Tumemshauri humu kazi ya kwanza baada ya kuapishwa ni healing the nation,
Kwa mujibu wa katiba yetu,akiishatangazwa,ndio ametangazwa,uchaguzi umekwisha,there is nothing anybody can do. Kitu cha kwanza baada ya kuapishwa,
1. atoe a general amnesty kwa wale wahalifu wote waliofanya ule uhalifu kwasababu japo ni wahalifu kwa maandamano yaliyoambatana na uharibifu wa mali wa kijinai, kwa wengine hawa vijana ni mashujaa wakombozi waliojitoa kuipigania nchi yao, asiwaadhibu. Tena CDF Mkunda aondoshwe, Wale the good ones waandikishwe JKT wachujwe, waajiriwe jeshini.
2. akubali serikali italipa fidia kwa kila uharibifu uliotokea kwasababu ni serikali yake imesababisha yote haya.
3. a heal the nation kwa kuwateua Lissu,Zitto,Mpina,na Mwalimu katika zile nafasi zake 10 za ubunge ili kuwapoza moto Gen Zii, mtu kama Lissu akisimama na kusema tulieni, vijana wanatulia.
4. Ashushe mabega chini,awe humble,aje down to earth, asiendelee kutambia urais wake wala u mimi ndie Amiri Jeshi, 5 days taifa limechafuka hakuna kauli ya CinC!
5. a wa disband wasiojulikana ambao ni 'wasiojulikana', na ni “wasiojulikana” kweli hawajulikani,akubali serikali yetu haina uwezo kuwabaini,aombe msaada wa kusaidiwa na yeyote,tukiwemo sisi waandishi wa IJ.
P
Tuangalie tlipojikwaa ila wengi tunaangalia tulipoangukia na kusahau tumefikaje na hulka ya huyo mtu anayepaswa kushusha mabega au ku heal the nation
Kwa watu wanaomfahamu na kwa kauli zake hadharani ni mama Haambiliki i.e Chura Kiziwi
JW limekuwa scapegoat lakini TISS ndio wenye dhamana kubwa ya kutoa taarifa na wamejaa humo JW na humu mitaani wakiwa na taarifa za kila mtu. Hakuna asiye julikana nchi hii hata humu mitandanaoni wote tunajulikana
Watu wa kumshauri wanamwambia anachotaka kusikia, "anaupiga mwingi"
Wazee kama Warioba ambao walijaribu kumsihi aongee na wapinzani wake walimshindwa na akaanza kuwananga yeye na JK kwenye msiba wa CD Msuya, naye ameamua kukaa pembeni
Viongozi wa dini hasa wa BAKWATA hawana moral authority ya kumwambia na wanashindwa kumueleza ukweli kwa sababu ni "mwenzetu" wakinufaika na mialiko ya futari na hafla za Ikulu
Hao wa dini nyengine ukitoa RC wengi wamekuwa compromised na misaada ya kifedha kwenye makanisa na taasisi za kidini wazozisimimamia, wanaogopa kukemea matukio yanayosababisha tofauti za kisiasa, kijamii, kidini, kikanda na kiuchumi
Mtu kama Askofu Shoo au Malasusa wa kukaa kimya kwenye situation kama hii?
JK alipaswa kuwa "stateman" akiwa kama Rais mstaafu aliyebaki hai badala yake anacheza na petty politics za CCM. Huko nje anaitwa kwenye migogoro kusuluhisha na kipindi chake aliweza kuwaita kina Lipumba, Lisssu na Mbowe kuepusha migogoro ya kisiasa. Nyerere alikuwa akiwasema pembeni na hadharani kina Mwinyi na Mkapa wakiwa ma Rais
It takes two to tango ila kwa yeye bado hata upande wa pili uwe tayari