeshazungumza naye na kumweleza jinsi ninavyojisikia kuhusu tabia yake ya kunywa kupindukia, ingawa anahudumia familia vizuri. Lakini, hupati muda na familia kabisa. Inanidhalilisha sana kwa sababu tunakaa na mdogo wake nyumbani, hivyo najihisi vibaya sana anaporudi asubuhi.

Ndoa yetu imefungwa kanisani na tumekuwa tukiishi pamoja kwa miaka miwili tu. Nashauriwa nifanye nini kuhusu maamuzi yangu haya, maana sijisikii furaha kabisa katika ndoa hii. Na mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo kitutenganishe.
Kwani ulimpendea nini? Pesa au? Ndo madhara ya kumpendea mtu pesa bila kuchunguza tabia, matokeo yake unakurupuka kuolewa na punga
 
Ungekaa tu,usubiri magonjwa na mambo mengine yatokanayo na umalaya?Daah! hii ni hatari sana,hata mume akiwa anasemwa vibaya kwa ulevi wake wewe hutajali,aisee na akipata maradhi ujue pia urasemwa kua yawezekana nawewe ni malaya ndiyomaana umepatwa na magonjwa yatokanayo na zinaa,sasa kwanini usifanye jitihada za kujiepusha na yatokanayo na umalaya...?
Daaah!

,u
We unajali maneno ya watu au mume kupambania kulea familia? Samahani mkuu,hata ivo Binadamu hatulingani
 
Daah tangu naanza mahusiano sijawahi kufumania au kuonyeshewa kwamba mtu ana cheat na naomba Mungu isinitoke nikajua bora afanye kimyakimya Maana nahisi Kama inauma vile
 
Natamani kuvunja ndoa yangu.

Habari zenu wakuu, natumai mko poa. Nimekuja na nia ya dhati kutafuta ushauri kuhusu jambo langu ambalo linanitatiza.

Mimi ni msichana mwenye umri chini ya miaka 30. Nina mtoto mmoja wa kiume. Nimekuwa katika ndoa na mume wangu kwa takriban miaka miwili sasa.

Sababu za maamuzi yangu ni kama ifuatavyo:

1. Uchepukaji uliokithiri: Huyu mume wangu amekuwa akinihadaa sana. Sijawahi kuona kitu kilichoniumiza zaidi ya kugundua kuwa anatoka na wanawake wengine. Ameomba msamaha kila mara ninapomfumania, lakini bado anarudia tabia hiyo. Kesi zetu zimekuwa nyingi kwa wazazi na nadhani wamechoka kutusuluhisha.

2. Ulevi uliopitiliza: Mume wangu ni mlevi sana. Kurudi nyumbani asubuhi ni jambo la kawaida kwake. Nimeshazungumza naye na kumweleza jinsi ninavyojisikia kuhusu tabia yake ya kunywa kupindukia, ingawa anahudumia familia vizuri. Lakini, hupati muda na familia kabisa. Inanidhalilisha sana kwa sababu tunakaa na mdogo wake nyumbani, hivyo najihisi vibaya sana anaporudi asubuhi.

Ndoa yetu imefungwa kanisani na tumekuwa tukiishi pamoja kwa miaka miwili tu. Nashauriwa nifanye nini kuhusu maamuzi yangu haya, maana sijisikii furaha kabisa katika ndoa hii. Na mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo kitutenganishe.
Tupointi tuwili unataka ndoa ivunjike?
Kaa hapo bado cha moto hujakiona.
Ule wimbo wa "Huyooooooo ni chaguo lakoo, ni chaguo lako" kausikilize mara tatu.
 
Kuperuzi tu , Maana kutoka hataki Nitoke
Hufanyi kazi? Wewe ni mama wa nyumbani? Hataki utoke kwamba hata kujitoa tu mchana ukakaa sehemu ukaburudika nalo ni kosa? ( aisee una mwanaume wa ajabu )
By the way kana umeridhika kushinda nyumbani kama fridge basi learn new hobbies kuna kupika, jifunze kutengeneza mawigi uza online au decor za kutengeneza nyumbani. Huko kukaa bure ndo unakaa unamfikiria na dharau zinazidi. ACHA KUTAFUTA USULUHISHI KWA WATU WANAOWAFAHAMU, TUMIA AKILI KUSOLVE MATATIZO YENU, KAMA NYIE WAWILI HAMUWEZI KUPATA SULUHU HAMNA NDOA HAPO
 
Hakuna kosa la kuvunja ndoa kama ku cheat, tena huyo ni serial cheater, dada hata usijiulize mara mbili...
 
