Baada ya kufuatilia uendaji wa chooni wa huyu dada muuza mgahawa, nimejiapiza sili tena migahawa ya uswahilini

Wahudumu wengi wa chakula huwa hawana tabia ya kumpa mteja sabuni ya kunawa mikono kabla ya kula, na ukitaka wakupe wengine wanakuona msumbufu, ila huwa wanaileta ukimaliza kula!
 
Ukimchunguza sana bata, hutokuja kumla kamwe.
Usafi sio bata, na bata akisafishwa hana shida. Wahadumu wa chakula wanapaswa kuanda chakula katika mazingira ya usafi, tuachane na mambo ya uswahili mwingi usio na tija.
 
Wahudumu wengi wa chakula huwa hawana tabia ya kumpa mteja sabuni ya kunawa mikono kabla ya kula, na ukitaka wakupe wengine wanakuona msumbufu, ila huwa wanaileta ukimaliza kula!
Wakati kunawa kwa sabuni kabla ya kula ni kwa usalama wako ila kunawa baada ya kula ni ustaarabu tu!

Ustaarabu unapewa kipaumbele kuzidi afya😀
 
Wakati kunawa kwa sabuni kabla ya kula ni kwa usalama wako ila kunawa baada ya kula ni ustaarabu tu!

Ustaarabu unapewa kipaumbele kuzidi afya
Ipo haja ya kuweka somo la usafi na afya ya binadamu kuanzia primary hadi chuo kikuu katika nchi hii.
 
Huyo ni msafi.

Umewahi kuona mkaanga au mchoma chapati wewe? Sema hapana, hapa kijiweni yupo, akimsafisha mtoto ni kwamba kazi inaendelea.

Mungu tu analinda walaji
Hawa wanawake wachoma chapati ndo funga kazi🙌, At least wale wanaume unakuta wanazichoma wakiwa wamesimama na wanavaaga kikazikazi na chapati zao huanzia 500+, Ila hawa wamama wa chapati za 250 hawa ni mziki kwenye suala la uchafu
 
Ipo haja ya kuweka somo la usafi na afya ya binadamu kuanzia primary hadi chuo kikuu katika nchi hii.
Sijui kama itasaidia sana! Labda kama ingewezekaba kuwekwa mkakati utakaoilazimisha kila familia kujenga tabia ya usafi, pengine ingesaidia.

Naamini usafi ni tabia ambayo mtu anapaswa kujengewa tokea akiwa mchanga.

Inashauriwa na wataalam, kwa mfano, mtoto tokea akiwa mchanga, kila anapojisaidia, akishafanyiwa usafi, anawishwe mikono kwa maji na sabuni. Afanyiwe hivyo pia kabla na baada ya kulishwa chakula.

Vitendo hivyo vitaishia kujikita kwenye kumbukumbu ya ndani na hivyo inakuwa kama vile ni tabia ya kuzaliwa nayo. Wengine wakikutana na mtu wa aina hiyo, watakuambia usafi upo kwenye damu, kumbe ni tabia aliyofundishwa tokea akiwa mchanga.
 
Hawa wanawake wachoma chapati ndo funga kazi🙌, At least wale wanaume unakuta wanazichoma wakiwa wamesimama na wanavaaga kikazikazi na chapati zao huanzia 500+, Ila hawa wamama wa chapati za 250 hawa ni mziki kwenye suala la uchafu
Kweli kabisa, anapokea pesa mkono huo huo na kushika chapati mkono huo huo, yaani ni kama hawaelewi kabisa.
 
Migahawa ya level ya kati hizi hand wash zikiisha wanajaza tena maji kwenye kile kichupa ndio maana unaona ni nyepesi. Maji yenyewe ya ndoo hayakufanyi ukanawa kabisa kabisa 100%. Bongo ni shida sana.
 
Mazoea! Kafanya hivyo tokea akiwa mtoto na hakuna aliyewahi kumwambia kuwa ni vibaya.

Wengine, hata ukisema uwaelekeze, wanaweza wakakuona una majivuno. Watakuambia wamekuwa wakifanya hivyo tokea zamani na haijawahi kuwaletea shida.

Sasa mtu kama huyo unafikiri itakuwa rahisi kumbadilisha?
 
Migahawa ya level ya kati hizi hand wash zikiisha wanajaza tena maji kwenye kile kichupa ndio maana unaona ni nyepesi. Maji yenyewe ya ndoo hayakufanyi ukanawa kabisa kabisa 100%. Bongo ni shida sana.
Kazi ipo.
 
