Attention Bodi Ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu Kwa Wanafuzi(HESLB)

Hapa nadhani kuna shida, Sheria ya PCB iliyo pitishwa juzi kuwa wabana viongozi watakao shindwa kuzitolea ufafanuzi mali walizo jilimbikizia, inaanza tu July mwaka huu!(Majibu ya Hosea akihojiwa na BBC juzi)

Iweje hii sheria ya kurudisha mikopo, nayo imepitishwa july mwaka huu yenyewe ihusishe miaka ya huko nyuma?

Wana sheria nisaidieni!
 
Waache ujinga,kwanini wamfunge mtu ambaye ameshindwa kulipa kwa sababu ya ukosefu wa kazi?Vitu vyote viwe synchronized.Mbali na kutoa mikopo serikali itengeneze mazingira ya watu wanaograduate wapate kazi.Wasituletee za kuleta,wawafunge hao wanaoiba pesa zisizokuwa zao wamejaa serikalini.Kuwafunga vijana wanaomaliza hakutaondoa matatizo yenu ya wizi na ujambazi wa mali zetu
 
Migongano ya Bodi ya Mikopo, wanafunzi yaibuka upya

na Schola Athanas na Mobini Sarya
Tanzania daima

SAKATA la wanafunzi wa elimu ya juu wanaodai mikopo yao limeibuka upya kufuatia hatua ya wanachuo hao kukusanyika katika ofisi ya Bodi ya Mikopo jana na kuanza kuimba wakishinikiza wapewe mikopo yao.
Baada ya viongozi wa bodi hiyo kuona wanafunzi hao wakiwa wanaimba kwa ghadhabu na hasira, walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambao walifika katika eneo hilo kwa lengo la kuhakikisha hali ya usalama.

Baada ya kufika kwa askari hao, wanafunzi hao walitulia na kukaa kimya wakisubiri hatima yao.

Wanachuo hao waliwaambia waandishi wa habari kuwa waliamua kukusanyika ofisini hapo kutokana na kuchoka kusubiri fedha zao za mkopo, ambazo walianza kufuatilia toka Septemba mwaka jana bila mafanikio yoyote.

"Inasikitisha kuona bodi hii haitujali kwani tumeanza kufuatilia fedha hizi tangu Septemba mwaka jana huku tukipewa majibu yasiyokuwa na utekelezaji," alisema mwachuo mmoja ambaye hakutaja jina lake.

Baadhi yao walisema kuwa wametokea mikoani kuja kudai fedha hizo.

Malalamiko ya wanafunzi dhidi ya bodi hiyo, sasa limekuwa ni jambo la kawaida.

Wakati hayo yakitokea, wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jana nao walitangaza mgomo baridi wa kutokuingia darasani, wakishinikiza Bodi ya Wakurugenzi wa chuo hicho itekeleze madai yao, ikiwemo kuchunguzwa kwa tuhuma ya kuliwa kwa fedha za mikopo ya wanafunzi.

Wakizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo, viongozi wa Serikali ya Wanafunzi (COBESO), walisema kuwa wanataka waelezwe fedha hizo zimekwenda wapi.

Fedha zinazodaiwa kuliwa ni zile zilizolipwa mara mbili na wanafunzi ambao baada kujilipia kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, walipata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Pia wanataka mamlaka zinazohusika kuajiri mkuu wa chuo ili kuondokana na tabia ya kukaimu nafasi hiyo wakidai kuwa mkuu wa chuo aliyepo sasa amekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wa miezi tisa sasa.

Walisema hali hiyo inasababisha matatizo kama lililoibuka hivi majuzi ambapo wanafunzi wapatao 300 waliokuwa wamesajiliwa kwa kozi ya diploma ya mwaka mmoja lakini sasa wanaambiwa wanatakiwa kusoma ngazi ya cheti.

Madai mengine wanayotaka yatekezwe wanasema chuo hakina daftari la muongozo wa wanafunzi (prospectus).

