Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 481
Hujui tu maji hutiririka toka kichwani kuja miguuni! Tusubiri sisi huku miguuni matone yatatufikia! Labda tuwe wajanja kuanza kunawa miguu kabla hatujalazimishwa kuoga!
Mkuu mbona unakuwa na Myopia kiasi hicho?, Shughuli inafanywa na UN hii na kati ya walipiga kura ya kuidhinisha ni Nigeria, South Africa, Gabon. Hawa wao wanatekeleza kazi waliyotumwa tu.
Unajua ukiangalia sana wanaolaani kichapo hiki ni viongozi wa Afrika waliotaka kuset precedence baada ya Gaddafi kuendelea kutawala kwa kuua raia wasio na hatia na kuitumia wao kama mfano kuwatishia wananchi wa nchi zao ili waendelee kuwatawala kwa nguvu. Kichapo hiki kinatoa somo kwa wenye mawazo kama Gaddafi na Tanzania tukiwemo kuwa dola haiwezi kuwa ndiyo source of power bali ni wananchi kwa ridhaa yao. Pia inaongeza ujasiri kwa wale watakao taka kupinga serikali za kidikteta kuwa theya are not alone, hata kama watauwawa sheria itachukua mkondo wake.
Ule wakati wa kuua wananchi kama ilivyotokea Pemba 2001, Mwembechai 1998 na Arusha 2011 na hakuna accountability yoyote sasa unatakiwa kukoma. Ninaamini kabisa kuwa watawala wa Afrika wanaong'ang'ania madaraka kwa kuchakachua hii attack ya Libya itawatisha sana na kuwatia kiwewe.
Africa kunatendeka nini?
Leo vikosi vya ushirika vimefanya mashambulizi na kuua raia wengi,uvamizi huu ni katika kile kinachodaiwa kuwalinda raia walibya..
Haiwezekani kuua rai eti ili kuwalinda,ni kweli Ghadafi amekaa madarakani muda mrefu,na ameua rai,lakini sikubaliani na hatua yoyote ya matumizi ya nguvu kumwondoa Madrakani.
Azimio la kuivamia libya ni batili,hakuna nchi yenye kura ya turufu kwa nchi nyingine
natoa wito kwa Africa kuungana na kupinga uvamizi huu wa kijeshi

mkuu nimekugongea thanks,
kwanini nguvu hiyo hiyo isitumike kumng'oa gbagbo, kule ivory coast? Au issue hapa ni mafuta?
Mkuu mbona unakuwa na Myopia kiasi hicho?, Shughuli inafanywa na UN hii na kati ya walipiga kura ya kuidhinisha ni Nigeria, South Africa, Gabon. Hawa wao wanatekeleza kazi waliyotumwa tu.
Unajua ukiangalia sana wanaolaani kichapo hiki ni viongozi wa Afrika waliotaka kuset precedence baada ya Gaddafi kuendelea kutawala kwa kuua raia wasio na hatia na kuitumia wao kama mfano kuwatishia wananchi wa nchi zao ili waendelee kuwatawala kwa nguvu. Kichapo hiki kinatoa somo kwa wenye mawazo kama Gaddafi na Tanzania tukiwemo kuwa dola haiwezi kuwa ndiyo source of power bali ni wananchi kwa ridhaa yao. Pia inaongeza ujasiri kwa wale watakao taka kupinga serikali za kidikteta kuwa theya are not alone, hata kama watauwawa sheria itachukua mkondo wake.
Ule wakati wa kuua wananchi kama ilivyotokea Pemba 2001, Mwembechai 1998 na Arusha 2011 na hakuna accountability yoyote sasa unatakiwa kukoma. Ninaamini kabisa kuwa watawala wa Afrika wanaong'ang'ania madaraka kwa kuchakachua hii attack ya Libya itawatisha sana na kuwatia kiwewe.
Unajua Gadafi keshaua watu wangapi hadi sasa, umeyaona madege yake yanavyoshambulia raia wanaoitwa waasi. Wenye nyumba wameamua kumuondoa mpangaji, wacha wasaidiwe
Naamini wengi wenu mnafuata upepo baada ya kulishwa propaganda ya magharibi,haiwezekani kuua raia eti kumtoa ghadafi,alafu nyie mnashabikia bila kujua adui namba moja wa dunia leo ni hizo nchi za magharibi,laiti kama mngekuwa mmefika libya muelewe ukweli na si kushabikia uvamizi,je ni njia ya kijeshi tu ndio sahihi?naamini wangetumia njia ya kidplomasia kuliko matumizi ya nguvu kama haya,,wanaoumia zaidi ni raia wa libya,na baada ya vita hii wataendelea kuteseka kama ilivyo iraq,,historia itawahukumu wote mnaoshabikia leo...nalaani uvamizi huu...
Je kitendo cha mataifa ya magharibi kumvamia kijeshi ni sahihi?hoja yangu ni kwamba uvamizi huu utaleta maafa zaidi kuliko tija,bado dunia inawez kutumia njia za amani na kidplomasia kumwondoa Ghadafi...ila hawataki kutumia diplomasia ili waweze kupora mafuta na kuharibu miundombinu ili wachukue hizo kandarasi