Wanaume hatujaisha "Kama amekuchoka atuachie sisi"
Pia wanawake hawajaisha!! Kama amemchoka akaachia jimbo wazi fasta kina dada watakaba nafasi hiyo!! Ndiyo hasara ya kukutania bar na kuanzisha mahusiano!! Siamini kama wakati wa uchumba jamaa alikuwa halewi!!
 
Natamani kuvunja ndoa yangu.

Habari zenu wakuu, natumai mko poa. Nimekuja na nia ya dhati kutafuta ushauri kuhusu jambo langu ambalo linanitatiza.

Mimi ni msichana mwenye umri chini ya miaka 30. Nina mtoto mmoja wa kiume. Nimekuwa katika ndoa na mume wangu kwa takriban miaka miwili sasa.

Sababu za maamuzi yangu ni kama ifuatavyo:

1. Uchepukaji uliokithiri: Huyu mume wangu amekuwa akinihadaa sana. Sijawahi kuona kitu kilichoniumiza zaidi ya kugundua kuwa anatoka na wanawake wengine. Ameomba msamaha kila mara ninapomfumania, lakini bado anarudia tabia hiyo. Kesi zetu zimekuwa nyingi kwa wazazi na nadhani wamechoka kutusuluhisha.

2. Ulevi uliopitiliza: Mume wangu ni mlevi sana. Kurudi nyumbani asubuhi ni jambo la kawaida kwake. Nimeshazungumza naye na kumweleza jinsi ninavyojisikia kuhusu tabia yake ya kunywa kupindukia, ingawa anahudumia familia vizuri. Lakini, hupati muda na familia kabisa. Inanidhalilisha sana kwa sababu tunakaa na mdogo wake nyumbani, hivyo najihisi vibaya sana anaporudi asubuhi.

Ndoa yetu imefungwa kanisani na tumekuwa tukiishi pamoja kwa miaka miwili tu. Nashauriwa nifanye nini kuhusu maamuzi yangu haya, maana sijisikii furaha kabisa katika ndoa hii. Na mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo kitutenganishe.
Samahani!! mtu umeolewa na kuishi na mwanaume miaka miwili bado unajiita msichana!! Wewe ni mwanamke wa miaka 30!! Ni vizuri ukajitambua!! Usichana ulishaisha zamani, lakini akilini bado unajiita msichana, hii itakufanya uchambuzi wako wa maisha ya unyumba kuwa wa kitoto sana!! Nikushauri: VUMILIA!! Msaidie hadi abadilike!! Wewe wa kwako naona yuko vizuri kama anawahudumia vizuri!! Kuna wenzio wanajihudumia wenyewe na bado wanavumilia!! Ukitoka tu kuna jirani yako atajiwahi fasta na anamjua kabisa ulevi wake!!
 
Tulia wewe, mwanaume akiingia kwenye ndoa ndio hupata zaidi vishawishi unakuta mke ndio ametoka uzazi amejiachia balaa hapo unaandika ila ukute umevaa mikanga tupu na minywele umeiachia tu.

Tulia nawe jikague vizuri, haiwezekani ndoa ya miaka miwili unaanza kulalamika mtu anakucheat. Mpe mambo jipake poda nukia oga osha mashuka, nyumba ing'ae acha kumsemesha upuuzi kila saa na acha kumkaguakagua simu yake na kumdadisi alikuwa wapi instead anza kumpa pole kwa kazi na kumwambia maneno mazuri.

Ongea nae mambo yanayokuudhi kwa upendo na upole na mfanye ajisikie aibu kwa anayoyafanya pia uasiache kumkumbusha viapo vyenu kanisani na usiache pia kumuombea kwa Mungu.

Pia ongea nae kwa upole kuhusu hisia zako kwake jinsi unavyompenda na namna anavyokuumiza kwa matendo yake. Mfahamishe kwamba wewe ni mwanadamu haupendi kujuta kuolewa nae na haupendi ifike pahala muachane au mvunje ndoa sababu ambazo anaweza kuzuia yeye mwanaume wako.

Tell him your feelings dewply kwa upole. Tafuta sehemu mtoe out na umwambie unataka kukaa nae faragha ya dinner. Mjadili bila yeye kunywa pombe ili aelewe maana akilewa atakuchukulia poa.