Akifafanua, Makamu Rais wa COBESO, Shomari Shomari, alisema kuwa mwaka 2004 na 2005, ada za wanafunzi 200 waliokuwa wanalipiwa na Bodi ya Mikopo pamoja na wizara ziliyeyuka.

Mwaka 2005 na 2006 zaidi ya wanafunzi 100 hawajui ada zao kutoka Bodi ya Mikopo zilichulikuwa na nani, pia wanafunzi wa mwaka 2006 na 2007 zaidi ya 80 wamekuwa wakichukua pesa ya stationeries tu lakini ya ada hawajui inaliwa na nani.

"Tumetangaza mgomo, hatuingii darasani hadi hapo watakapotueleza kama madai yetu yanatekelezwa… wale wanafunzi waliodangwanywa kuwa watasoma diploma kwa mwaka mmoja na sasa tayari wamekwisha soma wiki tatu, hatima yao ni nini?" alihoji Shomari.

Hata hivyo, Tanzania Daima ilipomfuata Kaimu Mkuu wa Chuo, Athuman Ahmed, alisema hawezi kuongea na mwenye mamlaka ya kulizungumzia suala hilo ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya chuo, Dk. Stergomena Bamwenda.

Hata hivyo, alipofuatwa ofisini kwake, Bamwenda hakupatikana na ofisa habari wa wizara hiyo alimtaka mwandishi kuacha maswali.
 
wakati mwingine hivi vitu ni kama ndoto tuu.....hili tatizo ni simu moja tuu toka Ikulu au PM office kwenda hapo Elimu ya juu,unaweza kukuta hela zipo ila hawajui cha kufanya maana kuna list fake kibao za wajanja sasa hawajui wa kumpa nani na kumnyima nani,kumbe maskini ni kutengeneza just simple software ambayo ingemaliza hili tatizo forever
 
nani kasema hela hakuna kule, ni uongozi wa kizembe wa Prof. Msolla.. how can a person be so incompetent and still being rewarded for his mediocrity?
 
Nimeona hili tamko japokuwa liko nyuma sana lakini nikaona labda niliweke hapa mpate kusema lolote .

RAIS AINGILIE KATI TATIZO LA MIKOPO WA ELIMU YA JUU
ARUSHA
• Vijana wa CHADEMA waitika mwito wa Rais Kikwete,
kuwakusanya wanasiasa na wasomi kujadili sheria ya
madini na ufisadi nchini
• Taarifa ya Kongamano lao la Wanavyuo zaidi ya 2000
kutolewa wiki ijayo

Kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA inamuomba Rais Kikwete
kuingilia kati matatizo ya mikopo kwa takribani
wanafunzi mia tatu(300) wa Chuo cha Uhasibu
Arusha(IAA). Wanafunzi hao wako kwenye uwezekano
mkubwa wa kushindwa kuendelea na masomo na baadhi yao
wamesharejea nyumbani baada ya kujulishwa kwamba Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) haitawapatia mikopo
ya kuwadhamini masomo yao.

Wanafunzi wa fani mbalimbali zikiwemo biashara, benki,
uhasibu, ugavi, kodi na fedha wengi wao wakiwa ni
wasichana waliopata daraja la tatu wamefika chuoni
hapo baada ya kuomba na kutimiza vigezo vya kudahiliwa
kujiunga na chuo hicho(admission criteria), na baada
ya kupata udahili(admission) waliwasilisha maombi yao
Bodi ya Mikopo na wakakubaliwa kupata
udhamini(sponsorship) kwa viwango mbalimbali kwa
kadiri ya mahitaji yao.

Tangazo la kustahili kwao kupewa mikopo lilitolewa na
bodi katika tovuti yake ya www.heslb.go.tz tarehe 11
mwezi Septemba mwaka 2007 wiki chache baada ya
kumalizika kwa kikao cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.

