Baada ya Januari 20 kupita, TCRA yasema itakuwa inazima laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kwa awamu

Mitambo yao inazidiwa watu wacheche hivi? Hizi system sijui hua wanamlipa nani awatengenezee, wana system zimetengenezwa na amateurs kabisa.
 
Ila nasikia TCRA wameona wawatafute wale wenye vitambulisho vya NIDA na hawajajisajili wawazimie line zao. Wasio na vitambulisho wataendelea kujidai. Sijui kama kama kuna ukweli.
Mi nimejisajili saa 2 zilizopita.
Me kitambulisho ninacho mda mrefu,sema uvivu tu wa kwenda kusajili. Ila this weekend ntaenda kusajili kama ntakua bado nmesalimika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema uzimaji wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole unafanyika kwa awamu kuanzia jana Jumatatu Januari 20, 2020 ili kuondoa usumbufu.

Amesema hadi jana saa nne usiku walikuwa wamezima laini 975,041.

Amesema kundi la kwanza waliozimiwa laini ni watu 656,091 ambao wana vitambulisho vya Taifa au namba lakini hawajasajili laini zao.

Kilaba amesema kundi la pili ni watu 318,950 waliosajili laini zao kwa kitambulisho cha Taifa kabla ya kuanza mfumo wa kusajili kwa alama za kidole.

“Hawa wote hawana sababu ya kutozimiwa laini zao leo, uzimaji huu hatutaki kumnyang’anya mtu laini yake ambayo ameizoea ila tutaisitisha kutoa na kupokea huduma. Hivyo simu yake itapokea ujumbe mfupi tu ambao utakuwa unamkumbusha usajili” amesema Kilaba akibainisha kuwa usajili wa laini za simu hauna kikomo.

Ameongeza, “tunazima kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, hauwezi ukazima laini milioni tano au 10 kwa mara moja.”

“Tunahitaji warudi, tukiwazimia tunategemea kesho watarudi kwenye foleni za kuhuisha laini zao kwa hiyo wakienda wengi zaidi hawatapata huduma kama ambavyo walijaa juzi na jana na leo mpaka mifumo ya Nida inaelemewa.”

Amesisitiza kuwa watafanya kistaarabu na kiufundi uzimaji laini ili mifumo isielemewe kwenye usajili.
Tunaikaliaga politiki.
 
Me kitambulisho ninacho mda mrefu,sema uvivu tu wa kwenda kusajili. Ila this weekend ntaenda kusajili kama ntakua bado nmesalimika

Sent using Jamii Forums mobile app
Cross your fingers for your safety
Hapa dar haichukui hata dakia 10 kama mtandao hausumbui.

Nahisi wanaozima line ni makampuni husika. Huenda Halotel wanatuvutia pumzi.
Ila ukijisajili unapokea 1GB kwa wiki:D:cool:
 
Mashine za kutusajilia zimetoka kwao wakizima ghafla bin vuu itakuaje.
Kuna suala la kiuchumi pia maana simcards hizi ndiyo zinafanya miamala mingi la kutuma, kulipa na kupokea fedha. Ni vizuri walivyochukua hatua kwa kuzima kwa zamu, ni namna bora ya kuwapa watu fursa ya kusajiri ili miamala iendelee kufanyika. Utashudia ripoti ya TRA mwezi huu kwa namna ambavyo makusanyo ya kodi yatavyopungua kwa asilimia fulani.
 
Back
Top Bottom