Kwa mtazamo wangu mpasuko ndani ya CCM naona ni mgumu sana ( sisemi hauwezi kutokea) Tatizo kubwa la nchi yetu, CCM inashikilia livelihood ya maisha ya Watanzania wengi katika nafasi za juu, serikalini na hata katika biashara, Kujitenga na CCM ni kujifungia kitanzi chako mwenyewe! au kuwa kinyume nayo tu, ndio unayamaliza maisha yako hata bila kukutoa roho! Katiba ya Tanzania ilitengenezwa hivyo kwa makusudi kabisa!
Watanzania wengi wenye nafasi au uwezo wa kufikiri ambao labda wengeweza kuja na njia mbadala wa kuongoza nchi hii, hawana ujasiri wa kuchukua kujitenga na CCM, huu ni mfumo ambao ulitengenezwa kuanzia TANU mpaka CCM umewaweka watanzania wengi wenye mitazamo tofauti rehani! Na CCM inalijua hilo na inalitumia kikamilifu, rejea hotuba nyingi za Kikwete utaona statements kama hizi "nawajua sana watanzania". Na yoyote tu atakaye kuja na mawazo tofauti atabebeshwa majina mengi "anatumiwa na mabeberu" " analetea udini" " anavunja amani yetu" etc.
Kwangu naamini kabisa kuindoa CCM kwa njia ya kura kwa mfumo huu , ambayo umebebwa na kusimamiwa na watendaji wa serikali ambao uhai wao wa maisha kila siku unategemea CCM, ni kitu kisichowezekana kabisa, uchaguzi huu umeonyesha hivyo, lakini pia umetoa mwanga kuwa mwisho wa CCM utakuwa violent! Hii haikimbiliki kabisa! Naamini kabisa ni vigumu CCM kukaa na kujirekebisha! Na haina Uwezo huo! CCM wanajua wazi kuibadili Katiba kwa njia yoyote ni kujifungia kitanzi chao, na vilevile utafungulia mlango wa wazi wa kuuangalia Muungano upya, kwa CCM hiyo ni kama Imani ya dini! ambayo you cannot negotiate! Wanajua madhara yake!
Maandamano haya yameonyesha wazi ni njia ipi ya kuchukua kuibadili Nchi yetu! Ni njia mbayo CCM yenyewe wameilazamisha na ambayo kwa sehemu kubwa haina uwezo wa kui control!