“Inasikitisha kwamba hawa waliwasilisha maombi bodi ya
mikopo baada ya kupata udahili(admission) kwa maana
nyingine bodi ilikuwa inajua kabisa ni fani zipi
wanakwenda kusomea. Bodi ikawakubalia na kutangaza
majina yao na viwango vya mikopo wanavyostahili
kupata. Mpaka hivi leo tarehe 7 Novemba 2007 majina
yao bado yapo kwenye tovuti ya bodi ya mikopo katika
kundi la wanaostahili kupewa mikopo. Inasikitisha
kwamba mpaka sasa hawajapewa mikopo yao. Na tayari
viongozi wao wa wanafunzi wamewaeleza kwamba bodi
imewajulisha kuwa hawastahili kupewa hata shilingi
moja. Kinachoshangaza zaidi ni kwanini bodi inaacha
kutoa tangazo la kubatilisha tangazo lake la awali
badala yake maofisa wabodi wanawadokeza tu viongozi wa
wanafunzi wawaambie wenzao. Ni vyema taarifa rasmi
ikatolewa na bodi yenyewe moja kwa mojan kufafanua
suala hili”.

Tangazo hilo la bodi ambalo liko sehemu ya ‘habari
mpya’(current news) limetaja daraja za viwango vya
mkopo mbele ya kila jina la mwanafunzi katika orodha
hiyo ya wanaostahili kupata mikopo- alama zilizowekwa
ni pamoja na A(100%), B(80%), C(60%), D(40%), E(20%)
na F(0%). Kutokana na tangazo hili la bodi vijana hawa
wengi wakiwa wanatoka familia masikini walifunga
safari toka majumbani mwao na kuja kuanza masomo kwa
matarajio ya kupata mikopo kama ambavyo bodi
imetangaza.

“Nimekutana na baadhi ya wanafunzi hao hapa Arusha,
hali yao ya kifedha wengine ni mbaya sana. Wengi wako
darasani lakini wanashindwa kusoma kutokana na kuhofia
hatma yao, huku ni kuwapa msongo na matatizo ya
kisaikolojia wanafunzi na hatimaye kuathiri maendeleo
yao chuoni. Baadhi wanataka kurudi majumbani kwao
lakini hata nauli hawana. Hali inakuwa ya hatari zaidi
kwa wanafunzi wa kike. Hii ni kama vile wametelekezwa.
Tangazo toka kwa taasisi ya serikali kama bodi ya
mikopo ni sawa na mkataba wa maneno kati ya serikali
na mwananchi. Utamaduni kama huu ukiendelea utawafanya
wananchi wasiwe wanaamini matangazo ya serikali yao.
Na tukifikia hapo kasi ya maendeleo itakuwa mashakani.
Ndio maana katika hatua hii tunamuomba Rais aiingilie
kati kunusuru maisha ya vijana hawa wakitanzania”.

Itakumbukwa kwamba Rais Kikwete aliwahi kufanya
mkutano na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar es salaam
kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya CCM tarehe 3
Februari 2007 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo
(baada ya kusikiliza risala ya wanafunzi) aliahidi
(kama mwenyekiti wa chama tawala) kwamba atawasiliana
na chama chake kutafuta ufumbuzi wa suala hili na
kwamba taarifa zingetolewa baada ya mwezi mmoja kuhusu
hatua ambayo ingefikiwa. Pia akasisitiza kwa namna ya
pekee kwamba hakuna mwanafunzi atayeshindwa kuendelea
na masomo kwa kushindwa kuchangia gharama za elimu ya
juu.

“Ahadi hii ya Rais ilikuwa ni mwanzo wa mwaka. Leo
tunaelekea ukingoni mwa mwaka matatizo ya mikopo ya
elimu ya juu bado yapo katika vyuo karibu vyote
nchini. Ni vyema Rais akaagiza watendaji wake
kumweleza hali halisi, mpaka leo kuna wanafunzi wa
vyuo mbalimbali ambao hawajapata mikopo hata wale
waliopata daraja la kwanza na la pili. Inafurahisha
kwamba wiki hii Rais Kikwete amerudia tena ahadi yake
ya mwezi Februari, amenukuliwa na vyombo mbalimbali
vya habari (7 Novemba 2007) wakati akiwapokea baadhi
ya wanavyuo ambao wamejiunga na CCM akiwa Dodoma
kwamba atakaa na Waziri wa Elimu ya Juu- Prof. Msolla
kuwasaidia wanafunzi ambao hawajapata mikopo. Ndio
maana tunaomba katika kufanya hivyo awape kipaumbele
wanafunzi hawa wa Arusha ambao wako wengi na wengine
hali yao ya kimaisha ni mbaya”

