Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Mheshimiwa Mpaka kieleweke ni kweli kwamba kuna tatizo kubwa huko kwenye Uongozi wa Juu ATCL,Na Mimi kwa bahati mbaya nilikuwa mmoja wa watu waliokumbwa na Adhma ya kukosa Usafiri kwa karibu masaa 6 kutoka Dar kwenda Arusha,hali iliyonifanya nisafiri kwa Gari kwenda Arusha.
Na Habari za ndani nilizozipata kutoka kwa mmoja wa Wafanyakazi wa ATCL ni kwamba Mkuu kwenye Kitengo cha pesa ni Mzembe na hakuna anayeweza kumwambia Chochote kwa sababu ni Rafiki Mkubwa wa Mkurugenzi Mkuu (David Mataka).Sakata la Kuahirishwa kuruka Ndege Nyingi Alhamis na Ijumaa ni matokeo ya Kukosa Mafuta,Kwani Kampuni ya BP imekataa kutoa tena Mafuta kwa sababu hawalipwi pesa zao kwa wakati,Kampuni hiyo ya BP inasemekana inawadai ATCL pesa nyingi kwa kukopwa Mafuta.
Uongozi wa Juu wa BP unadai kuwa Mkurugenzi wa ATCL anatumia Vibaya Urafiki wake na Viongozi wakuu serikalini kuliendesha Shirika hilo,kwani mwezi wa tano watu wa BP walipata note kutoka kwa katibu Mkuu Wizara ya Nishati na baadaye kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais,walipogoma kutoa mafuta kwenye ndege iliyokuwa inaipeleka Timu yetu ya Mpira Cape Verde.Hivi sasa hakuna mtu yeyote anayeongelea suala hili la Utata wa malipo ya Madeni kutoka ATCL,kila mtu yupo busy kwenye Maandalizi ya Harusi ya Mtoto wa Kike (Monalisa) wa Mkurugenzi Mataka.
Waungwana nafikiri sasa imefika wakati Tumpime Kiongozi kutokana na sehemu anayoongoza,ikiwa mtu anashindwa ku-deliver ni lazima aachie ngazi.Mataka aanze kuoyesha Mfano.Mapungufu yake yamekuwa mengi kuliko Mafanikio..
Nawaletea taarifa hii ambayo ingeliweza kulisaidia sana shirika letu la ndege kama ingefanyiwa kazi.
Jana ATCL wameshindwa kupata mafuta ya kurusha ndege zao na hivyo kushindwa kusafirisha abiria wao kwenda maeneo mbalimbali nchini.
Isome hapo chini .
Mkuu Kieleweke,
Nimeisoma hii tarifa yote uliyoambatanisha, lakini kwa uchungu kabisa ningependa kukufahamisha kuwa licha ya kuwa kamati iliundwa na wabunge maarufu kama Wah. Kaboyonga, mama Malecela, Dr. Mwakyembe, Lucy Owenya n.k., sidhani kama walifanya kazi nzuri.Kwa jinsi wanakamati walivyo na CV nzuri, nafikiri hili suala hawakuhangaika nalo kiuhakika, maana hata mwanafunzi wa degree ya pili pekeyake ukimpa miezi mitatu tu, anaweza kutengeneza ripoti nzuri zaidi ya hiyo waliyoiwakilisha bungeni. Ukiifananisha hii ripoti na summary tu ya ile ya ripoti ya Mwakiyembe-Richmond, ni sawa na sawa na kufananisha kazi ya mwanafunzi wa sekondary na ya wa chuo. Nafuu hii ingefanywa kuwa field work ya wanafunzi wa chuo kuliko hivi ilivyoundiwa kamati ya gharama kubwa ya bunge.
- Ripoti imetolewa Mei 2007. SAA wao walitoa notisi ya kuvunja mkataba March 2005. Mkataba wa GOT na SAA hatimaye ulivunjika August 2006. Lakini kamati badala ya kuijadili ATC as after mkataba kuvunjika na future yake, kwa asilimia kubwa, say over 90%, waliendelea kujadili ubabe wa SAA wakati wa ATCL na kidogo upuuzi wa GOT.
- Licha ya suala la ATC kukopa mafuta kuwa ni moja ya tatizo kubwa la madeni ya ATCL tokea 2006, kamati haikutoa wazo lolote kuhusiana na hili. Suala ambalo haitmaye ndio limeifikisha ATC hapa ilipo.
- Udhaifu wa uongozi wa ATCL kwa upande wa TZ nao umeongelewa kidogo sana kwenye ripoti. Ila cha kushangaza, hakuna msaada wowote wa kimawazo uliotolewa na kamati juu ya nini kifanyike.
- Conclussion zao zote hazina msaada wowote kwa ATC ya sasa. Karibu zote zinaangalia nyuma badala ya kutoa muongozo kwa shirika jipya la ATC. Shame on them.
Sidhani kama unaweza kusema CV zao ni nzuri kwa sababu tu ya Richmond! Ukiangalia ripoti ya Richmond, hakuna kipya walichokisema zaidi ya kile tulichokuwa tunakijua awali. Kama CV ni uboldness wa mwakyembe na uhodari wa kusoma basi nakubaliana na wewe ila kama CV ni jinsi ya kudadavua mambo na kutoacha shaka yoyte katika conclusions unazofanya, basi sidhani kama ripoti ya Richmond ina tofauti sana na hii. Zote zinaacha maswali magumu ambayo hayapatiwi majibu. Nitaishia hapa maana nadhani hoja hapa ni ATCL ambayo siku zote ndo kipenzi changu!
Mkuu Jobo,
Nakubaliana na wewe kuwa mengi ya yaliyokuwemo kwenye ripoti ya Mwakyembe tayari yalishakuwepo kwenye public domain, lakini at least waliweza kutengeneza conclussions ambazo zilikuwa zinaangalia mbele. Hii ya ATCL ni ubwabwa mtupu. Sio ripoti ya kufanyia kazi kw mwaka mzima na utitiri wa vichwa.
Anyway, ushauri wangu kwa ni kuwa;
- Wakurugenzi wote wa ATC kuanzia MD na wengineo wote, infaa wafukuzwe kazi na nafasi zao zitangazwe hadharani. Watu wenye sifa zao iwe ni waTZ au wageni waruhusiwe kuomba kazi, wachambuilwe na kuajiriwa kwa mikataba kwani sidhani kama tunao wabongo wenye elimu na uzoefu wa kila fani hasa za airline industry.
- Kipengele kimojawapo cha ajira zao iwe ni perfomance yao binafsi na ile ya shirika kwa ujumla.
- Wafanyakazi 300 kwa ndege sita ni mzigo mkubwa wa wazi kwa shirika. Sidhani kama Precission air wana zaidi ya wafanyakazi 100 ingawa wana ndege tisa.
- Ukaguzi wa mahesabu na uendeshwaji wa shirika ufanyike mara kwa mara na wabadhilifu au wazembe tu wa kawaida wachukuliwe hatua.

That will take 'mapinduzi' to happen.
Hakuna somo ambalo atc hawajapewa. anatakiwa mtu mpya na mambo mapya (mpya maana mpya sio mpya aliewekwa na watu wa zamani)
Sasa wamenunua hilo li Air Bus ambalo limezidi kurundika madeni kibao... watumie maji sasa kulirusha.. grrrrrrrrrrrrrrrr