Atakayeisoma namba ni yule mwenye kipato cha chini

Atakayeisoma namba ni yule mwenye kipato cha chini

Mimi nilimpa lowasa kura yangu na nishabiki wa chadema sana tu.ila swali nililojiuliza nikua hivi lowasa angeshinda uraisi kweli angeendesha inchi huku chadema wana viti vya ubunge 34.hiliswali limekua gumu sana. But ukweli nikua tumerudi nyuma hatuna moja kwa kuchagua mafisiem
 
Leo jamaa mmoja kakamatwa na traffic hana helement huku na la tshirt la umoja ni usindi nimechekaje.
 
Mbowe hawezi kuisoma namba. Ana biashara zake plus mshahara wa ubunge. Lowassa pia ana hela zake. Mbatia mhandisi pia mbunge. Tundu Lissu advocate. Ana hela zake. Kushangilia eti UKAWA watakoma ni ujinga.

Atakayeisoma namba ni yule ambaye akija hospita
li ukamwambia hela ya kumuona daktari ni 6000 anapanic anaanza kuwalaum madaktari. Anaeisoma namba ni yule mwenye kipato cha chini, bima ya afya hana, hata hela ya kumshonea mwanae uniform hana.

Anaeisoma namba ni yule ambaye hawez kuafford milo mitatu iliyo kamili kwa siku. Ni upuuzi kwa mtanzania wa manzese (asiyeweza kulipa ada ya shule ya 40k kwa mwaka) kusema Duni ataisoma namba wakati ana taaluma yake na pesa zake.

Unaeisoma namba ni wewe ambaye tokea umemaliza chuo ni miaka mitatu huna kazi (halaf kwa upumbavu unashabikia hapa kazi tu).

Unaeisoma namba ni wewe ambaye mtoto wako akiumwa mafua tu huwez kuafford dawa. Asilimia kubwa ya waliomchagua pombe ni ile 30% ya watanzania wanaoishi chini ya mstari wa umasikini (kipato cha siku kuwa chini ya dola za kimarekani 1.9.. sawa na sh 4000 hiv).

Hawa ndo wanaisoma namba, miaka 54 ya uhuru bado wanaishi gizani, bado hawawez kupata maji safi na salama... Halaf walivyo wanashabikia hapa kazi tu.. Kweli ni kazi..

Maana kushindia mlo mmoja kwa siku so mchezo, ni kazi kweli. Kumnywesha mwanao mwarobain kwa sabab huwez kumudu bei za madawa, so mchezo ni kazi haswa haswa.

Kama watanzania wenyewe ndo hawa ambao hawajitambui, WE HAVE A LONG WAY TO GO.
 
Miaka mitano sio mingi tutege macho na masikio yetu vizuri tuone viwanda vingapi vitafufuliwa na vingapi vitaanzishwa. Pia tutaona kila kijiji kikipata milioni 50 na mahakama ya mafisadi ikijengwa. Let's wait tym w'll tell.
 
Na bado wataendelea kukinga mikono kama Matonya (r.i.p) ilihali elimu bure hawataki
 
Kuna mtu alisema alishagakata tamaa na tanzania mim kupiga kura mpaka tuwe na tume huru isipopatikana basiiiii
Sipigi kuraaa
 
Kweli kabisa, mijitu mipumbavu kabisa hii......Lakini hata hivyo wengi walimchagua Lowassa kwa 62% CCM na liNEC lao wakapora usindi wake...

Walaaniwe CCM na NEC
 
Miaka mitano sio mingi tutege macho na masikio yetu vizuri tuone viwanda vingapi vitafufuliwa na vingapi vitaanzishwa. Pia tutaona kila kijiji kikipata milioni 50 na mahakama ya mafisadi ikijengwa. Let's wait tym w'll tell.
Mkuu maskini ambao wanaichagua ccm mimi siwaelewi kabisa yaani
 
Hata mimi siwezi kuisoma namba. Nina ajira yangu na watoto wangu na familia yangu inasavaivu bila shida.
 
Hasa ambao hospitali ya vuchaa imejengwa kwa yaani wangongo - Dodoma yetu hoyweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
57%hawataki elimu bure, Tanzania yangu mama weeee
 
Kusema kweli wengi tuliosimama hu Jf kupigania mabadiliko tunajitambua, tumeelimika na tunakipato cha uhakika. Tuliwapigania maskini ili nao wapate heshima inayowastahili kama binadamu sasa kama wamekataa tuwaache maana wameshazoea shida. But let's pray 4 our new leader whatever he is.
 
Kusema kweli wengi tuliosimama hu Jf kupigania mabadiliko tunajitambua, tumeelimika na tunakipato cha uhakika. Tuliwapigania maskini ili nao wapate heshima inayowastahili kama binadamu sasa kama wamekataa tuwaache maana wameshazoea shida. But let's pray 4 our new leader whatever he is.
Kweli mkuu, Magufuli is a good guy but akina Kikwete na ccm yao hawawezi kumuacha atende kwa maslahi ya taifa, lazima watamtuliza tu, hapo ndio shida inapokuja.
 
Pale shida au dhiki inapokuwa ndio maisha halisi hata ukijaribu kumwaonjesha maisha halisi hatokuelewa!

Mtu kazaliwa na akakua akinywa maji ya rangi ya maziwa, shuleni alikalia tofali/jiwe kwenye mavumbi, akiumwa ni either anywe mitishamba au ndg toka mjini ajitolee kugharamia matibabu yake!

Akibahatika kuja mjini kama housegirl au shamba boy hata kulala kitandani anaogopa keshazoea teremka tukaze, ngozi ya ng'ombe au mbuzi!! Au mwengine akija mjini kama mmachinga atatateseka kutwa nzima kwenye jua kali akitafuta riziki ambayo haitoshelezi mahitaji ya kimsingi...., na wakati mwingine kukimbizana na askari wa jiji ili mradi kila kukicha ni afadhali ya jana!!

Awamu iliyopita walihaidiwa maisha bora..., waulize kama hata maisha yao yaliboreka, kama ktk zahanati yao kuna dawa, je shule zina madawati.., je yeye binafsi ameona tofauti gani ya kipato/maendeleo binafsi ktk miaka 10 iliyopita.....? (Wengi nyuso zao zinaonekana kukata tamaa).

Kwa kifupi, hawaelewi wala kutambua kuwa wana haki ya kuwa na maisha bora na sio ufukara uliotopea, kushindia mlo mmoja tena wa kubahatisha, huduma mbovu za afya, kukosa ajira n.k.
 
Back
Top Bottom