Matatizo haya ya mikopo ya wanafunzi yamekuwa
yajirudia rudia kila wakati. Wakati wa utawala wa
awamu ya kwanza wa Hayati Nyerere hakukuwa na mfumo wa
mikopo ya elimu ya juu, serikali ilidhamini wanafunzi
wote kwa asilimia mia moja. Hata wakati wa utawala wa
awamu ya tatu wa Rais Mkapa pamoja na kuwa serikali
ilikuwa inatekeleza sera ya uchangiaji wa elimu ya juu
wanafunzi walikuwa wanapewa mikopo katika mahitaji
makuu kwa asilimia mia moja. Leo katika utawala wa
kipindi cha nne cha Rais Kikwete mikopo inatolewa kwa
asilimia ndogo na kiasi kinachobaki mwanafunzi
anapaswa ajigharamie mwenyewe na hata hicho kiwango
cha mkopo ambacho mwanafunzi amepangiwa kupata bado
kuna wengi hawajakipata kama hao wanafunzi takribani
300 wa Chuo Cha Uhasibu Arusha(IAA).

Hivyo, kama taifa bila kujali itikadi tunapaswa
kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu mfumo wetu wa
gharama za elimu hususani elimu ya juu. Na katika
kufanya hivyo hakuna njia ya mkato zaidi ya kuwekeza
katika elimu na kufanya elimu ya ngazi zote ikiwemo ya
vyuo vikuu kuwa kipaumbele mama cha serikali kwa
vitendo. Na ili tuweze kufikia huko ni lazima tuepuke
ufisadi, matumizi makubwa ya serikali na kuhakikisha
taifa linanufaika na rasilimali ambazo mwenyezi Mungu
amejalia Taifa letu.

Kama sehemu ya kutekeleza azma hii Kurugenzi ya Vijana
CHADEMA inaandaa Kongamano kubwa litakalofanyika
Mkoani Dar es salaam litakalojumuisha vijana hususani
wasomi zaidi ya elfu (2000) kujadili kuhusu Ufisadi na
Hatma ya Rasilimali za Taifa. Kongamano hili
limepangwa kufanyika Novemba 17 mwaka 2007 kama sehemu
ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanafunzi.
Wasomi mbalimbali wamealikwa kutoa mada katika
kongamano hili, pia wanasiasa mbalimbali wamealikwa
wakiwemo wabunge Zitto Kabwe na Dr Wilbroad Slaa.

“ Leo naondoka Arusha kurudi Dar es salaam kujua
maandalizi yalipofikia. Lakini nimeshatoa maelekezo
kwa Afisa Habari wetu David Kafulila na Afisa
Mwandamizi wa Vijana Taifa- Regia Mtema kuitisha
mkutano na waandishi wa habari mapema wiki ijayo ili
tutoe taarifa ya kina kuhusu watoa mada ni wakina
nani, mada ni zipi na Kongamano lenyewe litafanyika
katika ukumbi gani. ”

Hili ni tukio ambalo lilikuwa ndani ya Mpango wa Mwaka
wa Kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA lakini imebidi mambo
kadhaa yaongezwe kutokana na matukio mbalimbali ya
kisiasa yaliyotokea hapa nchini hivi karibuni.

“Baada ya Rais Kikwete kuahidi kuwashirikisha wasomi
na wapinzani katika Kamati ya Kupitia madini imebidi
tubadili kidogo ratiba ya Kongamano letu. Tumeona
tuweke mjadala pia kuhusu sheria ya madini. Lengo ni
kupata hoja mbadala ambazo tutaziwasilisha katika
kamati hiyo inayotarajiwa kuongezewa wajumbe. Sisi
tunaamini wasomi na wanasiasa hususani katika upinzani
wenye maono kuhusu rasilimali za nchi hii wapo,
kinachokosekana ni dhamira ya kisiasa ya
kuwashirikisha na kuzingatia maoni yao. Kwa kuwa Rais
Kikwete ameahidi, sisi vijana wa CHADEMA tumeona
tutimize wajibu wetu kwa kuwaleta pamoja wanasiasa na
wasomi hususani vijana kujadili suala hili. Tunapenda
vitendo zaidi ya maneno, tunaamini serikali itachukua
hatua ”.

