Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 304
- 518
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuruhusu mjadala wa ripoti ya CAG unaoendelea bungeni kuwa mjadala wa wazi, amesema uwazi huo utasaisia wezi wa pesa za miradi kuacha tabia hiyo
Kwa upande mwingine, Azim Dewji amewapongeza wabunge kwa kazi nzuri wanyofanya na ameshauri wabunge kuwasaidia mawaziri kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi mbalimbali katika majimbo yao ili fedha zisipotee kwani kwa kufanya hivyo hawatakuwa na kazi kubwa ya kuomba ridhaa kwa wananchi kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025
Sambamba na hayo, Mzee Azim Dewji amewashauri wabunge kutunga sheria kali kama vile kutowapa dhamana watakaobainika kuchezea pesa za miradi ili wapate hofu ya kutumia vibaya fedha za miradi ambazo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa amepambana kuzitafuta ili wananchi wanufaike kwa kutatuliwa matatizo yao