Mbeya: Bibi ashikiliwa kwa tuhuma za kumuua Mtoto wa mwaka mmoja kwa kumkata kwa jembe

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia bibi mmoja aitwaye MALOGI LUOBELA [75] Mkazi wa Kijiji cha Ikoho Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa tuhuma za kumuua mjukuu wake aitwaye VISION ERICK mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitano kwa kumkata kwa jembe.

Kuzaga.JPG

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ameelezea kuwa Agosti 31, 2023 majira ya saa 4:30 asubuhi huko Kitongoji cha Mapinduzi, Kijiji cha Ikoho, Kata ya Maendeleo, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, mtoto VISION ERICK, mwaka mmoja na miezi mitano alifariki Dunia baada ya kukatwa kwa jembe kichwani na Bibi yake aitwaye MALOGI LUOBELO [75] Mkazi wa Ikoho.

Chanzo cha tukio hili ni mtuhumiwa alikuwa anachimba udongo ili kukandika katika nyumba na ndipo wakati anaendelea mtoto huyu alitambaa hadi eneo hilo bila mtuhumiwa kumuona kutokana na hali yake ya uono hafifu [upofu] na ndipo alimkata kwa jembe kichwani na kusababisha kifo chake.
 
Bibi kaua bila kukusudia

Bibi Uono wake hafifu

Mtoto kamfata bibi mwenyewe akiwa kwenye kazi zake
 
Mbeya hakupoi Yani Bado hatujaziba mfereji wa hela wanazo kwangua wahuni Bibi anamlima mtu.
 
Back
Top Bottom