Kongamano hili litadhaminiwa na vijana wenyewe(wale
wenye uwezo) kupitia michango yao midogo midogo
itayowezesha kutolewa kwa nyaraka mbalimbali za
mkutano, viburudisho na usafiri kwa washiriki. Katika
mkutano huo washiriki watapewa nyaraka mbalimbali
ikiwemo uchambuzi wa Mkataba wa Richmond, Buzwagi,
Orodha ya Mafisadi(list of shame), Sheria ya Madini na
nyaraka zinginezo.

“ CHADEMA ni chama kinachopokea ruzuku ndogo toka
serikalini, na wala hatuna vyanzo visivyoeleweka wa
mapato yetu. Tukio la halaiki kubwa kama hii
linahitaji nguvu ya kila mmoja wetu mpenda demokrasia
na maendeleo. Linahitaji nguvu ya kila anayekerwa na
ufisadi na anayetaka kutetea rasilimali za taifa hili.
Tumeambiwa wenzetu waliwaita wawakilishi ishirini(20)
wa wanafunzi wenzao elfu moja(1000) na kuwapa takrima
ya shilingi elfu hamsini(50,000) kila mmoja ili kwenda
Dodoma kupokea kadi za chama kwa niaba ya wenzao. Sisi
tunataka vijana wasomi wenye uwezo watambue wajibu wao
katika jamii na kukutana kujadili mustakabali wa Taifa
letu hata kama ikiwa ni kwa kuingia gharama wenyewe
kwa niaba ya watanzania wengine masikini. Kama Mwalimu
Nyerere alivyowahi kuasa, vijana wasomi ni kama mtu
aliyetumwa na kijiji kwenda kutafuta chakula kwa niaba
ya wengine walioko kwenye njaa, kijana msomi
akishindwa kukumbuka alipotoka ni usaliti”.

Kurugenzi ya Vijana inaamini kwamba matatizo ya mikopo
na ukosefu wa ajira ni matokeo tu ya udhaifu katika
mifumo yetu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hivyo
mkazo unapaswa kuwekwa katika kukabiliana na vyanzo
badala ya kushughulikia matokeo katika mtindo wa
zimamoto. Tukiweza kupunguza ufisadi ni wazi tutaweza
kupata fedha za kusomesha wanafunzi wote bila kuweka
madaraja, na tukiweza kutumia vizuri rasilimali za
taifa ikiwemo madini ni wazi mazingira ya vijana wengi
kupata ajira yatakuwepo katika Taifa letu.

“ Leo vijana wasomi wanaahidiwa ukuu wa wilaya,
wakumbuke kuwa kuna mamia tu ya nafasi hizo na sehemu
kubwa zikishikiliwa na wazee. Lakini maelfu ya
wanavyuo wanahitimu katika vyuo vikuu kila mwaka. Na
kwa ujumla zaidi ya watanzania laki saba(700,000)
wanaingia katika soko la ajira kila mwaka huku ahadi
ya serikali ikiwa ni ajira milioni moja tu mpaka 2010
ambayo ni sawa na ajira laki mbili(200,000) kwa mwaka.
Vijana wasomi wanapaswa kujiuliza, hawa laki tano na
zaidi wanakwenda wapi kufanya nini? Ndio maana katika
kuadhimisha Siku ya Wanafunzi Duniani kurugenzi ya
Vijana wa CHADEMA tumeamua kuwakutanisha Vijana wote
bila kujali itikadi katika Kongamano kuhusu Ufisadi na
Hatma ya Rasilimali zetu.”

