Wenye wajibu wa kusimamia na kutoa elimu ya usafi sehemu za kula watimize wajibu wao

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,661
46,350
Kuna migahawa na Bar nyingi vyakula vinaandaliwa katika mazingira ya hovyo na uchafu sana kuanzia jikoni hadi kwa wahudumu. Unakuta wahudumu wenyewe ni wachafu sana pia.

Nimeshuhudia mtengeneza juice katika mgahawa anachokonoa masiko, anajishika miguu na kisha anahudumia watu kwa mikono hiyo hiyo bila hata kunawa.

Kuna sehemu za kuuza chakula nzi wamejaa kila mahali kama jalalani, watu wanakula na mkono mmoja huku mwingine ukiwa na kazi ya kufukuza nzia na wengine hadi wanafia kwenye vyakula.

Halafu kwa nini migahawa na bar nyingi hazina masinki ya kunawa mikono sehemu za kulia tofauti na ya chooni badala yake majagi yanayotumbukizwa kwenye maji machafu na masafi kunawashia watu ndio yamashika hatamu.
 
Jiko la kuchoma ktmoto pale erado pork pale area d dom limeshikana na ukuta wa toilet. Siku moja nilibahatika nikaingia mle jikoni chini nakutana na maganda ya ndizi yametapakaa plus wale funza weupe .Dah nilikataga tamaa sana kula hotelini.
 
Back
Top Bottom