Kuna mwaka mkuu wa mkoa wa lringa , kreluuu alifariki na kipindupindu, jiulize kwake vijakazi wangapi wa usafi, kwenye magonjwa kuomba mungu tu.
 
Nikiwa sina kazi leo nikaamua kujishughulisha kidogo kwa kufanya kautafiti kangu ka-usafi (afya) wa hivi vi-mgahawa vya hapa mitaani kwetu tunakopatia chai na lunch. Nikaona nishughulike na nyendo zao za chooni kwanza. Nimepitia migahawa minne na kote nimekutana na mambo yanayofanana kwa 100%. Nitasimulia cha mgahawa mmoja, kwa niaba ya mingine. Ikawa hivi;

Katoka chooni moja kwa moja hadi kwenye dishi lenye maji anayooshea vyombo na kutosa mkono wake wa kulia kujichuuzia maji kwa kutumia kiganja cha huo mkono wa kulia.......nilishangaa!

Kachukua sabuni ya unga ya kuoshea vyombo kwa mtindo wa kupamba (maana aliiweka tu katika chombo cha wazi (sahani) kwa kutumia mkono wake wa kushoto na kuendelea kujisuuzia maji na sasa akijihesabu ndo ananawa na sabuni.

Nikasema ngoja nifike na huko chooni kwenyewe kwanza nikaangalie mazingira. Nikaomba ruhusa kwamba naenda kujisaidia haja ndogo. Kwakuwa mi ni mzoefu wakaniruhusu......kufika huko Mungu wangu!!! Inye zinaonekana hovyo hovyo, uchafu mtupu.

Sili tena migahawani.

Kuna mugahawa mikubwa wanaweka kikombe kimoja cha maji ya maiti kwenye vyakula vyao kila siku, usile kabisa, kajipikie.
 
Mtu na akili timamu anategemea kweli elfu 2 itamoatia mlo? Serious???
 
Hakika hili ni janga,migahawani hadi mahotelini ni majanga,mamantilie ndio funga kazi uchafu kuanzia vyombo,vyakula hadi usafi wao binafs hasa wapemba ogopa sana migahawa ya wapemba.

Mahotelini wanajitajidi kwa usafi ila mnalishwa sana expired products pia na chakula kilicholala.

Kama una option achakula huko kale chakula cha kupikwa nyumbani kwako.
 
Kuna mwaka mkuu wa mkoa wa lringa , kreluuu alifariki na kipindupindu, jiulize kwake vijakazi wangapi wa usafi, kwenye magonjwa kuomba mungu tu.
Umesoma ulichoandika?
Kwa hiyo alivofariki huo mwaka
Baadae mwaka uliofuata akafufuka?

Halafu akauwawa tena na mwanamalundi?
Ebu weka sentence yako vzr
 
Nikiwa sina kazi leo nikaamua kujishughulisha kidogo kwa kufanya kautafiti kangu ka-usafi (afya) wa hivi vi-mgahawa vya hapa mitaani kwetu tunakopatia chai na lunch. Nikaona nishughulike na nyendo zao za chooni kwanza. Nimepitia migahawa minne na kote nimekutana na mambo yanayofanana kwa 100%. Nitasimulia cha mgahawa mmoja, kwa niaba ya mingine. Ikawa hivi;

Katoka chooni moja kwa moja hadi kwenye dishi lenye maji anayooshea vyombo na kutosa mkono wake wa kulia kujichuuzia maji kwa kutumia kiganja cha huo mkono wa kulia.......nilishangaa!

Kachukua sabuni ya unga ya kuoshea vyombo kwa mtindo wa kupamba (maana aliiweka tu katika chombo cha wazi (sahani) kwa kutumia mkono wake wa kushoto na kuendelea kujisuuzia maji na sasa akijihesabu ndo ananawa na sabuni.

Nikasema ngoja nifike na huko chooni kwenyewe kwanza nikaangalie mazingira. Nikaomba ruhusa kwamba naenda kujisaidia haja ndogo. Kwakuwa mi ni mzoefu wakaniruhusu......kufika huko Mungu wangu!!! Inye zinaonekana hovyo hovyo, uchafu mtupu.

Sili tena migahawani.
Bila kapicha haieleweki
 
Back
Top Bottom