Imetolewa 7 Novemba 2007 na:

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa
Mnyika@yahoo.com
0754694553
 
Ndio maana nasema vijana wasomi ambao wanaona kweli kuna ukandamizaji nchini na wanaona kuna haja ya mabadiliko ya lazima wawasiliane nami kwa mail novella2rhyme@yahoo.com.
Tunhahitaji mabadiliko ya laziama ikiwa ni pamoja na kutetea haki zetu kwanza sisi kama vijana wasomi.Tuanzie na hili.

Mungu Ibariki Tanzania
 
me hofu yangu kama kawa...wale viongozi wa wanafunzi wa juu wajiandae kusimamishwa masomo soon...if hawana kadi za ccm
 
Imetolewa 7 Novemba 2007 na:

Wewe,

Ndio nini tamko la Novemba 7 kutuwekea leo Novemba 11?

Heh, kumbe siku ile ile magazeti yalivyoandika Kikwete awapokea Vijana Dodoma kumbe ni siku hiyo hiyo Arusha vijana walilalamikia mikopo!Sasa handsome wetu ilijisifu nini kuwa ametatua matatizo ya mikopo?

Halafu kumbe CHADEMA walitangaza Novemba 7 kuwa ikifika Novemba 17 wataadhimisha siku ya Wanafunzi Duniani kwa kuandaa Kongamano. Msekwa alipotoa tamko lake Novemba 9 kuwa nao wanaandaa Kongamano inaamaana CCM waliamua kuwaiga au kuwafunika CHADEMA?

Nimewa-miss, eti WoRM yuko wapi?

Asha
 
Shadrack Sagati
HabariLeo; Tuesday,November 13, 2007 @00:02

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu, imesema licha ya kuwafanyia wanafunzi wote waliomba mikopo uchambuzi wa uwezo wa uchumi na kueleza kiasi cha asilimia wanayotakiwa kukopeshwa, lakini baadhi yao hawana sifa za kupewa mikopo hiyo.

Imetoa tamko hilo kutokana na wanafunzi ambao majina yao yalitoka kwenye tovuti kuitaka bodi hiyo iwape mikopo wakidai tayari wamefanyiwa uchambuzi wa uwezo wa uchumi na majina yao kuwekewa kiwango wanachostahili kukopeshwa. Hata hivyo hakutaja idadi ya wanafunzi ambao walifanyiwa tathmini ya uchumi lakini pia wakakutwa hawana sifa za kukopeshwa kwa kile alichoeleza kuwa kwa sasa itakuwa ni vigumu kujua idadi yao hadi hapo vyuo vyote vitakapofunguliwa na wanafunzi wote kukopeshwa.

“Naamini baada ya vyuo vyote kufungua tutakuwa kwenye nafasi ya kueleza idadi ya wanafunzi ambao waliomba mikopo, lakini hawakuwa na sifa,” alisema Mwaisobwa. Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu ya Arusha ni miongoni mwa waathirika ambao walifanyiwa kipimo hicho, lakini wameelezwa na bodi hiyo kuwa wengi wao hawana sifa za kupewa mikopo hiyo, hali iliyowafanya wanafunzi hao kuandamana.

“Nimezungumza nao kwa simu, lakini hawakutaka kunielewa. Lakini ukweli ni kwamba siyo wote ambao walifanyiwa ile tathmini ya uwezo wa uchumi kuwa wote wanastahili kupewa,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, Dar es Salaam jana.

Alisema tathmini hiyo ilifanywa kwa wanafunzi wote walioomba, lakini wakati wa kutoa mkopo walipeleka kila chuo kwa kuzingatia kwanza vigezo vilivyotangazwa na bodi. Moja ya vigezo hivyo ni kupata alama isiwe chini ya daraja la pili katika mtihani wa kidato cha sita na awe raia wa Tanzania. Alisema wanafunzi wengi ambao hawajapewa mkopo ambao wanalalamika ni wale waliomba mkopo wakati wako daraja la tatu.

“Ndiyo hao tuliowafanyia tathmini ya uwezo wa uchumi lakini kwenye mkopo hawana sifa za kupata,” alisema Mwaisobwa ambaye alikiri kuwa kuwekwa majina ya waombaji hao kwenye tovuti kumesababisha wanafunzi wengi kupatwa na usumbufu huo.