Jaribu kumuelezea namna ambavyo pombe inamzidi pia angalia kama inasababishwa na stress za kazi au nini? Ongea nae acha kukimbilia kutafuta ushauri mwingi maisha ni yako wewe.

Pambana ndoa sio Big Brother House. Fikiria mwanao je ataishi na wababa wangapi? Unamuacha huyu utakutana na malaika? Wanaume ndio sisi sisi tu hatuna tofauti sana we just sin differently.

Komaa na ndoa we tafuta jamaa akuliwaze kimyakimya huku unatunza ndoa kwa maana kuishi pamoja ili mtoto akue mazingira salama.
Umempa ushauri mzuri,
Ni yeye kuamua,,

Mda mwingine ya kilingeni na kibalazani ni ya kuyaacha hapohapo, ukibeba umeumia,

Ukikaa kilingeni kila jamaa anajifanya anachit,, mie mwenyewe nawalaghai na chit lakin kiukweli sichit kabisa,

Pia namwambia wife ukikaa kilingeni niseme vibaya, ili uonekane mpo kitu kimoja, ila yaache hapoahapo,

Elimu ya kitaa iache tu.
 
Ingekuwa ndio kinyume chake…. Mwanaume kaleta malalamiko mke anacheat na mlevi kupindukia nilitaka kuona majibu yenu wanaume ( na wanawake) wote mliosema Huyu dada abaki na hio ndoa…?!
Kuna watu humu (ke) watawahi kukaba nafasi kama wakijua ameshatoka kwenye ndoa! Watapeleleza hadi wampate!! Sikubaliani na ulevi wake, lakini nampongeza kwa kuhudumia vizuri familia yake pamoja na ulevi wake!!
 
Wanaume hatupendi kelele.
Huenda wewe una kelele sana na hiyo ndo sababu kuu ya ulevi wa mumeo na uchepukaji.

Cha kufanya we mwache kwa muda hata wa mwezi mmoja bila kumpigia kelele za uliwa wapi, kila siku nasema hili, we mwanaume mlevi sana, hujali familia, mbona wenzio hawako ivo nk nk.

Uwe busy na kazi au biashara yako, akiona umebadilika kazi itakua kwake sasa kuanza kufatilia kwanini hupigi kelele tena, au unachepuka akikuuliza ndo hapo mtakaa sawa.

Kelele, vikao na mshataka kwa wazazi haviwezi mbadilisha.
Hii kitu inakata stimu yakuishi na mwanamke ,kelele ndani ya ndoa hasa kwa wanawake kujidai ndio wenye haki sana nakutendewa mema wao tuu huathiri akili ya mwanaume ktk ndoa,jct imagine kila kukicha mwanmke anahitaji kutendewa mazuri yy tu,hajawahi kuwaza hata kukununulia kitu chochote kutokana namapato yake,hawazi kukutendea mambo yanayoweza kuimarisha mahusiano wala hafanyi jitihada zozote kujenga mahusiano bora bali yy anajiweka upande wa hakimu/wakili kukosoa utendaji wako ktk kuendesha familia,daima anakudai matumizi nakukupigia makelel hujatimiza hili mara hujakamilisha lile..daahh hayo yote nichanzo cha msongo wamawazo kwa mme hivyo kutafuta furaha ktk ulevi.
 
Sasa we mdada unalalamika weeee.

1. We mwenyewe hapo unachepuka. Bora yeye kashaliweka wazi. Na jichunguze kama wewe si chanzo cha yeye kuchepuka. Maana utendawizi wa siku hizi umewaharibu,utadhani nyie ndo mmeoa waume zenu. Pengine hujishughulishi kama inavotakiwa, kubali tu matokeo.

2. Kwamba analewa? Bado tatizo liko pale pale. Wanaume wengine wameamua wafunge ndoa na viti vya baa kwa sababu duniani kuna watu wanaboa. Hasa nyie viumbe. Kwa hiyo, umeyataka mwenyewe,kubali tu matokeo.

Ila,swali na mi moja. Wakati unakesha nae vichakani,getho kwake,au na yeye anakuja kwako, mnanyoana mavuzi, mbona hukuja hapa? Yamekukuta ya kukukuta umekuja kulia lia hapa. Tunatuma gari la kuchukua nguo chakavu,limeandikwa Toa nguo tunakuja
 
Back
Top Bottom