Alisema bodi yake imekuwa inapokea malalamiko mengi kutoka kwa wanafunzi mbalimbali ambao walifanyiwa tathmini hiyo. Wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha jana waliondoka mjini Arusha kwenda Dar es Salaam kuwasilisha malalamiko yao.

“Hao wa Arusha tumesikia na tumezungumza nao, hawana mpya maana wana daraja la tatu, nani atawapa mkopo. Waache waje labda wanakuja kutembea,” alisema Mwaisobwa na kusisitiza kuwa aliwafafanulia kila jambo kwenye simu lakini hawataki kuelewa.

Hadi Novemba 7 mwaka huu, Bodi ya Mikopo ilishatoa mikopo ya Sh bilioni 8.3 kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza fedha ambazo ni kwa ajili ya chakula, malazi na vitabu, na Sh bilioni 26.5 kwa wanafunzi wengine wanaoendelea kwa ajili ya chakula, malazi na vitabu.

Alisema bodi hiyo itaendelea kutoa fedha nyingine kwa kadri ambavyo watahitaji wanafunzi hao kama walivyojaza mkataba na bodi hiyo. Pia alisema bodi inaendelea na mchakato wa kulipa ada za wanafunzi hao kwa vyuo husika.

My Take:

This is a classic example of people intoxicated by the trappings of absolutely power! Ningemtimua huyo bwana kazi leo leo..
 
Ngoja kwanza mambo yakae sawa maanake sijui kwa wanafunzi wa nje hiyo bodi imetumia sheria gani katika kuallocate mikopo kwa wanafunzi hao kwani mfumo na hali ya maisha kwenye nchi hizo zinatofautiana.Ikumbukwe wapo wanafunzi 100 ktk kila nchi especially hizo tatu za kwanza Russia,China,India,SA,Algeria,Uganda nk.
 
Waache ujinga,kwanini wamfunge mtu ambaye ameshindwa kulipa kwa sababu ya ukosefu wa kazi?Vitu vyote viwe synchronized.Mbali na kutoa mikopo serikali itengeneze mazingira ya watu wanaograduate wapate kazi.Wasituletee za kuleta,wawafunge hao wanaoiba pesa zisizokuwa zao wamejaa serikalini.Kuwafunga vijana wanaomaliza hakutaondoa matatizo yenu ya wizi na ujambazi wa mali zetu

Yaandaliwe mazingira ya kurejesha mikoo kwa wahitimu wapya. Bila ajira itakuwa ngumu kui-enforce malipo ya mikopo hii. Kwa wale ambao wako ajira binafsi kuna utaratibu gani wa kuwafanya warejeshe mikopo?
 
Kitisho cha kuwafunga wahitimu wa Chuo kikuu ktaendelea kuwahamisha wasomi kwenda ng'ambo. Ni juzi tu wizara ya afya imesema zaidi ya madaktari 340 wanafanya kazi katika nchi zilikozo kusinin mwa africa kama Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini. Muswada huu umechoka kabla ya kupitishwa. Hivi ni nani aliyeturoga sisi watanzania?

Bodi ya Mikopo ijibu kwanza Tuhuma/Hoja Nzito za Mwkjj, kabla ya kukimbilia kuwatishia watz-wasomi. Warudishe kwanza "FEDHA" walizotumbua kupitia "SERA" isiyo na mashiko, ya kibaguzi na yenye kuendekeza "UFISADI".

WITO WANGU KWA WATANZANIA NI KUWA WAKATI UMEFIKA TUKATAE KUDANGANYWA KAMA WATU TUSIOFIKIRI, KUONA AU KUSIKIA.
 
Itakuwa ni zawadi kubwa ya Krismasi na mwaka mpya kwa maelfu ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini. ! Dear Santa, I have not asked for anything lately but just this time please!!!
 
mkuu hebu weka wazi na fafanua, sioni kitu, hii no romours au tayari imeshavunjwa. maana ww nawe kwa ......
 
Back
Top Bottom